Mwanaume mmoja ameshtakiwa kwa makosa 159 ya unyanyasaji kingono, yakiwemo makosa 136 ya ubakaji, jaji amesema kuwa labda mtu huyo hataachiwa huru tena kwa kuwa si mtu salama.
Reynhard Sinaga alikutwa na hatia ya kuwarubuni wanaume 48 nje ya kilabu cha Manchester na kuwapeleka katika makazi yake, ambapo aliwalewesha madawa na kuwafanyia vitendo viovu vya kingono -na kupiga picha matukio hayo.
Polisi wanasema kuwa, wana ushaidi unaomuhusisha Sinaga, mwenye umri wa miaka 36, ambaye alitajwa kwa mara ya kwanza kuhusika na udhalilishaji wa watu 190.
Mwendesha mashtaka wanasema kuwa Sinaga ni mbakaji aliyevunja rekodi katika historia ya Uingereza.
Mahakama imemuhukumu kifungo cha maisha au kifungo cha miaka 30 gerezani.
Mwanafunzi huyo wa chuo kikuu tayari ameanza kutumikia miaka 20 gerezani , kwa kukutwa na hatia ya makosa mengine aliyoyafanya 2018 .
Ukiachilia mbali mshtaka mengine manne ambayo alikutwa nayo, kijana huyo mwenye uraia wa Indonesia alikutwa na hatia ya makosa 136 ya ubakaji, na majaribio 8 ya ubakaji, makosa 14 ya unyanyasaji wa kingono na kosa moja lingine linalohusisha sehemu za siri, dhidi ya waathirika 48.
Maafisa wa upelelezi wanasema kuwa wameshindwa kuwabaini waathirika 70 na sasa wanataka watu wote waliohisi kuwa walifanyiwa unyanyasaji na Sinaga kujitokeza.
Wakati wa shauri la kesi hiyo jaji Suzanne Goddard alisema kuwa Sinaga alihusika katika matukio kadhaa ya unyanyasaji wa kingono kwa vijana wadogo ambao walikuwa wanataka kufurahi na marafiki tu.
"Katika hukumu yangu, wewe ni mtu hatari sana ambaye unahitajika kuadhibiwa na kutoachiwa huru tena," Jaji alimwambia mtuhumiwad - na kuongeza kuwa maamuzi hayo yamefanywa na bodi ya wafungwa.
Sinaga alikuwa anasubiri muda ambao watu wanaondoka kumbi za starehe kabla ya kuwarubuni kwenda kwenye nyumba yake iliyopo Montana mtaa wa Princess, mara nyingi alikuwa anawakaribisha kinywaji au kuwakodia gari.
Huwa anawalewesha kabla ya kuwafanyia vitendo vya ajabu huku wakiwa hawajitambui. Wengi wao wanapoamka huwa hawakumbuki kile ambacho kiliwatokea.
Wanafunzi ambao walikataa hukumu hiyo walidai kuwa waliridhia kupigwa picha huku wakijidai kuwa walikuwa wamesinzia ,jambo ambalo jaji alidai kuwa ni utetezi wa kipuuzi na uongo.
Katika shauri la kesi za awali, jaji alisema kuwa ana uhakika kuwa Sanaga alikuwa anatumia fomu inayoonyesha namna alivyowabaka watu.
Miongoni mwa watu waliofanyiwa vitendo hivyo vya kinyama na Sinaga, mmoja anasema kuwa ameharibiwa sehemu kubwa ya maisha yake na mwingine anasema kuwa anatamani mtu huyo asitoke gerezani maisha yake yote.
"Kuna wakati ambao nnashindwa kuamka na kufanya shughuli zangu za siku," mwingine aliongeza.
Watuhumiwa wengi walikuwa hawafahamu kuwa walibakwa mpaka walipotaarifiwa na polisi.
Lisa Waters, mtaalamu wa masuala ya ngono, anasema kuwa waathirika wa matukio hayo wanapopata msaada huwa baadhi ya wanaume wanakuwa katika wakati mgumu sana, wengine upata hata matatizo ya afya ya akili.
Sinaga, alikuwa mwanafunzi wa shahada ya uzamivu katika chuo kikuu cha Leeds, mahali ambapo alikuwa anafanya matukio hayo ya ubakaji kwa miaka kadhaa.
Mbakaji alikamatwa mwezi juni 2017 wakati muathirika mmoja alipodai kuingiliwa kimwili wakati akiwa ameleweshwa na kupoteza ufahamu, alipambana na Sinaga na kuwapigia polisi.
Afisa polisi alipochukua simu ya Sinaga alipomkamata alikuta amepiga picha nyingi za video zikiwa zinamuonyesha akiwaingilia watu mbalimbali, video hizo zilichukua mamia ya saa.
Ugunduzi wa matukio hayo katika video yalisababisha maswali kuibuka kuwa inawezekana mbakaji huyo akawa amevunja rekodi ya ubakaji ya Uingereza.
"Tunadhani mtuhumiwa alifanya makosa hayo kwa muda wa miaka 10" alisema.
"Taarifa na ushahidi unaonyesha wazi kuwa alifanya uhalifu huo kwa watu."
Wapelelezi walifuatilia pia simu zake ambazo ziliwahi kuibiwa, vitambulisho vyake na saa.