Mwanamke raia wa Msumbiji ajifungua mtoto juu ya mti wakati wa mafuriko

Amélia cradles na binti yake Sara katika kituo cha msaada cha DombeHaki miliki ya pichaUN
Image captionMama Amélia alijifungua binti yake , Sara, wakati wa dhoruba ambalo liliwauwa watu zaidi ya 700
Mwanamke mmoja amejifungua mtoto juu ya mti wa mwembe alipokuwa akiyakwepa mafuriko katika eneo la kati nchini Msumbiji yaliyosababishwa na kimbunga Idai.
Mama huyo afahamikaye kwa jina la Amélia alijifungua mtoto wa kike , Sara, alipokuwa juu ya mti pamoja na mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka miwili.
Familia yao iliweza kuokolewa siku mbili baadae na majirani, kufuatia dhoruba ambayo limewauwa watu 700 nchini mwake.
Tukio hili linakuja takribani miongo miwili baada ya mtoto mwengine kuzaliwa katika mazingira kama hayo. Mtoto huyo, Rosita Mabuiango alizaliwa wakati wa mafuriko yaliyokumba maeneo ya kusini mwa Msumbiji.
"Nilikuwa nyumbani na mwanangu wa kiume mwenye umri wa miaka miwili ambapo ghafla , bila onyo lolote, maji yalipoanza kuingia ndani ya nyumba yetu," Amélia aliliambia shirika la watoto la Umoja wa Mataifa Unicef.
"Sikuwa na njia nyingine ila kukwea mti, nilikuwa peke yangu na mtoto wangu wa kiume."
Amélia na familia yake kwa sasa wanaishi katika makazi ya muda ya msaada karibu na Dombe, na wanaarifiwa kuwa katika afya nzuri.
Rosita Mabuiango, ambaye sasa ana umri wa miaka 19, aligonga vichwa vya habari za kimataifa baada ya yeye na mama yake Sofia kuokolewa na helikopta kutoka kwenye mti uliokuwa umezingirwa na maji ya mafuriko.
Akizungumza na magazeti nchini humo Mail na Guardian, Sofia alisema kuwa alikuwa na uchungu "mkali , mkali sana."
"Nilikuwa najaribu kulia , kupiga mayowe. Wakati mwingine nilifikiri mtoto alikuwa anatoka, lakini wakati mwingine nikafikiri ilikuwa ni kwa sababu ya njaa ."
Aliongeza kusema kuwa : "Watu wengi walipoteza kila kitu katika mafuriko, lakini walau nilipata kitu ."
Rosita Mabuiangoakizungumza na BBC
Image captionRosita Mabuiango pia alizaliwa juu ya mti wakati mafuriko yalipopiga eneo la kusini mwa Mshumbiji mwaka 2000
Lakini katika mazungumzo na BBC, Rosita alisema kuwa ahadi za serikali ya Msumbiji za kumlipia masomo, na ahadi ya kumlipia gharama ya safari ya Marekani iliyotolewa na serikali ya Marekani zote hazijatimizwa.
"Masomo yangu yamekuwa wakati wote yakigaramiwa na mama yangu, sijapokea chochote kutoka kwa serikali ," alisema Rosita.
"Sawa , nyumba tulijengewa na serikali lakini kwa sasa haiko katika hali nzuri. Mvua inaponyesha, nyumba inavuja. Walau wangesaidia kuikarabati ."
ramani

Post a Comment

Previous Post Next Post