Vifo vinavyosababishwa na maambukizi ya virusi vya ugonjwa mpya unaofahamika kama 'corona' vimeongezeka nchini China na kufika watu 41, katika sku ya mwaka mpya wao.
Vifo vingine 15 vilitokea katika jimbo la Hubei, eneo ambalo virusi hivyo vilianzia, ilitangazwa siku ya jumamosi.
Maafisa wa afya bado wanahangaika kutafuta tiba au kinga ya virusi hivyo kwa kuwa mlipuko wa ugonjwa huo umetokea kipindi ambacho mamilioni ya raia wa China wanasafiri kwa ajili ya sherehe muhimu nchini humo ya mwaka mpya. Matamasha mengi yamezuiliwa kufanyika katika kipindi hiki.
Kuna visa zaidi ya 1,200 vimethibitishwa nchini China.Virusi hivyo vimeenea pia bara la ulaya, watu watatu wamethibitika kuwa na ugonjwa huo nchini Ufaransa.
Uchunguzi unaofanywa Uingereza kwa kuwachunguza watu 2000 ambao wamesafiri kutoka jimbo la Hubei kwenda Uingereza.
Australia imethibisha kuwa na visa kadhaa vya ugonjwa huo katika mji wa Melbourne na Sydney.
Virusi hivyo huwa vinafanyaje?
Virusi vya coronaus, awali vilikuwa havijatambuliwa na wanasayansi, huwa vinamfanya mtu mwenye maambukizi kuwa na dalili za homa na kikohoa.
Hakuna tiba wala chanjo inayoweza kuzuia maambukizi hayo mpaka sasa.
Ripoti ya awali ilisema kuwa watu 17 ndio wamefariki kutokana na ugonjwa huo, lakini inaonekana watu waliopata maambukizi hayo kuwa wengi zaidi na inaonekana kuwapata watu wazima zaidi.
Ingawa kati ya watu hao waliokufa hivi karibuni, miongoni mwao alikuepo daktari wa Hubei, televisheni ya China 'Global Television Network ' iliripoti.
Dalili zinaonyesha uanza kwa homa, alafu kinafuata kikohozi kikavu, baada ya wiki mtu anashindwa kuhema vizuri na baadhi ya wagonjwa huwa wanahitaji tiba ya hospitali wakiwa na dalili hizo.
Vitu gani vimekatazwa katika mji wa Hubei?
Watu wamekatazwa kusafiri kutoka mji mmoja mpaka mwingine.
Mji wa Wuhan, ambako mlipuko huo ulianza, vilevile umesitisha huduma zote za usafiri kuanzia wa mabasi yote, feri zote ndege zote na treni zote zimeacha kufanya kazi.
Gazeti la 'The People's Daily' limeripoti kuwa kuanzia jumapili, gari binafsi peke yake ndio zitaruhusiwa kutembea katika barabara za mji wa Wuhan.
Hospital mpya imeanza kujengwa katika mji huo kwa ajili ya wagonjwa wa virusi vya corona. Vyombo vya habari vya China vinasema kuwa ndani ya siku sita , hospital hiyo itakuwa na vitanda 1,000.
Maduka ya dawa katika mji huo yameanza kuishiwa dawa.
Wakazi wa mji huo wameshauriwa wasitokea nje huku barabara zikiwa zimefungwa.
Mji mdogo wa Ezhou, uliopo Hubei, umefunga huduma za treni. Mji wa Enshi umesitisha huduma zote za mabasi.
China yote ikoje?
Kiongozi wa Hong Kong, Carrie Lam, ametoa angalizo la hatua ya tahadhali siku ya jumamosi na kuongeza muda wa likizo za shule kwa wiki mbili.
Maafisa wa mji mkuu wa Beijing, na Shanghai wamewataka watu wanaotoka katika maeneo yenye maambukizi kubaki nyumbani kwa muda wa siku 14.
Mamlaka imefunga maeneo yote ya utalii likiwemo eneo la Forbidden mjini Beijing pamoja na upande wa Great Wall, Matukio ya umma yamesitishwa pia katika maeneo yote ya nchi ikiwa pamoja na :
- Huduma za kitamaduni za kwenye mahekalu Beijing
- Tamasha la kimataifa la Hong Kong
- Mashindano ya mwaka ya mpira wa mguu Hong Kong
- Sherehe zote za mwaka mkpya wa China huo Macau
Mgahawa wa McDonald umeripotiwa kufungwa katika miji mitano
Siku ya alhamisi mgonjwa wa corona alifariki kaskazini mwa jimbo la Hebei - na hicho kuwa kifo cha kwanza kutangazwa nje ya mji wa Hubei.
Vifo vingine vilithibitishwa kutokea baadae kaskazini-mashariki mwa jimbo la Heilongjiang, zaidi ya kilomita 2000 kutoka mji wa Wuhan.
Awali wakati vifo vya watu 17 vilivyotangaza baraza za afya la taifa la China, walisema kuwa mtu mwenye umri mdogo aliyefariki ni kuanzia 48 na kufikia miaka 89.
Lakini kati ya 15 kati ya 17 walikuwa wamepita umri wa miaka 60,na wengi wao walikuwa wanasumbuliwa na magonjwa ya muda mrefu kama kisukari. Na wanne kati yao ndio wanawake.
Je tunajua nini kuhusu virusi hivi?
Sampuli ya virusi vya ugonjwa vilivyochukuliwa kutoka kwa mgonjwa na kuchunguzwa katika maabara na maafisa wa serikali pamoja na wale wa shirika la afya duniani WHO zimethibitisha kwamba ugonjwa huo ni ule wa Coronavirus.
Virusi hivyo ni familia kubwa ya virusi sita na kirusi hicho kipya kitaongeza idadi hiyo kufikia saba ambapo ni maarufu kwa kusababisha maambukizi miongoni mwa binadamu.
Virusi hivyo vinaweza kusababisha homa, lakini pia vinaweza kusababisha ugonjwa mbaya wa Sars ambao uliwauwa watu 774 kati ya 8,098 walioambukizwa katika mlipuko ulioanza China 2002.
Uchanganuzi wa jeni za ugonjwa huo mpya unaonyesha kuhusishwa karibu na ugonjwa wa Sars zaidi ya ugonjwa wowote wa Coronovirus.
Mamlaka ya China imeripoti visa 139 vipya vya ugonjwa huo usiojulikana katika siku mbili, ikiwa ni mara ya kwanza kwa maambukizi hayo kuthibitishwa nchini humo nje ya mji wa Wuhan.