Binti wa mwanasiasa wa nchini Kenya Raila Odinga, bi Rosemary Odinga arejesha uwezo wa kuona baada ya miaka miwili

Rosemary Odinga, binti yake kiongozi wa chama cha ODM nchini Kenya Raila Odinga, amefichua kuwa kwa sasa amerejesha uwezo wake wa kuona baada ya kutoweza kuona kwa muda wa miaka miwili..
Bi Rosemary Odinga alipoteza uwezo wa kuona, baada ya kupatikana na uvimbe kwenye ubongo ambao ulitolewa, lakini awali madaktari wakamwambia hatakua na uwezo wa kuona.
Mtoto huyo wa kike wa Odinga alitangaza taarifa ya kuwa na uwezo wa kuona mbele ya Wakristo wa kanisa la St.peters ACK mjini Bondo Siaya Kaunti katika ibada ya Krismas, ambapo alisema amepitia kipindi kigumu cha kutoweza kuona.
''Nilijihisi niko peke yangu, na nilikua nimejifunza haraka kutambua sauti na hatua za watu ili kujua ni nani aliye karibu yangu'', amesema.
Alikumbuka jinsi hususan kama mama alivyoshindwa kuwaona watoto wake.
''Watu waliniona na kudhania nina uwezo wa kuona macho yangu yalikua 'yamekodoa wakati wote'. Ninashukuru kwa sala zenu na uungaji mkono wakati wa kipindi hicho kigumu'', alisema.

Ilikua ni changamoto kubwa kwa familia:

Bw Raila Odinga alisema kuwa familia yake ililazimika kuhama kutoka hospitali moja hadi nyingine za ndani na nje ya nchi, kutafuta matibabu.
''Tulifikia wakati ambapo karibu tukate tamaa baada ya kutopata mafanikio yoyote katika hospitali nyingi zikiwemo za Ujerumani, Uchina na Afrika Kusini," alisema.
Rosemary Odinga kabla ya kurejesha uwezo wa kuona, anasema alisikitishwa na kutoweza kuwaona watoto wakeHaki miliki ya pichaROSEMARY ODINGA/FACEBOOK
Image captionRosemary Odinga kabla ya kurejesha uwezo wa kuona, anasema alisikitishwa na kutoweza kuwaona watoto wake
Bw Odinga alisema kuwa kupona kwa binti yake ilikua ni moja ya mafanikio yaliyofikiwa na familia yake mwaka huu ambayo wanashukuru.
"Madaktari nchini Afrika Kusini walisema kuwa hataweza kuona tena. Hatahivyo, rafiki alitupeleka kwa daktari nchini India anayetumia dawa za mitishamba ili kumsaidia kupona ," alisema.
Alisema Rosemary alilazwa hospitalini nchini India kwa mwezi mmoja.
"Aliporudi baada ya miezi miwili kwa uangalizi, daktari alishangazwa na jinsi alivyokuwa akipona haraka ," alisema Bw Odinga.
Taarifa ya Bi Rosemary Odinga kurejesha uwezo wake wa kuona imeibua hisia katika mitandao ya kijamii nchini Kenya:

Ugonjwa ulimzuwia kutimiza azma ya kisiasa

Kuugua kulimlazimisha Bi Rosemary (kushoto)kujiondoa katika kinyang'anyiro cha kisiasa cha kuwania kiti cha UbungeHaki miliki ya pichaROSEMARY ODINGA/TWITTER
Image captionKuugua kulimlazimisha Bi Rosemary (kushoto)kujiondoa katika kinyang'anyiro cha kisiasa cha kuwania kiti cha Ubunge
Tangu alipougua kutokana na uvimbe uliomsababishia kupoteza uwezo wa kuona mwezi Februari, 2017 Bi Rosemary hakuonekana mbele ya umma.
Kuugua kulimlazimisha kujiondoa katika kinyang'anyiro cha kisiasa cha kuwania kiti cha Ubunge wa eneo bunge la Kibra kabla ya uchaguzi wa mwaka jana.
Ripoti za awali zilisema kuwa alikua na uvimbe kwenye ubongo na Februari 28 2018 akasafirishwa kwa ndege hadi nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
Alirejea nchini Mwezi Mei mwaka jana.

Post a Comment

Previous Post Next Post