Baba na mama wanaweza kukomesha kuharibika kwa mimba?

Baba na mama wanaweza kukomesha kuharibika kwa mimba?
Kiu ya kupata mtoto wa kumzaa mwenyewe ndio hamu ya mabinti wengi pindi wanapo funga ndoa. Lakini si kiu ya mabinti pekee kwani hata wazazi huwa na hamu kubwa ya kupata wajukuu.
Na hapa nazungumzia wazazi wote wa mwanamke na wa mwanaume. Lakini kuharibika kwa mimba ni mzimu unao sumbua wanawake wengi katika miaka ya hivi karibuni.
Kesi za kuharibika mimba zamani ilikua ni jambo la kifamilia zaidi, na si jambo ambalo lilikua lina elezewa waziwazi. Hata hivyo lilikua si jambo ambalo linatokea mara kwa mara au ya wezekana ni kwa sababu lilikuwa halizungumziwi. Wakina mama walipenda kufanya siri hata ikitokea biti amepatwa na tatizo hilo.
Katika kipindi hiki ambapo mitandao ya kijamii imepelekea watu kuweka wazi maisha yao binafsi,mazungumzo juu ya kuharibika kwa mimba ni moja kati ya mada kuu zinazo zungumzwa zaidi na wanawake.
Akina mama waliojigunguaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAkina mama waliojigungua
Baadhi yao hata huweka wazi majonzi yao kupitia mitandao ya kijamii au katika kurasa maalumu zinazo husika na ushauri wa masuala ya kina mama kama vile Active-mama na nyingine nyingi.
Baadhi huweka wazi ili kupata faraja hasa wanapo sikia habari za watu wengine ambao awali walipata hiyo changamoto ya kuharibikiwa mimba lakini baadaye walifanikiwa kupata watoto.

Mitazamo ya watu

Hata hivyo kumekuwa na minongono mbali mbali juu ya sababu zinazopelekea mimba kuharibika. Mara nyingi wanawake ndio wanao nyooshewa vidole kuwa wao ndio wenye mapungufu na kupelekea mimba kuharibika. Hali inayopelekea baadhi hata kukimbiwa na waume zao.
Asilimia hamsini mpaka sabini uharibifu wa mimba unao tokea katika awamu ya kwanza yaani first trimester husababiswa na matatizo ya vina saba vinavyoumba yai ama mbegu ya baba.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAsilimia hamsini mpaka sabini uharibifu wa mimba unao tokea katika awamu ya kwanza yaani first trimester husababiswa na matatizo ya vina saba vinavyoumba yai ama mbegu ya baba
Miongoni mwa sababu zingine zinazo tajwa ni pamoja na huenda mwanamke alitoa sana mimba akiwa shule, kurogwa yaani ushirikina, mwanamke pia hutajwa kuharibu mimba kwa makusudi, kula vyakula visivyotakiwa kwa wajawazito, mwanamke kupigwa na mume, kufanya kazi ngumu na sababu nyingine nyingi.
BBC imezungumza na mwanamama Zawadi, yeye anasema kwa miaka takribani kumi amekuwa akihaha kutafuta mtoto wake mwenye.
"Sijakata tamaa naaamini ipo siku nitabeba mwanangu, maana nimehangaika sana kila mtu ananipa ushauri wake ndugu wa mume wanahisi nilikuwa muhuni wakati mwanafunzi , marafiki wanahisi nimerogwa maana mume yeye alikuwaga na mtoto hko nyuma ila mie najua wakati wa Mungu waja," anasema Bi Zawadi
BBC imezungumza na Dokta Calman Living bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi hospitali ya taifa Muhimbili, anasema kuwa kuharibika kwa mimba kumegawanyika katika awamu mbili, awamu ya kwanza na ya pili husababishwa na sababu mbali mbali kwani baba na mama wote hu usika katika hilo.
Maandalizi kwenye chumba cha kujifungulia akina mamaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMaandalizi kwenye chumba cha kujifungulia akina mama
" Asilimia hamsini mpaka sabini uharibifu wa mimba unao tokea katika awamu ya kwanza yaani first trimester husababiswa na matatizo ya vina saba vinavyoumba yai ama mbegu ya baba.
Inawezekana kwamba mbegu ya baba au lile yai la mama likawa halina tunaita chromosome za kutosha kuungana na kuwiana kwa hiyo yule mtoto anaweza akawa na tatizo fulani na kupelekea mimba kuharibika.
Sababu nyingine pia unaweza kuta yai la mama au mbegu ya baba inakosa kiini cha uhai kwa hiyo mimba inatungwa lakini inakuwa haina uhai inaharibika," dokta Calman anaiambia BBC.
Hata hivyo Dokta Calman anataja maradhi mbali mbali yanayo sababisha kuharibika kwa mimba.
" Kwa sasa kuharibika kwa mimba ni jambo lililo wazi zaidi kwasababu idadi ya watu imeongezeka na watu wengi sasa wana fursa ya kufika katika vituo vya afya tofauti na zamani. Vile vile tukiangalia mfumo wa maisha wa zamani na sasa ni tofauti kwa mfano utumiaji wa vilevi na maisha tu kwa ujumla kuto kufanya mazoezi hali zinazo pelekea maradhi mbali mbali," anasema docta Calman.

