Taarifa njema kuhusu corona (COVID19)

Katika siku za hivi karibuni vipimo sahihi vya ugonjwa huo vimechukuliwaTunaweza kuorodhesha maambukizi ya virusi vipya vya corona kuwa janga au la , lakini ukweli ni kwamba ni suala nyeti.
Katika chini ya miezi miwili virusi hivyo vimesambaa hadi mabara kadhaa. Janga lina maana ya kwamba virusi hivyo vinasambaa kwa kasi ya juu katika zaidi ya mabara matatu.
Huenda tayari tumefikia awamu hiyo , lakini sio sawa na vifo, kwa kuwa jina hilo halimaanishi hatari ya virusi hivyo bali jinsi vinavyosambaa kutoka eneo moja hadi jingine. Kile kilichopo ni janga la hofu .
Kwa mara ya kwanza katika historia tunakabiliwa na janga hatari: Katika vyombo vyote vya habari kila siku katika kila eneo duniani vinaongea kuhusu virusi vya corona.
Imeripotiwa nchini Brazil kwamba virusi hivyo vimezaana mara tatu zaidi.

Ni muhimu kuripoti kinachotokea duniani lakini pia wasomaji wanahitaji habari njema, kama hizi:-

1.Tunafahamu ni ugonjwa gani

Katika siku ya 10 ya mlipuko huo virusi hivyo vilikuwa vimegunduliwaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKatika siku ya 10 ya mlipuko huo virusi hivyo vilikuwa vimegunduliwa
Kisa cha kwanza cha ugonjwa wa ukimwi kilitangazwa mwezi Juni 1981 na ilichukua zaidi ya miaka miwili kugundua virusi vinavyosababisha ugonjwa huo.
Visa vya kwanza vya ugonjwa hatari wa mapafu viliripotiwa nchini China mnamo tarehe 31 mwezi Disemba 2019 na ilipofikia tarehe 7 mwezi Januari virusi hivyo tayari vilikuwa vimefichuliwa. Virusi vya Corona viligunduliwa siku 10 baadaye.
Tayari tunajua kwamba ni virusi vipya kutoka familia moja na virusi vya SARS . Ugonjwa huo umepatiwa jina COVID19. Unahusishwa na virusi vya corona kutoka kwa popo.

2. Tunajua jinsi ya kuvigundua katika mwili wa mwanadamu

Sampuli ya RT-PCR inapatikana kila mahali tangu tarehe 13 mwezi Januari. Katika miezi ya hivi karibuni vipimo hivyo vimeboreshwa .
Vipimo kadhaa vimefanywa ili kugundua ni nani anayebeba virusi vya corona.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionVipimo kadhaa vimefanywa ili kugundua ni nani anayebeba virusi vya corona.

3. Nchini China hali inaimarika

Udhibiti mkali na mikakati ya kuwatenga walioambukizwa imeanza kuzaa matunda.
Kwa wiki kadhaa sasa idadi ya watu wanaopatikana na virusi hivyo imepungua kila siku. Katika mataifa mengine , visa vya maambukizi vinafuatiliwa kwa kina .
Mikakati iliowekwa ni ya nguvu na visa vinaweza kudhibitiwa kwa urahisi kwa mfano nchini Korea kusini na Singapore.
4. Asilimia 80 ya visa vyote vilivyobainika havijaonyesha makali
Ugonjwa huo hautoi ishara ama hauna makali kati ya visa asilimia 81.
Katika asilimia 14 iliosalia vinaweza kusababisha ugonjwa hatari wa mapafu na asilimia tano vikiwa hatari na hata kusababisha kifo

5. Watu wanapona

Mgonjwa wa virusi vya corona aliyepona anatoka katika hospitali Fangcang, WuhanHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMgonjwa wa virusi vya corona aliyepona anatoka katika hospitali Fangcang, Wuhan
Data ya pekee ambayo inaonyeshwa na vyombo vya habari ni ongezeko la visa vilivyothibitishwa na idadi ya vifo.
Lakini idadi kubwa ya watu walioambukizwa wamepona. Idadi ya watu waliopona ni mara 13 zaidi ya waliofariki na idadi hiyo inazidi kuongezeka.

