MADHARA YA MSONGO WA MAWAZO (STRESS)

Image result for STRESSMSONGO WA MAWAZO (stress) ni hali ya maumivu au mfadhaiko wa kihisia au kisaikolojia unaotokana na hali, tukio au jambo ambalo ni gumu sana au lenye changamoto kubwa.

Mara nyingi tunatumia msongo wa mawazo au msongo wa mawazo pale ambapo mtu anajisikia au anaona kama vile kila kitu kimekua kigumu…tunasema maji yamefika Shingoni…yaani too much
Ni pale ambapo mtu amezidiwa na hajui kama ataweza kupambana na changamoto na msukumo uliopo mbele yake.

Hatahivyo msongo wa mawazo kwa kiasi kidogo ndo inayofanya mambo yaende.bila msongo wa mawazo kabisa mambo yangekua yanaboa na yangekua hayana maana kabisa.

Mfano..ili mwanafunzi asome na afaulu..anahitaji kiwango kidogo cha msongo wa mawazo. Bila msongo wa mawazo kabisa hatosoma kwa kua hakutokua na umuhimu wa kufanya hivyo. Hapa nitazungumzia msongo wa mawazo ambayo ni mbaya

Mfano wa mambo yanayoweza kusababisha msongo wa mawazo ni kama matatizo ya kisaikolojia na afya ya akili, matatizo ya kiuchumi, magonjwa, kazi nyingi au matatizo kazini, kufiwa, mambo usiyokua na uhakika nayo kama vile kusubiria majibu ya mtihani au ugonjwa, matatizo ya kimahusiano, n.k

BAADHI DALILI ZA MTU MWENYE MSONGO WA MAWAZO (sio lazima mtu awe nazo zote)
 Maumivu ya misuli
 kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa
 Kuumwa kicha
 Kinga duni dhidi ya magonjwa
 Kung’ata kucha
 Kushindwa kulala
 kuvuruga tumbo

 Kuwa na hasira
 hofu
 kuchoka
 sonona
 kusahau
 kukasirika hovyo
 kushindwa kuconcentrate
 kukosa utulivu
 huzuni
 kuchoka
 Kula sana/kukosa hamu ya kula
 Matumizi mabaya ya pombe na vilevi
 Uvutaji wa sigara uliopitiliza
 Kujitenga kijamii
 Matatizo kwenye mahusiano

MADHARA YA MSONGO WA MAWAZO (STRESS)
1. Kodhoofika kiafya > jinsi ubongounavyopambana na mawazo makali unakosa raha na muda wa kutulia kuweza kuujenga mwili kwa namna yeyote ile afya yako inazorota kabisa.
2. Vidonda vya tumbo > mwanadamu anapokosa kupata chakula kwa wakati au kula kiwango kidogo sana pamoja na kukaa kwa muda mrefu bila kula utumbo huathiriwa na asidi ya haidrokloriki (hydrocloric acid-hcl).
Malengo ya mwili kuzalisha na kutiririsha asidi ya mtindo huu ni kwa ajili ya kulainisha chakula pamoja na kurahisisha ufyonzwaji wake kuelekea mwilini, lakini inapokosa kukutana na aina yoyote ya chakula tumboni huanza kuchubua ukuta wa utumbo na hivyo kuweka vidonda.
Hivyo hali hii ikiendelea vidonda haviponi kirahisi na kuwa kama vile sugu kwa mhusika,jambo hili linakuja kwa vile mtu yeyote mwenye mawazo makali kuhisi njaa ni vigumu ndio maana wengi hupatwa na tatizo hili.
3. Kujidhuru binafsi au mtu mwingine, kuwa na msongo wa mawazo kuna wakati mhusika anakosa uvumilivu au ustaamilifu kwa tukio jipya linalokuja mbele yake hata kama ni dogo sana.
Wapo ambao huweza kufikia hatua ya kujeruhi mtu au yeye mwenyewe kwa jambo dogo tu linalotokea kwa muda huo.
4. Vifo vya ghafla, kudhoofika kiafya na hasira za mara kwa mara dhidi ya matukio yanayomkabili mwathirika wa msongo wa mawazo vinapelekea kupatwa na mishtuko ya pumzi au yeye mwenyewe kujiondoa uhai.
5. Magonjwa ya akili, chanzo cha msongo wa msongo hutofautiana kutoka mtu mmoja na mwingine. Hivyo matokea yanayosababishwa na msongo huo pia nayo hutofautiana kwa kila mtu,wapo ambao huwabadili kwa haraka na kuwa vichaa.
6. Magonjwa ya mfumo wa upumuaji pamoja na magonjwa mengine yanayoathiri mfumo wa damu kama vile kushuka na kupanda mapigo ya moyo(BP), kisukari (kutokana na kushindwa kufanya kazi vizuri-liver failure), kuvimba na kushindwa kwa ini (liver cihosis).
7. Kupata choo kigumu (Constipation) > Kutokana na kutopata chakula kwa wakati au kula kiwango kidogo sana hufanya mzunguko wa kujisaidia kuwa mdogo au kushindikana kabisa.
Kitakacho kuja kutokea ni kugandamana kwa ule uchafu tumboni bila kuweza kujitoa wenyewe, kitu ambacho utaingia kwenye gharama mpya za matibabu.
8. Kukosa nguvu za kiume na hamu ya kujamiiana > Wakati ubongo unasumbuliwa na mawazo ya mara kwa mara hata zile homoni zinazo zalisha mbegu na hamu ya kujamiiana hushindwa kufanya kazi yake kwa vile ubongo huwa na kazi moja tu ya kupambana na mawazo(stress).
Ikiwa au utabahatisha kupata msisimko mara moja huwa vigumu kurudia tendo kwa mara ya pili au hata ukakatishwa mihemko katikati ya mchezo.
Kwa wanawake mara nyingi ashki(hamu) hupotea na kinachobaki ni kumridhisha mwenza wake tu.
10. Kuwahi sana kufika kileleni (pre-ejaculation) na kukosa nguvu ya kulimudu tendo kwa mara ya pili,hisia zinaweza kupanda kwa haraka na kupotea kwa haraka vile vile.
11. Kupoteza kumbukumbu mara kwa mara hasa kwa mambo mapya yanayotokea ambayo mwathirika wa msongo wa mawazo hajayakabili kama chanzo cha msongo wake.

NINI KIFANYIKE BAADA YA KUPATWA NA MSONGO WA MAWAZO
-Fanya mazoezi ya taratibu ,mfano kuruka kamba kukimbia mbio fupi au kushiriki kwenye michezo hii itasaidia mwili kurudi katika hali yake ya kawaida 
-Tenga muda wa kufurahi kila siku ,jaribu kutenga muda wa kufanya kitu ambacho kinakufurahisha
-Epuka kukaa peke yako unapokaa peke yako unajipa nafasi ya kuendelea kuwa na mawazo.
Endapo utaona hatua hizo hazikupi matokeo ni vyema kumuona tabibu wa ushauri nasaha au tembelea taasisi yoyote ya ushauri nasaha kupata suluhisho.

Post a Comment

Previous Post Next Post