- Epuka kumlazimisha mtoto kula wakati hataki, hapa tunasema mpe mazingira rafiki wakati wa kula. Kama hataki muache halafu utamjaribu tena baada ya muda mfupi (lisaa 1 – 2 baadae)
- Familia ijitahidi kuwa na muda maalumu wa kula, hata kama wazazi hawapo basi mlezi wa mtoto ale wakati mtoto naye anakula. Na muda uwe ule ule (Regula family meal)
- Wakati mwingine watoto wanachoka vyakula vya kuponda ponda sana hivyo kuanzia mwaka mmoja mtoto aanze kupewa vyakula vya kawaida, akivipenda aendelee navyo.Na wengine wanazoea aina hii ya vyakula vya kuponda hataki vigumu.
- Wazazi wanashauriwa kuwabadilishia watoto chakula mara kwa mara mfano asubuhi isiwe uji tu, siku nyingine unaweza mpa viazi vitamu vilivyo pondwa na maziwa au uji wa mchele wenye Matunda yaliyo sagwa nk.
- Vyombo vya mtoto visiwe vile vile kila siku awe anabadilishiwa.Akivikariri anaboreka navyo hata kama chakula ni tofauti.
- Wazazi wawe mfano bora wakula vyakula vyenye afya nzuri, watoto wanaiga wazazi na walezi wao
- Kwa watoto wakubwa washirikishwe kwenye uandaaji wa chakula. Mfano kukoroga unga wa chapati ya maji nk.
- Hakikisha unampa mtoto chakula chenye virutubisho vingi kwa mfano hapo chini, hivyo akila hata vijiko vitano anakuwa ameingiza virutubisho vingi hasa kwa wale watoto wasio penda kula kabisa.
- Epuka kumkaba mtoto wakati wa kumlisha na kumbuka huyo ni mtoto usitengeneze mazingira rahisi kwako umlishe haraka haraka. Mlishe taratibu kwa namna anavyokula taratibu na sio kumshikia fimbo mtoto anakula kwa woga.
- Kuongeza kiini cha yai kwenye uji au maziwa au viazi vya kuponda
- Chapati ya maji au mkate uliotiwa mayai
- Ongeza karanga ya kusaga katika vyakula vya mtoto.
- Tumia maziwa na samli kwenye vyakula vya mtoto
- Msagie mtoto matunda na maziwa /yoghurt na sio matunda peke yake
- Ukiona mtoto anakataa chakula ukimpa peke yake siku nyingine badilisha mazingira muwekee chakula chake au mlishe wakati na wengine wanakula hii itamsaidia kumjengea mazoea ya kupenda kula
MTOTO KUTOKULA HUSABABISHWA NA NINI?
- Mtoto kuto kupenda ladha ya chakula
- Mtoto kuwa mgonjwa .Imegundulika wakati mwingine mtoto anaweza kuwa na vidonda au uambukizo kooni.Hivyo akawa hapendi kula labda anaumia na wewe mzazi hujui kwa sababu hasemi unachoona ni anakataa kula.
- Pia upungufu wa madini Fulani mwilini au virutubishi unaweza msababishia asipende kula.Na hii hutokana na mzazi kumpa mtoto chakula cha aina mojaa bila kumchanganyia vyakula vya makundi mbali mbali.Matokeo yake anakosa hivyo virutubishi vinavyomchochea kupata hamu ya kula hasa vitamin na madini.
- Mtoto kula wakati ameshiba, hata kama alikunywa maji kabla ya kula (kutohisi njaa)
- Mazingira mabaya ya kula (makele, jua kali, joto, baridi nk.)
- Mtoto kurithi tabia hii kutoka kwa familia yake,hapendi tu kula (Genetical reason)
Tags:
AFYA YA WATOTO