6. Virusi hivyo haviwaathiri karibia watoto wote

Ni asilimia tatu pekee ya watu walio chini ya umri wa miaka 20 walioathirika na idadi ya vifo ni asilimia 0.2. kwa watu walio chini ya umri wa miaka 40.
Miongoni mwa watoto dalili ni chache hali ya kwamba mara nyengine hazionekani.

7. Ni rahisi kuua virusi hivyo

Virus hivyo vinaweza kuuliwa katika sakafu kupitia ethanol , Hydrogen peroxide au sodium hypochlorite katika dakika moja pekee.
Uoshaji wa mikono mara kwa mara kwa kutumia maji na sabuni ndio njia bora ya pekee ya kuzuia maambukizi.
Kuosha mikono ndio njia moja ya kuzuia maambukiziHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKuosha mikono ndio njia moja ya kuzuia maambukizi

8. Kuna takriban ripoti 150 za kisayansi kuhusu ugonjwa huo.

Ni wakati wa sayansi na ushirikiano. Katika kipindi cha mwezi mmoja , takriban ripoti 164 zimeandikwa kuhusu ugonjwa COVID19 au SARSCov2, ikiwemo ripoti nyengine nyingi zaidi ambazo hazijachapishwa.
Ni kazi za ya utangulizi juu ya chanjo, matibabu, ugonjwa, jeni na phylogeny, utambuzi na mambo ya kliniki.
Ripoti hizo zinaandaliwa na watunzi kote duniani.
Kufikia sasa nchi 33 kati ya 47 Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara zina vifaa vya kupima virusi hivyo, ukilinganisha na mataifa mawili pekee JanuariHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKufikia sasa nchi 33 kati ya 47 Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara zina vifaa vya kupima virusi hivyo, ukilinganisha na mataifa mawili pekee Januari
Mwaka 2003, wakati virusi vya SARS vilipotokea , ilichukua zaidi ya mwaka mmoja kupata chini ya nusu ya ripoti kama hizo.
Kuongezea ni kwamba majarida mengi ya kisayansi yameweka wazi ufadhili wao wa virusi vya corona.

SOMA PIA:DHANA potofu kuhusu ugonjwa unaosababishwa na coronavirus

9. Tayari kuna sampuli tofauti za chanjo zinazojaribiwa

Uwezo wa kutafuta chanjo tofauti ni mzuri. Tayari kuna zaidi ya miradi minane dhidi ya virusi hivyo.
Kuna makundi yalioanzisha juhudi za kutafuta chanjo dhidi ya virusi vingine kama hivyo.
Kile kinachorefusha uboreshaji wake ni vipimo vyote muhimu vya sumu yake, madhara yake , usalama wake , kinga na uwezo wake katika kinga.
Maabara kadhaa kote duniani zinafanya kazi kuhusu chanjo ya virusi hivyoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMaabara kadhaa kote duniani zinafanya kazi kuhusu chanjo ya virusi hivyo

10. Kuna majaribio 80 ya kutumia dawa za kukabiliana na virusi

Chanjo zina kinga. Umuhimu wake zaidi ni tiba ya watu ambao tayari ni wagonjwa. Tayari kuna majaribio 80 ya kutafuta tiba ya virusi vya corona.
Hizi ni dawa ambazo zimetumika kwa mambukizi mingine ambayo tayari yamethibitishwa na tunajua ziko salama.
Mojawapo ya dawa hizo ambayo tayari imejaribiwa katika binadamu ni dawa ya remdesivir - dawa ya virusi vya ukimwi ambayo bado inafanyiwa utafiti ambayo imejaribiwa dhidi ya magonjwa kama vile Ebola na SARS/MERS.
Dawa nyingine ni ile aina ya Chloroquine, dawa ya kukabiliana na malaria ambayo pia ina uwezo wa kukabiliana na virusi .
Inajulikana kuwa na uwezo wa kuzuia maambukizi.
Dawa za kukabiliana na virusi zimependekezwa na watafiti kutoka Chuo kikuu cha Ural Federal, Urusi kuwatibu wagonjwa wenye virusi vya coronaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDawa za kukabiliana na virusi zimependekezwa na watafiti kutoka Chuo kikuu cha Ural Federal, Urusi kuwatibu wagonjwa wenye virusi vya corona

Post a Comment

Previous Post Next Post