Macho kuwasha na kutokwa na machozi (conjuctivitis)
Huwakumba zaidi watoto wa umri kati ya miaka 5 -15 ambao hupendelea kucheza sehemu za vumbi au kwenye muangaza mkali (pwani yenye mchanga mweupe sana) Watu wazima wenye kufanya kazi kwenye viwanda vinavozalisha vumbi, na wenye pumu ya muda mrefu.
Dalili
Macho kuwasha (Nuru ya macho haipungui) Macho kubadilika rangi (kahawia) Kutokwa na machozi mengi (sana) Kushindwa kuangalia kwenye muangaza mkali
Matibabu
Kusafisha macho mara kwa mara kwa maji safi. Kutumia dawa kwa maelekezo ya daktari
Kinundu katika mfuniko wa juu au chini wa jicho
Kinundu kisichouma
Mara nyingi hupona chenyewe au unaweza kukikanda kwa maji ya uvuguvugu. Kisipopona au kitakapokuwa kikubwa huhitaji upasuaji mdogo.
Tags:
MACHO