MAGONJWA YA MENO: AINA, CHANZO, DALILI & TIBA

UTANGULIZI – YAJUE MATATIZO YA MENO

Matatizo ya meno ni shida au magonjwa yanayohusiana na meno, karibia matatizo yote ya meno yanatokea baada ya bakteria na wadudu wengine kuwepo mdomoni, hii hufanya mtu kuwa na maumivu makali kwenye meno na mpaka kupelekea kutoa damu au halufu mbaya na kuathiri meno. Matatizo mengi ya meno yanazuirika na hutibika.

Katika maeneo mengi watu wengi wanatatizo la meno ila wanatofautiana wengine wanatatizo dogo wengine pia wanatatizo kubwa, tunawasauri watu wawe na tabia ya kuchunguza meno yao ili kujilinda na matatizo ya meno, tibu tatizo mapema ili usikuze tatizo, usipotubu tatizo basi meno uendelea kuaibika na mtu anaweza kuwa kibogoyo.

AINA ZA MAGONJWA YA MENO

Mdomo una magonjwa mengi ila meno ndio tatizo kubwa sana na ndio linaweza kuleta na matatizo mengine, aina za magonjwa ni kama;

  1. Meno kutoboka – Hili ni tatizo linalotokea kwenye meno kwa kuwepo kwa bakteria kwenye meno na kuharibu meno, bakteria hao wanaweza kutokana na kuwepo kwa mabaki ya vyakula hasa vyenye sukari nyingi. Mabaki yasipoondolewa bakteria huzalisha acidi ambayo ndio huharibu meno na kutengeneza vijitobo.article_cavities2
  2. Meno kuvunjika – Hili ni tatizo ambalo huwatokea watu wakionekana meno yao kuna baadhi na vipande kutoonekana, jino laweza kuwa nusu au robo tatu, mara nyingi hili sio tatizo hatari halina madhara makubwa kwakuwa haliathiri fizi ila linaweza kumnyima mtu uhuru wa kucheka na pia ulimi ukigusa unahisi kama ni kitu chenye ncha.a03b132b06df25c18ed12108fb5e1411
  3. Meno kusagika au kupungua kimo – Hili tatizo hutokea ukiwa umelala, hata mchana ukiwa na mawazo, hasira au hisia ambapo meno hugusana na kusagana. Meno huweza kupungua kimo na kuisha hii hutokea kwa mda mrefu kidogo, meno yakisagika na kupunguwa kimo husababisha maumivu ya meno na kubadilika rangi.teeth+wear
  4. Tatizo la fizi – Hili ni tatizo katika fizi kuna kuwa na maumivu, kama vidonda au kutokwa damu, kuwa na usaa au uchafu. Mara nyingi hutokana na bakteria wanaokuwa kwenye mabaki ya chakula usipoyaondoa bakteria wanaanza kuvamia fisi na kuziharibu. Mtu mwenye hili tatizo hutoa harufu mbaya.signs-of-gum-disease
  5. Meno kuharibika, fizi kuachia na kulegea – Hili tatizo ni pale meno yanapoonekana sio ya kawaida; yaani yanakuwa yamebadilika rangi, fizi kuharibika, fizi kupungua, fizi kutoka damu na meno kulegea. Hili ni tatizo ambalo laweza kuwa kubwa na kutotibika.110126-F-0000W-001-750x410
  6. Meno kufa ganzi na kushindwa kuhisi – Hili ni tatizo huwakuta wengi katika mazingira ya baridi sana au joto sana, pia wakila baadhi ya vyakula vyenye uchachu, vyenye sukari na vingine. Tatizo hili ni dalili za kuharibika kwa jino ndani au nje
  7. Harufu mbaya na kupumua vibaya – Hili tatizo hutokea kwa mtu kutoa harufu mbaya mdomoni ambayo huwakela watu wengi, hii hutokea pale anavyokuwa na mabaki ya vyakula kwenye mdomo, kutofanyia usafi meno na mdomo pia, kuwa na tatizo la meno au mdomo.
  8. Mhozo au Utando mdomoni – Hili ni tatizo ambalo mdomoni huwa na weupeweupe usioeleweka kama ute, mara nyingi huwatotea watu wasio na kinga imara hasa wenye matatizo ya kiafya kama kisukari, UKIMWI, Kansa (Saratani), Asthma. Hii hali huondolewa na dawa.
  9. Meno kuwa na rangi ya njano, kaki au kahawia – Hili tatizo limeonekana kuchukua baadhi ya maeneo, ambapo idadi kubwa ya watu wameonekana wakiwa na meno yenye rangi inayoendana. Hii ni kwasababu ya vyakula na maji ya kunywa yanayopatikana maeneo hayo kuwa na uwingi wa aina flani ya madini hasa Fluoride.kenya teeth

