Shirika la afya duniani latangaza corona kuwa janga la dunia

Abiria wakiwa wamefunika pua na mdomo uwanja wa ndege wa Beijing tarehe 30 mwezi JanuariVirusi vipya vya corona vimetangazwa kuwa janga la dharura,wakati virusi hivyo vikiendelea kusambaa kwa kasi nje ya China, kwa mujibu wa shirika la afya duniani(WHO).
"Sababu kubwa ya tangazo hilo si kwa sababu ya kile ambacho kinatokea China kwa sasa lakini kile ambacho kinatokea katika mataifa mengine," alisema kiongozi mkuu wa shirika la afya duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus .
Kinachoangaziwa zaidi ni kuhusu ugonjwa huo kusambaa mataifa mengine huku kukiwa na mfumo duni wa afya
Watu takribani 213 wamefariki kutokana na virusi hivyo nchini China.
Shirika la afya duniani limesema kuwa kumekuwa na visa 98 katika mataifa mengine 18 ingawa hakuna vifo vilivyobainika. Visa vingi vya wagonjwa hao walikuwa wamesafiri kutoka mji wa Wuhan, eneo ambalo mlipuko wa ugonjwa huo ulianza.
Hata hivyo kuna kesi nane zilizosababishwa na maambukizi ya kati ya mtu kwa mtu huko Ujerumani, Japan, Vietnam na Marekani.
Akizungumza katika mkutano wa habari Geneva, Dkt Tedros alielezea virusi vya corona kuwa mlipuko wa ugonjwa ambao haujawahi kutokea awali na bado haujaweza kupata suluhu.
Dkt.Tedros alisifia hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na serikali ya China katika kuzuia maambukizi yasienee na alisema kuwa hakukuwa na sababu ya kuzuia watu wasisafiri au biashara zisiendelee.
ChinaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
"Lakini nataka kueleweka kuwa ,tangazo hili halimaanishi kuwa ni kura ya kutoiamini China".
Lakini nchi mbalimbali zimechukua hatua ya kufunga mipaka na kusitisha safari za ndege za nchini China, vivyo hivyo makampuni makubwa pia yamefunga maduka yao.
Presentational grey line

Maandalizi katika mataifa mengine yakoje

Presentational white space
Itakuwaje kama virusi hivi vitasambaa katika mataifa mengine? Mataifa ambayo uchumi wake uko chini au wa katikati na ngumu kwa wao kupata vifaa vya kujizuia maambukizi au kutafuta tiba.
Hofu ipo kuwa inawezekana ugonjwa huu ushindikane kuzuilika na unaweza kumpata mtu bila kujijua wakati mwingine.
Kumbuka kuwa ugonjwa huu umeanza mwezi mmoja tu mpaka sasa na tayari kuna kesi 7,736 zimethibitishwa kuwepo nchini China na watu wakiwa wanashukiwa kuwa na ugonjwa huo.
Mwaka 2014, mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ulitokea magharibi ya Afrika, ugonjwa huo uliweka historia kubwa katika maisha ya binadamu, na ulionyesha wazi ni namna gani nchi maskini zinavyoweza kushambuliwa na mlipuko wa ugonjwa.
Na kama hali kama hii ya virusi vya ebola ingetokea katika maeneo ya aina hiyo ingekuwa ngumu sana kuzuia maambukizi.
Tuko kwenye hatua ambayo asilimia 99 ya kesi za watu wenye maambukizi iko China na shirika la afya duniani lina imani kuwa nchi hiyo inaweza kukabliana na mlipuko huo.
Lakini kutangaza kuwa janga la dharura la dunia kutaweza kuruhusu WHO kuzisaidia nchi zenye kipato kidogo na cha katikati kujiandaa kukabiliana na virusi vya corona.
Presentational white space

Matangazo ya dharura huwa yakoje?

Shirika la afya duniani huwa linatangaza kwa umma kuhusu dharura ya afya ya kimataifa kwa kuangalia tukio la mlipuko wa ugonjwa ambao sio wa kawaida ,na kuna hatari kubwa ya maambukizi ya ugonjwa huo duniani.
Dharura za afya duniani zilizowahi kutangazwa na shirika la afya ni pamoja na :
  • Mafua ya Swine, 2009 -Virusi vya H1N1 vilisambaa duniani mwaka 2009, na kuua zaidi ya watu laki mbili 200,000 na dhurara ya afya duniani ilitangazwa ili kuhakikisha kuwa dunia inaangazia kwa umakini maambukizi ya ugonjwa huo na kuhakikisha kuwa chanjo inapatikana.
  • Polio, 2014 - Ingawa ugonjwa huu unakaribia kuisha tangu mwaka 2012, maambukizi ya polio yalianza mwaka 2013.
  • Zika, 2016 - Shirika la afya duniani lilitangaza kuwa Zika ni ugonjwa wa dharura mwaka 2016 baada ya ugonjwa huo kusambaa Marekani. Ingawa dalili nyingi za Zika zilikuwa hatari zaidi kwa wanawake wajawazito na tangazo la dharura lilitaka uchunguzi zaidi kufanyika.
  • Ebola, 2014 na 2019 - Mlipuko wa kwanza wa virusi vya ebola vilikuepo kuanzia Agosti 2014 mpaka mwezi machi, 2016 ambapo watu wapatao 30,000 waliambukizwa na zaidi ya watu 11,000 walikufa magharibi mwa Afrika.Shirika la afya duniani liliseama kuwa mfumo wa afya katika jamii hiyo ulikuwa uko chini ndio maana hatari ya maambukizi ilikuwa juu.

Post a Comment

Previous Post Next Post