Jinsi ya kupima mimba kwa njia ya mkojo (UPT)Kipimo cha mimba kwa njia ya mkojo kimekuwa kikiuzwa katika maduka mbalimbali ya dawa za binadamu, lakini cha ajabu wauzaji wa kipimo hiki miongoni mwao wamekuwa wakikiuza pasipo kutoa maelezo kamilifu ya namna ya kukitumia na ni kwa muda gani wa ujauzito uweza kutoa majibu halisi tangu kuhisi kuwa na ujauzito.

Leo katika safu hii ntakufahamisha namna sahihi ya kutumia kipimo hiki na utungaji wa mimba hadi muda wa kupima mimba kwa kutumia kipimo hiki na kubaini matokeo halisi.Baada ya mimba kutungwa embryoni husafiri kwenya mfereji wa uzazi na kisha hujipenyeza katika ukuta wa ndani wa mfuko wa uzazi . Hali hii huitwa upenyezaji (implantation ) huanza siku 6 na humalizika siku 10-12 baada ya kutunga mimba. Chembe hizi za embryoni changa huanza kuzalisha homoni huitwao “korionik gonadotropin" au “HCG" ambazo hutumika katika yipimo yya mwanzo yya mimba. HCG hutolewa katika mkojo hiyyo kuwa msingi wa kipimo cha mimba kwa njia ya mkojo.

Kipimo hiki hujulikana kama Urinary Pregnancy Test (UPT). Wanawake wengi hutumia njia hii ili kutambua iwapo wana ujauzito ambapo Kipimo hiki huweza kubaini iwapo mwanamke ana ujauzito kuanzia siku 8 toka mimba kutengenezwa.

Jinsi ya kutumia kipimo cha mimba kwa njia ya mkojo (UPT)

  1. Weka mkojo kwenye chombo kikayu.
  2. Tumbukiza kipimo mpaka kwenye mstari kwa dakika 1 halafu kitoe.
  3. Angalia mabadiliko kwa muda usiozidi dakika 5, Ukitokea mstari mmoja basi hakuna mimba na Ikitokea mistari miwili inawezekana kuwa na ujauzito na kama hakuna mstari wowote inamaanisha kipimo hicho kina itilafu.
Ili kubaini undani zaidi na kuthibitisha juu ya kupimo hicho unapaswa kwenda katika kituo cha afya kwa ajii ya kipimo zaidi na ushauri wa Daktari.
kipimo cha mimba kwa kikionyesha itilafu (cha kwanza), mwenye mimba(cha pili) na asiye na mimba (cha tatu)
kipimo cha mimba kwa kikionyesha itilafu (cha kwanza), mwenye mimba(cha pili) na asiye na mimba (cha tatu)
 Kama unataka kujua siku ya makadirio ya kujifungua bonyeza hapa

1 Comments

Previous Post Next Post