hii ni njia ya kitaalamu ya kuondoa ngozi ya juu ya uume ambayo mwanaume huzaliwa nayo ili kuongeza ufanisi katika tendo la ndoa, hufanyika kwa njia za kitaalamu mahospitalini au kwa njia za kiasili.hakuna umri mbaya wa tohara japokua ni vizuri mtoto akafanyiwa tohara kabla hajabalehe yaani miaka 10 ili akianza mahusiano awe tayari amepata tohara.
kutailiwa au tohara ni utamaduni wa muda mrefu ambao ulikuwepo kabla hata ya kuja kwa yesu, utamaduni huo pia ulikuepo hapa africa na kulikua na makabila mbalimbali ambayo yaikua yakiongoza zoezi hili kulingana na tekinolojia waliokua nayo kwa wakati huo.lakini baadhi ya makabila ya hapa afrika na nje ya africa walikataa utamaduni huo na ukipita maeneo yao utagundua hilo.mfano watu wengi wa mikoa ya iringa na mbeya hawajatahiriwa na hii inawezekana hakuna mila ya tohara kwenye jamii yao.lakini pamoja na hayo yote kuna madhara makubwa sana ya kiafya ya kutotailiwa kama ifuatavyo.
hatari ya magonjwa ya zinaa na ukimwi; utafiti unaonyesha kutailiwa tu kunazuia ukimwi kwa zaidi ya asilimia 80 kwani virusi ambavyo ni rahisi sana kunasa kwenye ile ngozi laini ikichanika kidogo,hukosa pa kwenda lakini pia kama nilivyosema hapo juu mikoa ya iringa na njombe inaongoza kwa maambukizi ya virusi na sababu kubwa ikiwa hiyo ya kutopata tohara.
huleta kansa ya kizazi; mwanaume ambaye analala na mwanamke ambaye hajatahiriwa anakua kwenye hatari kubwa ya kumusababishia kansa ya mlango wa uzazi mwanamke husika hii ni kwasababu anaweza kubeba virusi vya kansa hiyo kitaalamu kama human papiloma virus kutoka mke huyu kwemda mke mwingine.
husababisha magonjwa ya njia ya mkojo; magonjwa ya mkojo uti huweza kusababishwa na uchafua ambao hujificha ndani ya uume na huweza kupita katikati ya tundu la uume hadi kwenye kibofu cha mkojo na kusababisha madhara makubwa wakati mwingine ugonjwa huu hufika mpaka kwenye figo na kuliharibu.
husababisha kansa ya uume; utafiti unaonyesha kansa ya uume iwewashambulia watu wanaume wengi ambao hawajatailiwa kuliko wale waliotailiwa.. hii ni kutokana na uwekaji wa uchafu kwenye ile ngozi ambayo huondolewa kipindi cha kutailiwa.
hupunguza sana uwezo wa mwanaume kujiamini; wanaume ambao hawana tohara hua ni waoga sana wakienda mijini kwani wanahofia kugundulika na wanawake iwapo wataingia kwenye mahusiano lakini pia wanafunzi ambao huenda kuanza sekondari bila kutahiliwa huishi maisha magumu sana ya kujitenga na wenzao kwenye mabafu ya shule.