Jinsi ya kupunguza tumbo baada ya kujifungua

Kwa sasa utakua unafurahia sana ujio wa kichanga chako, una furaha sana kuwa mama. Ujauzito umekupatia zawadi bora na ya milele, zawadi ya mtoto, lakini pia umekupatia kitu kingine cha ziada ambacho hujakipenda, nacho ni ongezeko la uzito kutokana na ujauzito.
Hakika utahitaji kupunguza uzito wa mwili wako lakini  hakikisha unafanya hivyo katika njia iliyo salama kinyume na hapo unaweza kumuumiza mtoto kwa kumkosesha chakula kama utajinyima chakula (diet) na kusababisha mtoto kukosa maziwa pia utaidhuru afya yako, ni vema kama utapunguza uzito zingatia njia asili na salama.
Zifuatazo ni njia 20 za kupunguza uzito baada ya kujifungua:
 1. Kula mara kwa mara
Unaweza kudhani kuacha kula ni njia sahihi ya kupunguza uzito kwa haraka lakini kwa bahati mbaya hii inaweza kuleta matokeo tofauti. Ukiwa kama mama mpya una mengi ya kuhofia kiasi kwamba mawazo yatazidi, utashindwa kula kwa usahihi, mawazo yataongezeka na kufanya uzito wako kuongezeka.
Hakikisha unakula mlo kamili na wenye afya kuliko kuacha kula kabisa. Hii inaweza kuwa njia bora ya kupunguza uzito.

 1. Kula mara nyingi kwa kiasi kidogo kidogo
Kuliko kula mara tatu kwa kiasi kikubwa kwa siku, kula milo sita katika kiasi kidogo kidogoWeka kiasi kidogo cha chakula ambacho hautashiba kwa mara moja. Kula milo sita kuliko mitatu kwa siku pia itakusaidia mda wote kutokuhisi njaa.

 1. Kula vyakula vyenye kiasi kidogo cha mafuta.
Ukiwa tayari ni mama mpya mwili wako unahitaji virutubisho vya kutosha kwa ajili ya kulinda afya yako na kutengeneza maziwa kwa ajili ya mtoto. Epuka kula chakula ambacho kitakushibisha lakini kisiwe na kazi mwilini. Kula vyakula vyenye omega 3, asidi ya fati, kalsiam, protini, na vyakula vya nyuzi nyuzi kama samaki, nyama isiyo na mafuta,kuku, mayai,maharagwe,kunde,mtindi na vyakula vya mbegumbegu. Epuka vyakula vyenye mafuta mengi. Ulaji huu mzuri utasaidia kupunguza uzito.

 1. Kunywa maji mengi
Hakikisha unakunywa angalau glasi 8 hadi 10 za maji kila siku, hii itasaidia kutoa sumu mwilini. Kunywa maji kwa wingi kunasaidia kuondokana na ukosefu wa maji mwilini na kuimarisha metabolic (uvunjajivunjaji wa kemikali mwilini) ambayo husaidia kuweka sawa uzito wa mwili. Husisha vimiminika katika mlo wako wa kila siku kama vile maziwa, mchuzi, supu na maji ya matunda.

 1. Anza mazoezi
Ukiwa kama mama mpya una mengi ya kuzingatia lakini ni muhimu kuweka ratiba ya mazoezi katika ratiba yako ya siku. Zungumza na daktari kujua ni wakati gani sahihi kwako kufanya mazoezi. Fanya mazoezi mepesi nay a kawaida kuepuka uchovu na kujiumiza. Mazoezi ambayo unaweza kujaribu ni kama kutembea, kukimbia, kuogelea na yoga

 1. Pata mapumziko
Ukiwa kama mama mpya si rahisi kulala kwa masaa8 moja kwa moja ila jitahidi upate mda wa kupumzika. Kukosa muda wa kupumzika kunaweza kuathiri “metabolic” yako na kukwamisha zoezi lako la kupunguza uzito. Jaribu kutafuta msaidizi wa kazi ili mtoto anapolala upate mda wa kupumzika pia, unaweza kumkamulia maziwa mtoto kwenye chupa na kumuonesha mwenza wako jinsi ya kumnywesha.

 1. Kupunguza uzito kwa kumtumia mwanao
Huna haja ya kwenda sehemu maalumu ya kufanyia mazoezi (gym) wala huhitaji mazoezi magumu. Unaweza kumtumia mwanao kupunguza uzito. Muweke mwanao kifuani ukiinama na kuinuka kila siku,hakikisha daktari amekubaliana na hilo hilo.Njia nyingine bora zaidi ni kumuweka mtoto mgongoni kisha panda na kushuka chini ukiwa umejilaza.

 1. Angalia vitafunwa unavyokula
Ukiwa kama mama mpya ambaye unanyonyesha utakua unahisi njaa zaidi kuliko mwanzo. Ina maana kwamba utahitaji vitu vya kutafuna zaidi. Vitafunwa unavokula vinaweza kupunguza au kuongeza uzito wako.Pamoja na chakula chenye afya, katika orodha ya vyakula vyako ni vizuri jumuisha na vitafunwa kama vile nazi, matunda yaliyokatwakatwa, aina zote za nafaka, viazi vitamu vilivokaangwa na mchanganyiko wa mtindi.

