Usonji ni hali ambayo ubongo
unashindwa kufanya kazi ya kutambua mazingira kwa hiyo mtoto anakua kwenye
mazingira yake yeye mwenyewe
Dalili za usonji kwa watoto(autism)
Mtoto kuonesha tabia tofauti na
watoto wengine mfano anaweza kua pekeyake pekeyake au kwenye mazingira yake
yeye mwenyewe
mtoto ataonesha tabia tofauti
sana ukilinganisha na watoto wengine wa rika lake
Wataalam wanazungumzia nini kuhusu usonji?
Wataalam wanazungumza kua tatizo
hili huwa lina gundulika mara nyingi mtoto anapofikia umri wa miaka mitatu
Je usonji unaweza kuutambua mapema?
Ndiyo,usonji unaweza kuutambua
mapema hata mtoto akifikisha miezi sita ikiwa unamfuatilia kwa karibu
Je, utatambuaje kama mtoto amekumbwa na tatizo la usonji?
-Utakapokua unamnyonyesha anaweza
akawa ananyonya kwa nguvu sana au anabana nyonyo sana
-Ukitaka kumvalisha au
kumbadilisha nepi anaweza akawa mkali sana
-Ukimgeuza tuu kidogo anaweza
akalia sana
-Mtoto kwa kawaida anatakiwa
kucheka akisha fikisha mwezi baada ya kuzaliwa,lakini mtoto ambaye anadalili za
kuonesha usonji kucheka kwake huwa ni tabu sana au hata kuonesha kucheka kwake
hua ni tabu sana
-Huonesha kukasirika sana
-Haoneshi mawasiliano kwa mama
mfano wakati mama akitaka kucheza nae wakati anamyonyesha au kumbadilisha nguo
-Hizo ni dalili za awali ambazo
unaweza kuzitambua ni kwa nini mtoto anakua mkali kwenye vitendo vya kawaida
vya kila siku.
-Jinsi mtoto anavyokua ndivyo
usonji unavyozidi kukua
-Inafika hatua mtoto kushindwa
hata kuzungumza na ndio maana wataalamu husema kwamba usonji hugundulika kwa
miaka mitatu kwa sababu ni kipindi ambacho mtoto anapaswa kuzungumza lakini
mtoto mwenye usonji kufikia kipindi hiki cha miaka mitatu hua mara nyingi hushindwa
kuzungumza
-Huchagua sana vyakula
-Wakati mwingine akianza kutembea
hua anatembelea vidole tuu
-Hupenda kupanda sana juu ya vitu
vilivyoinukaa mfano juu ya meza juu ya dirisha na akishapanda huganda hapo kwa
muda mrefu bila kuachilia wala kudondoka
-Anaweza asiwajue anaoishi nao
hata mama yake na baba yake au hata mazingira ya nyumbani huyapoteza kumbukumbu
kwa haraka
Ni sehemu gani kwenye mwili huhusika sana na tatizo la usonji?
Ubongo huhusika sana na usonji
kwa sababu hisia ndio chakula cha ubongo kwa sababu ili ubongo uweze kufanya
kazi vizuri ni lazima hisia zinazofika kwenye ubongo ziwe nzuri yaani
zisizoathirika zisiwe nyingi sana au kidogo sana kwa sababu hisia zinafanya kzi
kwa uwiano ulio sawa
SABABU ZINAZOWEZA KUPELEKEA MTOTO
KUWA NA USONJI
-Njaa kali
-Mama kua na msongo wa mawazo
kipindi cha ujauzito
TIBA YA USONJI
-Mzazi unapaswa kua karibu sana
na mtoto endapo utagundua tabia tofauti kwa mtoto wako
-Mpeleke mtoto kwenye kituo cha
afya pindi tuu uonapo dalili za usonji
-Mzazi unapaswa kumruhusu mtoto
kucheza ili kukuza milango yake ya fahamu
-Afya ya mama mjamzito inachangia
kwa kiasi kikubwa kumlinda mtoto asikumbwe na usonji
Tags:
MAGONJWA YA WATOTO