VYAKULA MUHIMU SANA KWA SHINIKIZO LA DAMU AU PRESHA.

katika matibabu ya ugonjwa wowote vyakula ni muhimu sana kwani ndio vinaujenga mwili wetu.. kimsingi muonekano wa miili yetu huchangiwa sana na chakula tunachokula.
vifuatavyo ni vyakula ambavyo ni muhimu sana kutumika na wagonjwa wa presha ili kupunguza presha hiyo ya damu.
mboga za majani; uwepo wa chumvi nyingi au sodium kwenye damu ni moja ya vyanzo vikuu vya presha kua juu kwa wagonjwa hawa wa presha.
potassium husaidia sana kuondoa kiasi kingi cha sodium mwilini au chumvi na kupunguza presha.
mboga za majani zenye potassium nyingi ni kama bamia, chainisi, spinachi, na mchicha ni nzuri sana kwa wagonjwa hawa.

berries; haya ni aina ya matunda ambayo yana kemikali inayoitwa flavonoids ambayo imethibitika  kuzuia ugonjwa wa shinikizo la damu na kushusha presha kwa wagonjwa hawa.
Mara nyingi hupatikana sana kwenye super market kubwa hapa nchini.
                                                                  

samaki; samaki ni chanzo kizuri cha protini kwenye mwili wa binadamu, samaki wa aina ya salmon kama anavyoonekana kwenye picha hapo chini ni chanzo kizuri cha kemikali ya omega 3 ambayo husaidia kushusha shinikizo la damu kwa kupunguza lehemu au cholestrol, na kuponya mishipa ya damu.              
                                    
mbegu; mbegu ni chanzo kizuri cha madini ya pottasium na magnesium ambayo husaidia kupunguza kiasi kikubwa cha chumvi mwilini na kupunguza presha.
Mbegu za maboga na alizeti ni nzuri zikiliwa na wagonjwa hawa.
                                              

vitunguu swaumu; hivi vina kiasi kikubwa cha kemikali ya nitric acid ambayo inafanya kazi ya kupanua mishipa ya damu, hii huongeza nafasi kubwa kwa ajili ya kupitisha damu vizuri kwenda sehemu mbalimbali za mwili bila kuongeza shinikizo la damu.
                                                                

ndizi mbivu; kama ilivyo kwa mboga za majani, ndizi mbivu ni muhimu sana kwani zina kiwango kikubwa cha potassium ambayo hutumika kuondoa chumvi nyingi mwilini ambayo husababisha presha kupanda.                         

                                                
tangawizi; hii hufanya kazi ya kulainisha damu kwa kupunguza uzito wake(blood thinner), na kupunguza shinikizo la damu kwa kiasi kikubwa sana.
unaweza kutumia unga wa tangawizi kwenye chai yako kila siku badala ya kutumia majani ya chai ambayo tunajua hayana faida yeyote.
                                                      
CREDIT:SIRI ZA AFYA BORA

Post a Comment

Previous Post Next Post