Utafiti umebaini kuwa wanawake 300,000 duniani karibu wote kutoka nchi zinazoendelea hufa kila mwaka kutokana na upasuaji.
Utafiti, uliiongozwa na chuo cha Queen Mary jijini London, unaaminika kuwa wa kina zaidi kuhusu suala hilo kuliko tafiti nyingine zilizowahi kufanyika.
Watafiti walichambua data za wanawake wajawazito milioni 12.Na wakagundua kuwa hatari ya vifo kutokana na upasuaji katika nchi zinazoendelea iko juu kuliko walivyotarajia.
Njia hii ilikua ikisaidia kuokoa maisha ya mama na watoto wao.
Lakini katika maeneo mengi, hasa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara, sasa inaonekana kuwa ya hatari.
Idadi ya wanawake wanaopoteza maisha katika eneo hilo ni mara 100 zaidi ya nchi zilizoendelea kama vile Uingereza.
Na 10% ya watoto wote hufa wakati au baada ya upasuaji.
Utafiti huo uliochapwa kwenye jarida la masuala ya afya, Lancet unawataka wanawake katika nchi zinazokabiliwa na changamoto hizo kupata huduma nzuri za upasuaji zenye kutekelezwa na watu wenye utaalamu kuhakikisha kuwa upasuaji unafanyika kwa usalama.