Kuganda kwa damu wakati wa hedhi huonekana kama jambo la kawaida kwakuwa ni hali tu iliyo katika sehemu ya mzunguko wa hedhi. Wanawake wengi, kwa mtazamo mwingine wakati wa mizunguko yao ya hedhi hushindwa kupitisha mabonge ya damu. Baadhi ya mabonge yanaweza kuwa makubwa yenye tishu nyeupe yakiambatana kwa pamoja katika mzunguko wa hedhi wa muda mrefu, yaani siku 8-14. Hali hii inaweza kujitokeza baada ya kuporomoka kwa mimba, lakini je, ni hali ya kawaida kwa mwanamke?
Mabonge ya damu hayakupaswa kumtokea mwanamke wakati wa hedhi. Hapo chini utaona mambo gani yanayosababisha damu kuganda wakati wa hedhi, na dalili gani zinazojitokeza, na je, unaweza kuzuiaje damu isigande wakati wa hedhi?
Je, Ni Kawaida Kuwa Na Mabonge Ya Damu Wakati Wa Hedhi?
Kwa asili, wanawake wengi huwa wanapatwa na hali hii ya mabonge wanapokuwa hedhini. Lakini hata hivyo, kuna mambo ambayo kwa kawaida huonyesha kuwa unaweza kuwa na mabonge wakati wa hedhi au la. Mambo yanayoweza kusaidia kubaini tatizo hili ni kama yafuatayo:
- Uvimbe aina ya Fibroids
- Kizazi kuongezeka na kuwa kikubwa
- Uwezo wa misuli ya kizazi chako kusinyaa
- Uvimbe katika mlango wa kizazi
Vyanzo Vya Kuganda Kwa Damu Wakati Wa Hedhi
Kwanini mwanamke anatokwa na damu iliyoganda wakati wa hedhi? Na nini husababisha damu kuganda wakati wa hedhi? Kwa ujumla, chanzo cha kuganda kwa damu wakati wa hedhi yako hutokana na kushindwa kwa kutoka kwa ute wenye kemikali unaozuia kugandanda kwa damu(anticoagulants) ili kuukinga ukuta wa kizazi usiharibike. Wakati wa hedhi, ute ute mzito unakuwa kwenye ukuta wa kizazi huanza kutoka. Ute huu unaokuwa na kemikali huanza kuachiliwa ili kuzuia damu isigande wakati wa hedhi. Wanawake wengi wanaotokwa na damu ya hedhi muda mrefu hutoka na damu yenye mabonge kwasababu damu inayotoka kwenye ukuta wa mfuko wa kizazi(uterus) hutoka kwa kasi kuliko ute wenye kemikali(anticoagulants) unazuia damu isigande. Hali hii ndio husababisha damu kuganda na hedhi kutoka na mabonge ya damu kwa muda mrefu.
- Uvimbe Katika Kizazi(Uterine Fibroids)
Uvimbe mmoja au zaidi ambao huwa sio salatani, kwa kawaida huota ndani ya kizazi cha mwanamke. Hata hivyo kwakuwa sio salatani, huwa havionyeshi kuwa vimetulia tu. Dalili za kawaida anazozipata mwanamke mwenye uvimbe aina ya fibroids ni kama ifuatavyo:
- Maumivu ya tumbo chini ya kitovu
- Maumivu wakati wa tendo la ndoa
- Kutokwa na damu ya hedhi muda mrefu
- Tumbo kujaa gesi ama kukosa choo
Ikiwa kama umewahi kuwa na dalili yoyote au zote nilizozitaja hapo juu, yafaa ukaenda hospitali haraka ili kufanya vipimo katika tumbo lako la kizazi. Daktari takuambia ikiwa kama una tatizo la uvimbe kabla hujapata utaratibu wa matibabu.
- Mpango Wa Uzazi Pamoja Na Kutokwa Na Mabonge Ya Damu Wakati Wa Hedhi
Mwili wa mwanamke umekuwa ukipokea vichochezi vya uzazi wa mpango kwa utofauti mkubwa sana, kwa mfano; vidonge vya uzazi wa mpango, nk. Kwa hali hiyo, wanawake hao wanapoingia hedhini hutokwa na damu kwa muda mrefu zaidi ya siku 8 na kuendelea.
