Binti wa miaka 14 apata saratani ya kizazi!!

Kelliyah huhizi kuimba kunamsaidiaAlipokuwa na umri wa miaka 14- Kelliyah alianza kuhisi maumivu makali ya tumbo, na mwanzo alifikiri yanasababishwa na na vinywaji vya gesi anavotumia kwa wingi na kutofany amazoezi ya mwili.
Aliishi na maumivu hayo kwa muda wa wiki kadhaa kabla ya kwenda hospitali.
Madaktari walibaini kuwa una uvimbe wa ukubwa wa boga, na katika kipindi cha saa 24 Kelliyah alipatikana na saratani ya mfuko wa mayai ya uzazi (ovari). Madaktari walibaini kuwa uvimbe ulikuwa na uzito wa zaidi ya kilo 5
Saratani ya ovari ni nini ?
Ni moja ya saratani zinazowakumba wanawake zaidi , na nchini Uingereza pekee takriban wanawake 7,500 hupatwa na saratani hii kila mwaka- hii ikiwa ni sawa na watu 20 kila siku.
Asilimia 80 ni wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka 50 na viwango vya kupona ni vya juu zaidi kwa wanawake hao zaidi ya wanawake wenye umri mdogo. Hata hivyo inategemea saratani imesambaa kwa kiwango gani wakati inapobainika.
Katika maeneo ya England na Wales, karibu nusu ya wanawake wanaopatikana na saratani hii wanaweza kuishi kwa miaka mitano na zaidi baada ya kutambuliwa kuwa na maradhi hayo.
Hakuna vipimo vya kuaminika vya saratani ya ovari, ikilinganishwa na saratani ya mfuko wa uzazi, utumbo na ile ya matiti , kwasababu dalili zake zinaweza kuwa ngumu kuzitambua.
" Tumbo langu lilikuwa kubwa sana, lakini nikadhani nilikuwa tu naongeza uzito wa mwili," anasema Kelliyah, kutoka London.
" Nilianza kufanya mazoezi , kukimbia vilimani, kufanya mazoezi ya tumbo, kupiga push-ups, lakini hakukuwa na mafanikio yoyote.
"Halafu nikaanza kula mboga za majani , lakini tumbo langu likaendelea kuwa kubwa na kubwa zaidi '' .
"Mama yangu alisema , 'hebu ngoja niguse tumbo lako,' na akabaini kuwa lilikuwa kama kuna kitu kinachoweza kushukumwa , lilikuwa ni kama mimba .
"Baada ya hapo , Nilianza kuhisi maumivu makali, ilikuwa ni kama kuna kitu kinanichoma ndani, na sikuweza kula chakula kabisa."
"Nilitaka kujifananisha na mtu fulani."
Daktari bingwa wa uzazi kutoka hospitali ya chuo kikuu cha London Adeola Olaitan anasema : "Uwezekano wa mwanamke wa kupata saratani ya ovari maishani mwake ni wa mwanamke mmoja kati ya wanawake 50.
"Ni jambo la kawaida zaidi kwa mwanamke ambaye hajawahi kupata mwatoto, wanawake waliowahi kupata matibabu ya kutafuta watoto wale ambao hawajawahi kuwa na matatizo hayo kwa pamoja ... Wanaotumia vidonge vya kuzuia mimba, ambavyo humlinda mwanamke ambaye hajawahi kunyonyesha ."
Kelliyah alihangaika kupata taarifa mtandaoni kuhusu tiba ya saratani ya ovari na namna inavyowaathiri wanawake wenye umri mdogo na wasichana.
"Nilianza kuwaona wanawake wengi wenye saratani walio na umri wa miaka 40, 38 na nikajiuliza, ' Mimi sio mzee, ni kwa nini hakuna wasichana wadogo ?' - Nilitaka kupata uzoefu kutoka kwa mtu wa miaka yangu," anasema.
"Baadhi ya vijana wanahisi aibu ya kusema kuwa wanaumwa saratani na kuizungumzia. Ni mada nyeti kuizungumza ."
Kelliyah kwa sasa ana nafuu lakini lazima afanyiwe uchunguzi wa kimatibabu kila baada ya miezi mitatu kwa kipindi cha miaka mitano.
Anaweza bado kupata watoto lakini anakabiliwa na uwezekano wa kufikia kipindi cha ukomo wa uwezo wa kupata ujauzito mapema.
"Hali hii imenifanya nibaini kuwa kila kitu kinaweza kutokea na kwamba unapaswa kufurahia kila kitu hata kikiwa ni kidogo maishani ," anasema.
"Ninataka kufanya kila kitu sasa, sasa, sasa - muda haumngojei yeyote ."

Hukumu

Mama yake Kelliyah, Ashley Avorgah pia ana hofu juu ya unyanyapaa wa kiafya katika baadhi ya jamii za watu weusi.
"Wanaona saratani kama aibu na hawataki kudharauliwa," anasema
"Kuna ukosefu wa mawasiliano baina ya jamii yangu inapokuja katika swala la ugonjwa. Hawataki yeyote awadharau."
Kiwango cha utambuzi wa kimatibabu wa saratani ya ovari miongoni mwa wanawake wenye chini ya umri wa miaka 25 nchini Uingereza kimeongezeka kwa 85% kati ya 1993-95 na 2014-16, lakini kwa ujumla kiwango cha utambuzi wa ugonjwa huo bado kiko chini - kuna takriban ripoti 140 kila mwaka.
Ben Sundell, kutoka taasisi inayohusika na saratani miongoni mwa vijana walio katika umri wa barehe -Teenage Cancer Trust, anasema : "katika saratani ya mfuko wa mayai ya uzazi , inakuwa ni vigumu kwa mtu kushuku kuwa msichana anaweza kuwa na saratani ya mfuko wa uzazi kutokana na ukweli kwamba huwa ni nadra sana miongoni mwa watu wenye umri huo na kwa hivyo inakuwa ni vigumu kugundua dalili kwani mara nyingi dalili zake huwa ni sawa na za maumivu ya hedhi ."
Dawa ya saratani ya ovari iliyokithiri iliidhinishwa kutolewa kwa wagonjwa wapya nchini Uingereza Julai 2019. Majaribio yake yalionesha kuwa inaweza kuchelewesha kusambaa kwa maradhi hayo kwa miaka mitatu.

Post a Comment

Previous Post Next Post