Je! ni kweli ebola imeingia Tanzania?

Maafisa wa afya wakipambana na Ebola nchini DR Congo
Serikali ya Tanzania imefutilia mbali uvumi kwamba kuna visa vya ugonjwa wa Ebola nchini humo.
Waziri wa afya nchini humo bi Ummy Mwalimu aliambia mkutano na wanahabari mapema leo kwamba hakuna kisa hata kimoja cha ebola katika taifa hilo.
Kumekuwa na tahadhari na madai ya kuwepo kwa kisa cha ebola nchini humo.
Shirika la Afya Duniani WHO lilituma kundi la wataalamu kuchunguza kisa cha ugonjwa usiojulikana na ubalozi wa Marekani ulifuatilia hatua hiyo kwa kutoa tahadhari .
Hatua hiyo ilisababisha uvumi katika mitandao ya kijamii kwamba ugonjwa huo hatari umeingia nchini Tanzania.
Alisema kwamba taifa hilo limejiandaa kukabiliana na mlipuko wowote wa ugonjwa na tayari limefanya majarabio ili kujua jinsi ilivyojiandaa huku ikiweka tayari vituo vya kuwatenga waathiriwa.
Waziri huyo pia alionya kwamba wale ambao wataendelea kusambaza uvumi huo wa uwongo kuhusu kisa hicho watachukuliwa hatua kali za kisheria kupitia sheria ya uhalifu wa mtandaoni.
Uvumi wa visa vya ebola nchini tanzani unatokana na visa viwili vya wagonjwa waliokuwa tukiwashuku.
''Nataka kuwahakikishia kwamba idara ya afya ilichukua sampuli na matokeo yake ni kwamba wawili hao hawakuwa na ugonjwa wa Ebola. Hakuna Ebola Tanzania na watu hawafai kuwa na wasiwasi'', alisema Mwalimu.
Mwaka 2014 kulikuwa na uvumi kama huo nchini Tanzania ambapo kulikuwa na wagonjwa waliotiliwa shaka kuwa na ugonjwa huo.
Wagonjwa hao waliohisiwa kupata maambukizo kutokana na dalili za awali, walikuwa raia wa Benin na Mtanzania, lakini vipimo vilionyesha kwamba hawakuwa na maambukizo hayo.

Msururu wa matukio ya mgonjwa aliyeshukiwa kuwa na Ebola

Tarehe 10 Septemba 2019, Shrika la Afya duniani WHO lilipokea ripoti ya taarifa ya kisa cha mambukizi ya Ebola mjini Dar es Salaam, Tanzania.
Kisa hicho kinachoshukiwa kilimhusu mwanamke mwenye umri wa miaka 34 ambaye alikuwa akisomea nchini Uganda.
Aliwasili nchini Uganda akitokea nchini Tanzania tarehe 08 Agosti 2019.
Taarifa hiyo inasema kwa kuanzia tarehe 08 hadi 22 Agosti, alikuwa katika eneo la kati la Uganda, akiishi katika hosteli ya kibinafsi karibu na mji mkuu Kampala .

Je Shirika la afya duniani linasemaje?

