Maziwa ya mende chanzo bora cha protini


Diploptera puncataHaki miliki ya pichaTOM LIBBY KAUSHIK JAYARAM AND PAULINE JENNINGS
Image captionMende wa Diploptera puncata hujifungua
Wengi huenda wakawa hawawezi kuwavumilia mende, hata kuwatazama pekee, lakini wanasayansi nchini India wanasema huenda mende wakatoa tumaini kwa binadamu, katika lishe.
Wamegundua kwamba chembe za protini za maziwa kwenye mende zina virutubisho "vingi ajabu”.
Wanasema vinasema kutumiwa kama tembe ama chakula chenye virutubisho vya protini kwa kiwango cha juu.
Wanasayansi katika taasisi ya sayansi ya seli katika mji wa Bengaluru, wamefanya ugunduzi huo baada ya kutafiti muundo wa chembe za protini zinazopatikana katika utumbo wa aina ya mende wajulikanao kama Diploptera puncata, ambao ndio pekee hujifungua.
Ingawa mende wengi kwa kawaida hawatoi maziwa, mende aina ya Diploptera puncata huwa wanatengeneza aina fulani ya maziwa yenye protini kwenye utumbo, ambayo hutumiwa kulisha watoto wake.
Chembe moja ya protini hiyo inakadiriwa kuwa na kiwango mara tatu cha nguvu ya mwili ikilinganishwa na kiasi sawa cha maziwa ya nyati.
Aidha, chembe hizo zina nguvu mara nne kushinda maziwa ya ng’ombe.
“Ni chakula kamili, unapata protini, mafuta na sukari,” amenukuliwa mmoja wa watafiti waliohusika, Sanchari Banerjee, na gazeti la The Times of India.
Diploptera puncata
Image captionMende huliwa katika maeneo mengi duniani hasa Mashariki ya Mbali
Matokeo ya utafiti huo yamechapishwa katika jarida la kimatibabu la International Union of Crystallography.
Ramaswamy anasema kwa kutumia ufahamu wao wa muundo wa protini hizo, wanaweza kutumia hamira kuzalisha chembe kama hizo kwa wingi kwenye maabara.
Isitoshe, anasema muundo wa chembe hizo unaonesha matumaini kwamba zinaweza kuundwa na kutumiwa katika vidonge vya dawa.
chanzo bbc

Post a Comment

Previous Post Next Post