Tumbo kujaa gesi ni tatizo linalowakumba watu wengi gesi inapojaa tumboni tumbo linaweza kuvimba,kuwa gumu na wakati mwingine kuuma kama vichomi.
Dalili za tumbo kujaa gesi
-Kutoa hewa mara kwa mara kupitia mdomoni (kubeua) au kwenye njia ya haja kubwa
-Kuwa na milio kama muziki ndani ya tumbo
-Tumbo kuwa kama limebanwa kiasi cha kusababisha kufungua mkanda au kulegeza nguo iliovaliwa
-Mara nyingine ni kutokana ma magonjwa kama figo,ini au moyo
Sababu za tumbo kujaa gesi
-Kula chakula kwa haraka huku mtu akiongea
-Uvutaji sigara
-Magonjwa na maambukizi katika mfumo wa chakula na hasa kwenye utumbo hali inayozuia kusagwa na kufyonzwa kwa chakula
-Kutumia vinywaji vyenye kaboneti (carbonates) nyingi kama vile cola na kula vyakula vyenye gesi mara kwa mara kama vile maharage,vitunguu na kabeji
Tiba yake
-Kunywa chai yenye tangawizi au karafuu kunasaidia kupunguza gesi
-Kutafuna mbegu za maboga kunasaidia kulainisha mfumo wa chakula
-Kufanya mazoezi mepesi ya kutembea na kurukaruka
Iwapo hatua za tiba binafsi hazitoi matunda inashauriwa muhusika aende hospitali kwa ushauri zaidi wa kitabibu.
Tags:
TUMBO KUJAA GESI