Baadhi ya maradhi yanayopelekea kuharibika mimba

•Unywaji pombe kupita kiasi
•UTI ikiwa kali
•Sukari kuwa juu sana
•Shinikizo la damu
•Malaria kali
Hata hivyo Dokta calman amefafanua sababu ya kina mama wengi kuambiwa wapimzike na kutobeba vitu vizito.
"Uwezo wa kushika mimba anao lakini lile yai uwezo wa kusapoti hiyo mimba unakua haupo, kwa hiyo huyu mama mbali na kumpa dawa za kuisapoti hiyo mimba atahitaji mapumziko mpaka mimba hiyo iwe na uwezo wa kujitegemea huenda mpaka miezi minne.
Wengi wenye matatizo hayo unakuta alisha wahi kupoteza mimba ya kwanza ya pili kwa hiyo labda hii ya tatu anayo ipata ndo akagundua kuwa kuna tatizo na matibabu yake yakajumuisha bedrest. Kuna mimba nyingine inatoka katika awamu ya pili ya mimba unakuta shingo ya kizazi haina uwezo wa kuhimili uzito wa mimba.
Huyo mama atahitaji kushonwa na kutegemeana na ukubwa wa tatizo atahitaji complite bedrest," anasisitiza dokta Calman.
Hata hivyo Daktari huyo mtaalamu wa masuala ya wanawake anasisitiza juu ya mwanamke na mwanaume kufanya vipimo maalumu kwani matatizo mengine ya mimba huanzia kwa baba.
Aliyekuwa rais wa Marekani akiwasalimia wanawake wajawazito hospitali ya wilaya ya Meru alopofanya ziara nchini Tanzania mwaka 2008Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAliyekuwa rais wa Marekani George Bush akiwasalimia wanawake wajawazito hospitali ya wilaya ya Meru alopofanya ziara nchini Tanzania mwaka 2008
"Inapaswa kabla ya kuwa mjamzito nenda kliniki utapewa zile supliment miezi mitatu kabla pamoja na ushauri na vipimo vya maradhi mbali mbali mfano sukari na hata magonjwa ya zinaa.
Baadhi huzoea kuamini tatizo ni la mwanamke wakati Wengine tatizo huanzia kwa baba mfano kwenye ku match blood group hapa utakuta mimba zinaharibika kuanzia miezi saba au nane na hata mtoto anapozaliwa anakuwa anapata shida hapa unakuta blood group ya baba na mama haziendani hapo huwezi mlaumu mama ndio mwenye shida, inabidi baba aelewe tu yeye ndio sababu.
Unakuta mama kapima vipimo vyote viko sawa na hapati mimba daktari anamshauri mama amwambie mumeo aje baba hataki kuja sasa pale kwa sababu anaamini yeye anauwezo wa kufanya kile kitendo basi uwezo pia wa kumpa mwanamke mimba upo wakati sio sahihi," anasisitiza Dokta Calman
Daktari huyo bingwa amemaliza kwa kusema ukijiandaa mapema yaani mimba ukii panga basi hata haya matatizo si rahisi yakatokea.

Post a Comment

Previous Post Next Post