Usugu wa vimelea vya magonjwa


Wananchi waaswa kuacha kutumia hovyo dawa za vijiua sumu (antibiotic)kwa matumizi ya kibinadamu,mifugo na mimea  kwani husababisha usugu wa vimelea vya magonjwa.

Wito huo umetolewa na shirika la Food and Agriculture Organization of the United Nations (FAO) wakati wa warsha ya Siku mbili iliyotewa kwa waandishi wa habari mjini Dodoma.

Warsha hiyo pia ilishikisha wadau mbalimbali kutoka wizara ya mifugo na uvuvi,wizara ya Afya jinsia wezee na watoto,wizara ya mazingira ofisi ya makamu wa Rais, mamlaka ya udhibiti wa chakula na dawa(TFDA)Wizara ya kilimo kutoka Zanzibar na maprofesa kutoka chuo  kikuu  cha kilimo cha (SUA) pamoja na msajili wa baraza la vetenary Tanzania(VCT).

Wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo Bachana Rubegwa ambaye ni Mratibu wa TAIFA , chini ya mradi wa  Fleming Fund unaohusika na kupambana na usugu wa vimelea vya magonjwa  alisema kuwa usugu wa vimelea vya magonjwa vimekuwa ni janga la kitaifa,na pia limekuwa likisababisha vifo vingi duniani.

Alisema Usugu huu wa vimelea vya dawa husababisha Vifo vya magonjwa laki 7 kwa mwaka duniani na inakadiriwa ifikapo mwaka 2050 takriban watu million 10 watakuwa wanapoteza maisha kila mwaka.

" kama takwimu zinaonyesha ukubwa huu wa tatizo je kwa Tanzania tutakuwa tunapoteza watu wangapi kila mwaka kutoka na matumizi haya mabaya ya dawa za vijiua sumu" alisema bachana.

Aliongeza kazi kubwa ya FAO  kwa kushirikiana na shirika la Afya duniani (WHO) pamoja na shirika la wanyama duniani(OIE) ni kuhakisha matumizi mazuri ya dawa za viua sumu inatumika vyema katika makundi yote matatu ya Binadamu,Mifugo na Mimea lengo ikiwa ni kupunguza usugu wa vimelea vya magonjwa kutokana na utumiaji mbaya wa dawa.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi kutoka Wizara ya Kilimo na Uvuvi Mkurugenzi wa Utawala na Lasilimali watu Selina Lyimo alisema kwa sasa kumekuwa ni vigumu kutibu magonjwa yaliyopo kutokana na usugu huu wa vimelea vya madawa  na matumizi mabaya ya viua sumu kwa binadamu, mifugo na mimea.

Alisema tunatakiwa kutumia njia mbadala ya chanjo ili kupunguza usugu huu ma vimelea vya madawa na hapa tunaweza kuwa salama.

Bedan Masuruli ni Msajili wa Baraza la Vetenary Tanzania (VCT) alisema kuwa wafugaji wanapaswa kufuata kanuni bora za ufugaji ili kuepukana usugu wa vimelea vya magonjwa kwa wanyama na kuleta madhara kwa watumiaji wa nyama hizo.

"Wafugaji wengi wamekuwa wakiwapa wanyama dawa bila ya kujua uzito wa mnyama na mnyama anaweza kupewa dawa Leo kisha akachinjwa na nyama yake kuliwa.

" kikawaida mnyama akipata dawa anatakiwa akae siku saba ndiyo anaweza kutumika kama chakula au kama ni ngombe anatakiwa akipewa dawa maziwa yake pia yasitumike kwa kipindi chicho cha Siku saba.

" kama ni kuku Naye anapo patiwa dawa anatakiwa kutoliwa kwa kipindi hicho cha Siku saba hata mayai yake pia hayatakiwi kutumika ndani ya Siku hizo saba lakini tumekuwa tukienda kinyume na kanuni bora za ufugaji.

"Na kutokana na sababu hii wanyama wengi wanakuwa na usugu wa vimelea vya magonjwa na kuleta madhara pia kwa mwanadamu". Alisema masuruli.

Naye  mtaalamu wafamasia kutoka wizara ya Afya jinsia wazee na watoto Edgar Basheka alisema ipo miongizo inayo elekeza juu ya matumizi ya dawa ambayo inatambulika kisheria.

Alisema katika miongozo hiyo inaelekeza vyema matumizi sahihi ya dawa za viua sumu pamoja na uuzaji wake katika maduka ya dawa muhimu.

" wauzaji wa dawa wote wakizingatia uuzaji wa dawa vizuri uwezekano wa kupu guza usugu wa vimelea vya magonjwa upo kwa kiwango kikubwa" alisema basheka.

Iskari Fute ni mwanasheria kutoka mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) alisema sheria zipo ambazo zina ainisha juu ya matumizi ya dawa na kusema kama sheria hizo zikifuatwa basi tatizo la usugu wa vimelea vya dawa litapungua kwa kiasi kikubwa .

Alisema kuwa sheria ambazo zipo zinatumilka katika bara la  Afrika na zipo sheria pia za Afrika ya mashariki alitolea mfano baadhi ya sheria ambazo zipo kitika katiba kama sheria ya dawa ambayo IPO katika ukurasa wa 319 katika katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Post a Comment

Previous Post Next Post