 1. Punguza mawazo
Kuwa mama mpya kunakuja na majukumua mengi pamoja na hofu, unapaswa kuwa mtulivu na kupunguza kuwaza. Mawazo yanaweza kukwamisha zoezi lako la kupunguza uzito hivyo ni vema kupunguza mawazo. Muombe mwenza wako  akusaidie katika uangalizi wa mtoto ili ujipe mda wa kupumzika uwezavo, pumzika ili upunguze mawazo au fanya vitu ambavo vitakusaidia kuondoa mawazo. Hii ni njia bora ya kupunguza uzito baada ya kujifungua.
 1. Kucheza
Kucheza kutasaidia kupunguza mafuta mwilini. Weka mziki au kitu chochote ambacho kinaweza wafurahisha wewe na mwanao na kufanya mcheze. Haijalishi kama unajua miondoko ya mziki au haujui, cheza hadi utoe jasho mwilini.
 1. Mchanganyo wa mtindi na vitafunwa
Unapojihisi uchovu na hamu ya kula kula jitahidi kula vitu vitamu vyenye afyaWeka mtindi kwenye jokofu pamoja na nazi na matunda yaliyokatwa katwa. Pia unaweza kuongeza vyakula kama vanilla na kutengeneza mchanganyo. Kula mchanganyiko wako wa mtindi. Inaweza kua njia bora ya kupunguza uzito.
 1. Kunywa maji kabla ya kupata chakula
Kama unajihisi unakula kwa kiasi kikubwa kuliko unavohitaji ni vema ukanywa maji kabla ya chakula, hili linaweza kuwa jibu sahihi. Taratibu kunywa maji glasi iliyojaa kabla ya kuanza kula chakula. Itasaidia kujaza tumbo na utakula kiasi cha chakula utakacho, kinyume cha kula sana utakula kiasi kinachohitajika mwilini na kujihisi umeshiba.
 1. Punguza baadhi ya vyakula
Kwa kawaida kuna mazingira unaweza kushawishika kula sana pasipo na maana. Anza kupunguza kula vitu ambavo havina msaada mwilini na katika afya yako. Kama unakula wali au kachumbali epuka jibini na utumie mboga za majani kwa wingi.

 1. Kula mapema
Jitahidi kula cha kula cha jioni dakika za mwisho za jioni na siyo usiku. Kama inawezekana kula chakula cha jioni saa 1 na saa 1 na dakika 30 jioni , uwe umemaliza kabla ya saa 2 usiku,hii itakuza  “metabolic” yako na kupelekea kupunguza uzito. Kama unakaa macho hadi majira ya usiku sana, kunywa  glasi ya maziwa au chai ya rangi. Kula mapema ni njia bora ya kupunguza uzito baada ya kujifungua.

 1. Tembea pindi uwezavyo
Kama una ratiba ya kufanya mazoezi katika ratiba yako ya siku unahitaji kufanya matembezi ya kawaida. Jaribu kutembea kadri uwezavo,hata kama utatakiwa kumchukua na mtoto. Unaweza kutembea na mtoto bustanini, katika viwanja vya mazoezi, madukani au sokoni, au unaweza kumlaza mikononi mwako wakati unaizunguka zunguka nyumba.

 1. Jipe muda mwenyewe
Uliongezeka uzito katika kipindi cha miezi tisa ya ujauzito hivo usifikirie kupungua kwa mda wa mwezi mmoja tuu baada ya kujifungua. Mwaka wa kwanza mtoto kuzaliwa utakua mwaka mgumu kwako na itakuchukua muda kupunguza uzito. Usikate tamaa na kupunguza kasi ya kufanya mazoezi hata kama unaona hupungui, endelea kufanya mazoezi sahihi na kwa utaratibu, usijipe mawazo endelea kujitahidi na kujipa moyo kuwa bado miezi michache ufike unapohitaji.

 1. Fanya manunuzi sahihi
Ni rahisi kupata matamanio vyakula vitamu kama chokleti vinapo kuwa mbele yako. Hakikisha unaepuka vitu vitamu kama chokolati,ice creams na vitafunwa vingine vinavoongeza uzito, kama unahisi kutamani vinapokua kwenye jokofu epuka kununua. Kama unadhani ni vitu pendwa sana kwako na utataka kununua utakapoviona,muombe mwenza wako afanye manunuzi kwa ajili yako.

 1. Epuka kahawa na vilevi
Unaweza kudhani kikombe cha kahawa kitakusaidia kuondoa usingizi lakini kinaweza kuzuia uzito kupungua. Hata ikiwa umeacha kunyonyesha epuka kunywa pombe au jaribu kunywa chini ya chupa 2 kwa wiki. Kama unajihisi uchovu na unatamani kunywa kitu, kunywa kikombe cha chai ya majani au kahawa.

 1. Pata chakula cha nyumbani
Ingawaje ni sawa kula nje, jitahidi upate chakula nyumbani kadri uwezavyo. Kula nje kunaweza kusababisha ukatamani kula chakula ambacho unajua si rafiki kwa uzito wako. Ikiwa utahitaji kula nje jitahidi ule mara moja kwa wiki au wiki mbili. Kula nyumbani ni njia bora ya kupunguza uzito baada ya kujifungua.
 1. Hamasika
Kama ulikua na gauni nzuri ulilopendelea kuvaa, weka mbele ya kabati au sehemu ambayo ni rahisi kuliona kila mara. Itakusaidia kufanya uhamasike zaidi kufikia lengo lako la kupungua uzito ili uweze kulivaa tena.
CREDIT: AFYA TRACK

Post a Comment

Previous Post Next Post