Unaweza ukatambua kuwa unatokwa na damu ya hedhi nyingi kwa kuangalia idadi ya pedi unazobadirisha kwa siku. Ikiwa kama unapaswa kubadirisha pedi zaidi ya mara moja kila baada ya masaa mawili au kama mtiririko wa damu yako ya hedhi una mabonge makubwa ya damu yasiyokuwa ya kawaida, basi inamaanisha kwamba unatokwa na damu nyingi mno.
Endapo kama utagundua kuwa mtiririko huo wa damu ulianza tu kipindi ulipoanza kutumia aina mpya ya vidonge vya mpango wa uzazi, basi unapaswa umweleze daktari wako akupe usahuri kuhusu jambo hilo.
- Kuporomoka Kwa Mimba
Kati ya asilimia 15-20 za ujauzito, mara nyingi huishia kuporomoka kabla haujafikisha wiki ya ishirini. Mabonge ya damu huwa ya kawaida sana wakati mwanamke mimba inapoporoka. Hata hivyo, kama ukigundua kuwa ulitokwa na mabonge kwa kipindi cha mwezi mmoja, lakini yakaendelea mwezi uliofuata, basi usishangae kuona kuwa mimba iliporomoka, ikiwa pia kama kuna mabadiriko badiriko kwenye mzunguko wako wa hedhi.
- Kukaribia Kukoma Kwa Hedhi
Hali ya kukoma kwa hedhi mara nyingi huambatana na kutokwa na mambonge mengi ya damu wakati wa kipindi cha hedhi. Hii ni hatua ambayo huonekana kabla ya kuanza kukoma hedhi(menopause). Mwanamke anapokuwa katika hatua hii, utagundua kuwa mwili wake utazarisha vichochezi(hormone) aina ya progesterone kwa viwango tofauti. Wakati uzazrishaji wa vichochezi(hormone) vya progesterone unapopanda na kushuka, viwango vya vichochezi(hormone) vya estrogen vitaanza kupanda na kufikia viwango ambavyo visingeweza kuchukuliwa taarifa hapo nyuma, na hali hii inaweza kusababisha kukua na kuvimba kwa tishu za ukuta wa kizazi.
Tishu za ukuta wa kizazi baadaye husababisha damu kuganda na kutokwa na damu nyingi muda mrefu wakati wa hedhi. Hivyo basi, naomba usishikwe na hofu kwakuwa umefikia hatua ya kukaribia kukoma hedhi. Endapo utaona hali ya mbonge ya damu sio ya kawaida, hakikisha kuwa unawahi hospitali kumuona daktari.
- Mabonge Ya Damu Yasiyo Ya Kawaida
Unapoona mabonge madogo ya damu iliyoganda wakati wa hedhi, chanzo chake kinaweza kuwa damu iliyoganda isiyokuwa ya kawaida. Magonjwa mbalimbali ya kuridhi yamekuwa yakifahamika kuwa yanaweza kumfanya mwanamke kupatwa na tatizo la kutokwa na damu muda mrefu. Kwa mfano, ugonjwa wa Von Willebrand, ni moja ya ugonjwa huo.
- Unapokuwa na ugonjwa huo, siku zako za hedhi zinaweza kuwa nyingi
- Siku zako za hedhi zinaweza kuambatana na vibonge vidogovidogo vya damu.
Mwanamke mwenye ugonjwa wa kurithi hujeruhiwa kwa urahisi sana. Kwa nyongeza, anaweza kupata tatizo la kutokwa na damu siku zote mara kwa mara, kwa mfano; damu kutoka kwenye fizi au puani, hali ambayo inaweza kuwa ya muda mrefu. Moja ya masomo ambayo wanawake wote wanahitaji kuyakumbuka ni kwamba, kadiri damu inavyozidi kuganda na kutengeneza mabonge ya damu mabaya, usiwe na hofu, yawezekana mabonge hayo yanakuonyesha jambo fulani kuhusiana na afya yako.
- Maambukizi
Aina ya kwanza ya maambukizi yanayoweza kusababisha hali hii ya kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi ni maambukizi katika via vya uzazi(PID). Maambukizi ya aina hii huathiri viungo vya uzazi kwa mwanamke, na kama tatizo hili litaendelea bila kufahamika vizuri, basi linaweza kusababisha uharibifu mkubwa katika mfumo wa uzazi wa mwanamke. Hata hivyo, matatibabu yake yatatakiwa kuwa dawa za antibiotic