Ni kwa karne nyingi sana tangu watu wa jumuiya ya usovieti kuanza kutumia virusi kama dawa ya kutibu magonjwa ya backteria. Na kwa taarifa yako nchi ya Georgia mpaka leo inatumia virusi hao kama dawa kuliko hata madawa ya kawaida yanayotumika kwe nchi nyingine za ulaya na kote duniani.
Picha ikionyesha mwingiliano wa bakteriofagi, bakteria na watu |
Virusi hao huitwa bakteriofagi (ama bacteriophage kwa kiingereza bofya hapa kusoma zaidi), hawa vijidudud kama ilivyo kwa binadamu hupata magonjwa ya virusi basi na bakteria hupata magonjwa pia. hushambuliwa nao na ndio maana wanatumiwa na wanasayansi kuweza kumaliza magonjwa yasababishayo na bakteria.
Kwanini virusi hawa hutumika pale madawa yanaposhindwa?
Kiuharisia nchi nyingi bado hazijaapprove matumizi ya bakteriofagi mpaka sasa lakini nchi zilizoendelea zimeruhusu matumizi yake pale ambapo madawa yameishia yani hayawezi kutibu wadudu sugu.
Ni upi ufanisi wa virusi (bakteriofagi) hivi?
Kwa namna jinsi inavyoelezwa virusi hivi vina ufanisi wa hali ya juu sana.kwqni huweza kujigeuza na kuzaliana hili mradi viweze kuwashambulia bacteria husika.
Je ni upi mtazamo wa watu kuhusiana na virusi (bakteriofagi) hivi?
Watu wengi huhisi Kila kirusi ni adui wa afya zao bila kujua Wana virusi zaidi ya mamilioni katika miili Yao ambavyo havijawai wadhuru tangu uchanga Hadi wamekua. Mpaka sasa hakuna madhara yaliyooneka kutokana na virusi hivi hivyo vinaaminika kuwa salama hata kuliko madawa ya kawaida.
Kwanini wanadamu waliacha kutumia virusi (bakteriofagi) hivi baadae ya ugunduzi wa madawa?
Ugunduzi waadawa ulionekana una faidi kwani madawa yalikua na uwezo wa kuangamiza bacteria wengi kwa wakati wakati virusi hawa huwa Na bacteria wa aina moja ambaye ndiyo adui. Kwa maana kama mtu ana magonjwa ya bacteria tofauti atahitaji mchanganyiko (Cocktail) wa virusi tofauti kupambana navyo.
Kwanini wanasayansi wanarudi kwenda kutumia virusi (bakteriofagi)?
Virusi ni viumbe hai kwa maana hiyo vina uwezo wa kubadilisha njia za kupambana na adui mara kwa mara bila mwanadamu kuhusika. Wakata madawa ya kawaida hayawezi Fanya ivo kwa maana inapotokea Kuna bacteria sugu kama wale wa mfumo wa mkojo (UTI) kuna uwezekano was mtu kuto kupona kama atatumia madawa ya kawaida.
Tatizo LA magonjwa sugu ya bacteria lipoje duniani?
Wanasayansi wanakadiria endapo binadamu wataendelea na matumizi ya madawa kama ilivyo sasa kufikia 2050 watu watakufa kwa magonjwa sugu yasiyotobika kuliko kitu kingine chochote kinachoweza kusababisha uhai kutoweka. Bacteria wanakuwa sugu kwa madawa Kila siku kadri madawa uanavyotumika. Pia wizara na mashirika mbali mbali yameshatolea taarifa kuhusu magonjwa haya yasiyosikia dawa. soma zaidi bofya hapa
Asante kwa kusoma chapisho letu unaweza kutoa maoni yako hapo chini na usisahau kufollow blog hii fwenye ukurasa wetu wa facebook