Vidonda kooni kwa watoto na matibabu yake

Image result for vidonda kooni kwa mtoto
Vidonda kooni

Vidonda kooni kawaida hutokana na mafua. Koo linaweza kuonekana jekundu kwa ndani na kutoa maumivu mtoto anapojaribu kumeza chakula. Vifindo (vifindo 2 ambavyo huonekana kama uvimbe katika kila upande nyuma ya koo) vinaweza kuongezeka ukubwa na kutoa maumivu au hata kujaa usaha.

Matibabu

Mpe juisi za matunda kwa wingi, chai na vyakula vyenye asili ya majimaji.
Mfundishe mtoto kusukutua kwa kutumia maji ya vuguvugu yenye chumvi. (Koroga chumvi ½ kijiko cha chai kwenye glasi ya maji).
Mpe parasetamo kupunguza maumivu.
Kwa koo lenye vidonda, dawa za antibotiki hazitasaidia na hazipaswi kutumika. Lakini aina moja ya vidonda vya kooni miongoni mwa watoto ambayo husababishwa na maambukizi ya bakteria ya streprotokokasi ni hatari na hupaswa kutibiwa kwa kutumia penisilini.

Dalili ya vidonda vya kooni ambavyo husababishwa na bakteria (ya streprotokokasi)

Uvimbe na usaha sehemu ya nyuma ya koo
Uvimbe au maumivu kwenye matezi shingoni na chini ya masikio
Homa
Hakuna kikohozi au kutokwa kamasi
Kama mtoto ana dalili hizi 3 au 4, huenda vidonda kwenye koo lake vimetokana na maambukizi ya bakteria za streprotokokasi. Anapaswa kutibiwa na penisilini au amoksilini ya vidonge kwa siku 10, au kupewa sindano 1 ya penisilini benzathini (benzathine penicillin). Utaratibu wa kimaabara wa kuotesha vimelea vinavyosabaisha maambukizi kooni (throat culture) ndiyo njia ya uhakika zaidi ya kujua chanzo cha vidonda vya kooni. Utaratibu huu unapaswa kutumika pale unapowezekana.

Visipotibiwa, vidonda vinavyosababishwa na bakteria kooni hugeuka kuwa ugonjwa hatari wenye maumivu makali ambao hujulikana kama homa ya rumatizimu (rheumatic fever).

Post a Comment

Previous Post Next Post