Kabla ya kuanza mazoezi haya fanya mambo yafuatayo,jilaze chini kama picha inavyoonesha hapo chini vuta pumzi na kuitoa nje taratibu kwa sekunde 15,nyoosha mguu wako mmoja juu huku mwingine ukiwa umebaki chini kisha ukunje mguu wako usawa wa goti lako fanya hivyo mara tano kisha ulaze chini uinue mguu mwingine fanya kama mguu wa kwanza.Mazoezi haya ya awali yanauandaa mwili wako tayari kwa mazoezi ya kupunguza tumbo au mafuta tumboni.kisha fuata hatua zifuatazo:
1.JILAZE HUKU UKIINUA MIGUU YAKO JUU
-Jilaze huku ukiinua miguu juu ukiwa umeibananisha kama inavyoonesha kwenye picha weka viwiko vyako usawa wa kiuno chako.
-Tulia kwa sekunde kumi huku miguu yako ikiwa imeinuliwa juu
-Ishushe miguu yako kwa pamoja taratibu ukiwa umenyooka
-rudia zoezi hilo mara tatu.
2.NYOOSHA MIGUU NDANI NA NJE IKIWA IMEBANANISHWA
-Kaa chini weka mikono yako nyuma yako hakikisha haipo mbali na mwili wako
inua miguu yako ikunje usawa wa magoti kisha inyooshe tena bila kuigusisha chini
-Pindi unakunja miguu yako hakikisha usawa wa magoti umekaribiana na sehemu ya juu ya mwili wako
-Rudia zoezi hilo mara tatu hakikisha miguu yako haigusi chini mpaka utakapo maliza zoezi.
TAHADHARI
Kwa lengo la kupunguza mafuta tumboni hakikisha unafanya moja kati ya mazoezi haya mara kwa mara bila kuacha kwa muda wa miezi miwili utaona mabadiliko ya kupungua kwa tumbo lako kwa haraka
Usipozingatia kufanya mazoezi mara kwa mara utaifanya misuli yako kua migumu kushindwa kufanya kazi ipasavyo kwa ajili ya kupunguza mafuta tumboni hivyo hautaona matokeo ya kupungua tumbo lako kwa haraka na wengi wao huwa wanakata tamaa na kuacha kabisa kufanya mazoezi.
Tags:
MAZOEZI
Love it.congrats dr
ReplyDelete