CHANZO CHA MAGONJWA YA MENO

Chanzo cha magonjwa ya meno kwa asilimia kubwa ni mitindo ya maisha tukimaanisha usafi, ulaji, mazingira na tabia mbalimbali, mambo yanayoweza kukusababishia kupata matatizo ya meno ni kama;

  1. Kuto kusafisha mdomo pamoja na meno
  2. Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi
  3. Kuto kupata tiba ya kisukari na ugonjwa wa moyo
  4. Kuvuta sigala
  5. Kuwa na magonjwa yanayopunguza kinga ikiwemo na UKIMWI
  6. Kubadilika kwa baadhi ya homoni
  7. Umri
  8. Utumiaji wa madawa yenye kemikali nyingi huharibu mfumo wa vimiminika vinavyofanya mmeng’enyo
  9. Historia magonjwa yanayoambatana na meno katika familia
  10. Mazingira

DALILI ZA MTU MWENYE TATIZO LA MENO

Mara nyingi dalili hujionesha wazi wengi hujijua kuwa tayari wanatatizo na mara nyingi huwa haiitajiki vipimo, zaidi huhitajika uchunguzi kujua chanzo, dalili zake ni kama

  1. Meno kuuma wakati wa kula au mda wa baridi au joto
  2. Kutokwa na damu kwenye fizi
  3. Meno kuanza kulegea na kuachana na fizi
  4. Kutoa harufu mbaya mdomoni, hii huonesha kuna tatizo
  5. Meno kubadirika rangi mfano nyeusi, njano, kahawia na rangi zingine zisizo za kawaida
  6. Fizi huwa nyekundu kama damu ikiwezekana kuna na vidonda
  7. Mdomo kuwa mkavu
  8. Meno kufa ganzi
  9. Meno kuchomoka au kutikisika

JINSI YA KUEPUKA MAGONJWA YA MENO

  1. Ondoa mabaki ya chakula kwa kusukutua mdomoni na maji baada ya kutoka kula pia Kunywa maji mengi dakika 30 baada ya kutoka kula
  2. Safisha meno yako hata mara mbili kwa siku
  3. Punguza mawazo
  4. Usivute sigara
  5. Punguza au acha kunywa pombe
  6. Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali, vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi

TIBA YA MATATIZO YA MENO

Matatizo ya meno linatibika kufuatana na mda wa tatizo, mara nyingi wagonjwa wamekuwa wakizalau dalili za tatizo la meno na kudhani kuwa hakuna madhara makubwa.

Tuna dawa ya kutibu Meno ambayo ni ya asili isiyo na kemikali ambayo hufanya mtu kupona na kuimarika kabisa. Dawa hiyo hutibu kwa mda  kulingana na mda wa tatizo, tatizo halirudi tena maana huondoa chanzo pamoja na ugonjwa sio kituliza maumivu,  ukianza kutumia ndani ya wiki moja huanza kutibu na  huonesha mabadiliko, pia mgonjwa anapewa mfumo wa maisha ambao inatakiwa autumie kwasababu kuna mtindo wa maisha unaendelea kuongeza tatizo pia kuna mtindo unapunguza hatari ya ugonjwa.

Tunamshukru Mungu kwa uumbaji wake na kutupa dawa ambazo alizileta ili kutuimarisha na kutuponya, Mungu hakuumba dawa nyingine zaidi ya mimea na vitu vingine vya asili, japo wengi hudharau. Mungu tunaomba utuokoe na kutuponya.

Post a Comment

Previous Post Next Post