Kulingana na shirika la WHO alitembelea vituo vya afya katika eneo hilo alipokuwa akifanya utafiti wake wa kimasomo kwa ajili ya kufuzu masomo yake.
Hata hivyo inaaminiwa kuwa hakuna visa vya ugonjwa wa Ebola vilivyokwisha ripotiwa mjini Kampala, na hata katika maeneo ya kati ya Uganda.
WHO linasema tarehe 22 Augusti 2019, alirejea nchini Tanzania. Alisafiri hadi mjini Mwanza kaskazini mwa nchi , halafu akaenda Dar es Salaam na alikuwa akisafiri mara kwa mara katika maeneo ya Kusini magharibi yaani ya Mtwara au Songea .
Alipatikana na dalili za ugonjwa huo tarehe 28 Agosti (kichwa, joto, upele, na kuharisha damu ) na kutafuta matibabu katika kliniki ya kibinafsi ambako kwa mara ya kwanza alipatikana na ugonjwa wa malaria. Hakupona na matibabu yakasitishwawa wa with malaria. Hakupona na hivyo matibabu yakasitishwa.
Tarehe 5/6 Septemba, alisafiri kurudi Dar es Salaam, ambako alilazwa tarehe 7 Septemba katika mojawapo ya hospitali za rufaa za mkoa.
Baada ya kushukiwa kuwa na virusi vya homa ya Ebola , alihamishiwa kwenye kitengo maalum katika hospitali nyingine ya rufaa -Temeke ETU- kwa uangalizi zaidi ,na sampuli za vipimo vyake zikachukuliwa. Tarehe 8 Septemba 2019, mgonjwa huyo alifariki, na mazishi yaliyosimamiwa yalifanyika siku hiyo hiyo.
Tarehe 11 Septemba 2019, kwa mujibu wa duru zisizo rasmi , kipimo cha RT-PCR kilichochukuliwa katika maabara ya kitaifa ya Tanzania-n National Health Laboratory kilionyesha matokeo chanya ya virusi vya EVD.
Leo , taarifa hii haijathibitishwa wala kukanushwa na mamlaka za taifa . Wakati maambukizi ya Ebola EVD hayajathibitishwa katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania , Kufanya vipimo tena vya homa ya Ebola katika maabara inashauriwa sana ili kuthibitisha matokeo ya vipimo na hivyo kubaini aina ya virusi Ebola . WHO linasema kuwa limewapatia maafisa wa Tanzania ushauri huu.
Serikali ya Tanzania ilivyojiandaa kukabiliana na kisa chochote cha ugonjwa wa ebolaHaki miliki ya pichaWIZARA YA AFYA TANZANIA
Utambuzi wa watu ambao mgonjwa aliwasiliana nao umekwisharipotiwa kwa njia isiyo rasmi na "wamewekewa karantini." Hakuna taarifa za ziada zilizopo.
Mahali ambapo mgonjwa alibainika kukutana na watu wengine hakujajulikana .
Shirika hilo la afya dunianin linasema kuwa tarehe 11 Septemba 2019, WHO lilipokea ripoti ambazo hazikuwa rasmi kuhusu mfanyabiashara kutoka Mwanza ambaye alikuwa na dalili kama za maambukizi ya Ebola. Alikuwa na historia ya kusafiri katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo -DRC. Anaripotiwa kuwa hakukutana na mtu aliyepatikana na matokeo chanya ya sasa, katika kisa kilichoripotiwa mjini Dar es Salaam.
Tahadhari iliochukuliwa na serikali ya tanzania katika kukabiliana na EbolaHaki miliki ya pichaWIZARA YA AFYA TANZANIA
Kwa mujibu wa ripoti zisizo rasmi hakupatikana na virusi vya Ebola -EVD. Hata hivyo , hakuna udhibitisho rasmi kutoka Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania uliopokelewa . Zaidi ya hayo ,vipimo vipya vilivyochukuliwa katika maabara ya kimataifa ya homa ya Ebola vinapaswa kkuchukuliwa.
Wizara ya afya Tanzania ilivyojiandaa kukabiliana na EbolaHaki miliki ya pichaWIZARA YA AFYA
Tarehe 12 Septemba 2019, shirika la WHO lilipokea ripoti zisizo rasmi kuhusu mwanamke mwenye umri wa miaka 27-aliyeshukiwa kuwa na dalili za Ebola katika hospitali ya Muhimbili mjini Dar es Salaam tarehe 11 Septemba.
Alihamishiwa katika hospitali ya Temeke ETU tarehe 12 Septemba.
''Hakuna taarifa zilizopo kuhusu vipimo vya maabara na matokeo ya vipimo wala maelezo kuhusu dalili. Hakuna taarifa rasmi kutoka Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu kisa hiki kinachoshukiwa yaliyokwishapokelewa'', limesema shirika hilo la Afya duniani katika ripoti yake.

Post a Comment

Previous Post Next Post