Coronavirus: Serikali ya Tanzania yawataka wazazi wa wanafunzi waliopo likizo kutowaruhusu kurudi China

Kassim MajaliwaSerikali ya Tanzania imewataka wazazi na walezi kutowaruhusu watoto zao waliopo likizo kutorudi masomoni China hadi pale serikali itakapotoa tangazo.
Kulingana na taarifa iliotolewa na afisi ya waziri mkuu hatua hiyo inatokana na China kukumbwa na mlipuko wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona.
Katika taarifa hiyo waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema kwamba kwa sasa serikali inawasiliana na ujumbe wake nchini China ili kufahamu yanayoendelea.
"Tunawasihi watoto wasirudi hadi hapo tutakapopata taarifa za kidiplomasia kuhusiana na maendeleo ya ugonjwa huo."
Majaliwa alikuwa akijibu swali la mbunge wa Mafinga mjini , Mheshimiwa Cosato Chumi katika kipindi cha maswali kwa waziri mkuu.
Mbunge huyo alitaka kujua jinsi serikali ilivyojipanga kukabiliana na homa hiyo pamoja na baa la nzige.
Akijibu Majaliwa amesema kwamba tayari waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu ametoa taarifa kwa umma huku akiwahakikishia Watanzania kwamba homa hiyo haijaingia nchini humo.
Afisa wa matibabu akichunguza sampuli za wagonjwa wa virusi vya CoronaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAfisa wa matibabu akichunguza sampuli za wagonjwa wa virusi vya Corona
Waziri mkuu amesema kwamba serikali imekuwa ikiwasiliana na ubalozi wake nchini China mara kwa mara hali kujifahamisha kuhusu hali ilivyo kupitia balozi Mbelwa Kairuki ambaye amekuwa akitoa mrejesho wa mara kwa mara kwa serikali.
Amesema kwamba mbali na mrejesho wa mara kwa mara anaotoa balozi huyo pia amekuwa akitoa elimu kwa Watanzania kupitia madaktari wa nchi hiyo ambao wamepata mafunzo kuhusiana na ugonjwa huo ili kuwaelimisha Watanzania waliomo nchini humo namna ya kujikinga na homa hiyo.
Virusi hivyo vinauwezo wa kusababisha maradhi hatari ya mapafuHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionVirusi hivyo vinauwezo wa kusababisha maradhi hatari ya mapafu
Hatua hiyo inajiri baada ya wanafunzi walioko nchini China katika mji wa Wuhan kuzungumzia walivyokwama nchini humo.
Jiji la Wuhan ni kitovu cha mlipuko wa virusi vya Corona, ambapo mpaka sasa watu 170 wamefariki.
Kulingana na Dkt Bakari ambaye ni mwanafunzi wa taasisi ya Tongji, chuo kilichopo mjini Wuhan kinachohusika na utafiti wa magonjwa mbalimbali ya mlipuko, maisha yamebadilika kwa kuwa watu hawaruhusiwi kutoka nje huku katika vyuo vingine wanafunzi wakizuiwa hata kushuka ngazi kutoka ghorofa moja kwenda nynegine.
Mwanafunzi huyo amesema kwamba katika vyuo vingine utaratibu maalum umewekwa ambapo wanafunzi wanapelewa chakula hadi mlangoni.
Jumuiya ya wanafunzi nchini China inasema kuwa wanawasiliana na ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing kwa kila kinachoendelea.
MwanafunziHaki miliki ya pichaKHAMIS BAKARI
Dkt. Khamis anasema kuwa kuna Watanzania 420 kwa sasa, huku wengine takribani 200 wakiwa wamerejea Tanzania kwa likizo kabla ya mlipuko wa virusi hivyo kutokea.
"Kwenye vyuo vyote wameweka walinzi na hairuhusiwi kabisa mtu kutoka nje ya geti la chuo. Tunawasiliana kwa simu tu hata na majirani hatuonani.
Aidha ameongezea kwamba baadhi ya wanfunzi kutoka nchini Tanzania wanataka kurudi nyumbani kufuatia mlipuko huo.
Wanafunzi wengi wanataka kurudi nyumbani, "kundi moja la Watanzania walikusanyika wengi juzi na wakanipigia simu wakitaka kurudi nyumbani, lakini changamoto ni usafiri, hakuna namna ya kutoka hapa tulipo".
Anasema kuwa China imeweka katazo hilo ili kuzuia mlipuko huo kuwa janga la kimataifa.
"Na sababu kuu ni kuwa wagonjwa wa virusi hivi wengine huwa wanapitiliza muda wa wiki mbili, wengine zinafika hata nne hivyo kama tutaweza kurudishwa nyumbani basi inabidi tutengwe eneo maalum kwa muda wa wiki nne."

Post a Comment

Previous Post Next Post