Mwanamke raia wa Uchina aishtaki hospitali iliyokataa kugandisha mayai yake ya uzazi

Teresa XuMwanamke raia wa Uchina ameishtaki hospitali baada ya madaktari kukataa kugandisha mayai yake ya uzazi kwasababu hajaolewa, jambo linaloendana na sheria ya njia za uzazi zisizo asili.
Teresa Xu aliwasili katika hospitali moja inayoshughulikia masuala ya kina mama mwaka uliopita, akiwa na nia ya kugandisha mayai yake katika kipindi ambacho anataka kuweka kipaumbele kwa taaluma yake.
Mwanamke huyo ambaye ni mwandishi huria mwenye umri wa miaka 31, anasema kwamba mhudumu wa hospitali hiyo alimsihi apate mtoto badala ya kugandisha mayai na kwamba baadaye akafahamishwa kuwa hawezi kuendelea na matibabu hayo.
"Nilikuja hapa kwa ajili ya kupata huduma ya kitaalam lakini badala yake nimepata mhudumu anayenisi niachane na kazi yangu kwa sasa na kupata mtoto kwanza, " Xu ameliambia shirika la habari la Reuters.
Chao Wei, msemaji wa hospitali, anasema kwamba hospitali hiyo ilikuwa inafuata sheria za serikali chini ya Tekinolojia za uzazi wa njia zisizo za asili, kwa mujibu wa gazeti la New York Times.
Jumatatu, mahakama moja huko Beijing ilisikiliza keshi iliyowasilishwa na Bi. Xu dhidi ya hospitali hiyo. Kesi hiyo ambayo inatarajiwa kuendelea kwa miezi kadhaa, imezua gumzo katika mitandao ya kijamii ya Uchina ambapo wengi wanamuunga mkono Xu.
Akizungumza baada ya kusikilizwa kwa kesi, Bi. Xu amesema: "Kwangu mimi siku hisi kama niko mahakamani peke yangu. kilichonijia ni kwamba nimesimama kupigania haki ya wanawake wengine wengi ambao hawajaolewa."
Yai la mwanamke linapungua nguvu yake kadiri anavyoendelea kuzeeka, na kufanya iwe vigumu zaidi kwa wanawake wenye umri mkubwa kupata mtoto. Kwa sasa hivi, ugandishaji wa mayai ni jambo ambalo linafanyika kwa wingi nchini Uchina huku wanawake wenye uwezo wakisafiri nje ya kupata matibabu hayo.
Mwaka 2013, muigizaji wa kike maarufu wa Uchina Xu Jinglei, alitangaza kwamba amegandisha mayai tisa ya uzazi wake. Jinglei, alisafiri Marekani akiwa na umri wa miaka 39 kupata matibabu ya uzazi wa njia zisizo za asali.
Bi. Xu anasema alikuwa akitaka kwenda nje ya nchi kupata matibabu hayo lakini imekuwa ghali mno kwake baada ya kuarifiwa kuwa gharama ya matibabu anayohitaji ni 100,000 yuan (£11,016) nchini Thailand na 200,000 yuan (£22,032) nchini Marekani.
Watuamiaji wengi wa mtandao wa kijamii wa Weibo walimuunga mkono Bi. Xu kwa kutumia hashtag yenye maneno sawa na "Kesi ya kwanza ya kugandisha mayai ya uzazi kwa mwanamke ambaye hajaolewa".
Mtu mmoja aliandika: "Uzazi hakustahii kuwa jambo pekee lenye kutathmni thamani ya mwanamke. Kando na kuwa mama, wewe ni mtu unayejitegemea."
Mwengine akasema: "Ikiwa sheria za Uchina zitabadilika, na iwe huru kwa wanawake ambao hawajaolewa kuwa na hifadhi ya kugandisha mayai ya uzazi! Tatizo la idadi kubwa ya watu linaweza kutatuliwa baadaye. Bado kuna wengi ambao hawataki kuolewa lakini wanataka watoto."
Kumekuwa na sheria kali dhidi ya wanawake wa Uchina tangu kuanzishwa kwa sera ya upangaji uzazi miaka ya 1970. Uchina ilibadilisha sera yake ya kuwa na mtoto mmoja hadi kuwa na watoto wawili mwaka 2015, lakini bado kuna sheria nyingi za matibabu ya uzazi na wanawake bado hawajaolewa hawaruhusiwi kugandisha mayai yao ya uzazi.
Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Weibo waliuliza kwanini mwanamke huyo anaishtaki hospitali. "Sidhani kama hospitali ina tatizo lolote katika uendeshaji wa shuguli zake. Anastahili kushtaki Shirika la Taifa la Uzazi wa Mpango badala ya hospitali," mtu mmoja amesema.
x

Post a Comment

Previous Post Next Post