Kwa sayansi ya afya iliyopo ulimwenguni hivi sasa inaleta uwezekano wa mwanamke asiye na uwezo wa kubeba mimba akawa na uwezo wa kuwa na mtoto wake mwenyewe endapo tu atakuwa na uwezo wa kuzalisha mayai yake ya kike na akawa na mwanaume ambae pia anaweza kujizalishia mbegu za kiume.
Sayansi iliyo nyuma ya hilo ni kwamba mwanaume atatoa manii zake kwa njia ya kujichua ama kwa tendo la ndoa na mke wake ambapo atapewa kondomu maalumu kwa ajili ya kukusanyia manii(kondomu hiyo si ya kawaida ni ile iliyotengenezwa kwa silicon hivyo ni ghali).
Na mwanamke atafanyiwa aspiration(yaani kuvutwa kwa yai kutoka katika ovari zake).
kisha yai litatengenezewa mazingira ya kurutubishwa nje ya mwili wa mwanadamu kwa kutumia mbegu za mwanaume husika basi siku ya tatu baada ya urutubishwaji embryo itatengenezwa na siku hiyo ya tatu ndipo atatafutwa mdada ama mwanamke mwingine aliyejitolea na atawekewa iyo mimba na iatakuwa ndani ya mji wake wa mimba japo mtot atakae zaliwa ni wa mama aliyetoa yai. natumai umependa dondo ya leo. karibu
Tags:
DONDOO YA SIKU