Mwanamke apewa dawa ya kusimamisha uume badala ya dawa ya kutibu macho

Woman having her eye treated by a doctorMwanamke mmoja nchini Uingereza amepata majeraha ya kemikali baada ya kupewa kwa makosa dawa ya kusimamisha uume badala ya dawa ya kutibu macho.
Mwanamke huyo kutoka Glasgow, Uskochi alipewa dawa ya kupaka ya Vitaros badala ya VitA-POS.
Daktari wake alimuandikia dawa sahihi ya kutibu matatizo ya macho ya VitA-POS, ambayo ipo katika mfumo wa kiminika kilaini.
Hata hivyo, kulitokea mkanganyiko wa kusoma maandishi ya daktari na mfamasia akatoa dawa ya Vitaros, ambayo pia ipo katika mfumo wa kiminika laini, lakini yenyewe huchochea kusimama kwa uume.
Baada ya kupaka dawa hiyo, alipata maumivu makali, jicho kuvimba hali iliyompelekea kushindwa kuona vizuri.
Majeraha hayo ya kemikali hata hivyo yaliweza kutibika, na jicho lake kusafishika baada ya siku chache.
Mkasa wa mwanamke huyo umeandikwa kwenye jarida la BMJ Case Reports. Jarida hilo limewataka madaktari kutumia herufi kubwa ili kuepuka makosa kama hayo kutokea.

Maandishi yalofanana

Daktari Magdalena Edington, ambaye ameandika ripoti hiyo amesema: "Makosa katika kutoa dawa ni jambo la kawaida. Dawa zenye vifungashio na majina yafananayo zinaongeza hatari za kutokea makosa hayo.
"Hata hivyo, ni jambo la kustaajabisha katika mkasa huu kuwa hakuna hata mtu mmoja, akiwemo mgonjwa mwenyewe, daktari na mfamasia ambaye alijiuliza iweje mgonjwa mwanamke apewe dawa ya matatizo ya kiume.
"Tunaamini kuwa mkasa huu ni muhimu sana kuuripoti ili kukuza uelewa wa kutoa dawa kwa njia salama."
Ijapokuwa dawa nyingi huandikwa kidijitali kupitia kompyuta badala ya kuandikwa mkono, tabibu huyo anataka kusukama uelewa kuwa dawa zenye maandishi ya majina yaliyofanana zipo na kuwataka watoaji "wahakikishe kuwa dawa ziandikwazo kwa mkono ziwe kwenye herufi kubwa ili kuepuka kosa kama hilo mbeleni".
Prescription showing how handwriting can be misreadHaki miliki ya pichaBMJ
Image captionCheti hiki kimeelekeza mgonjwa kupewa dawa ya kifua isordil, lakini mfamasia akadhani imeandikwa plendil ambayo ni dawa ya shinikizo la damu. Mgonjwa alifariki ndani ya wiki moja baada ya kunywa dawa hiyo ambayo haikuwa sahihi.
Takwimu zilizotolewa mwaka jana zinaonesha kuwa madaktari, mafamasia, hospitali na nyumba za malezi (ya wazee) zinafanya makosa milioni 237 katika kutoa dawa, ambayo ni sawa na kosa moja kwenye kila dawa tano zitolewazo.
Makosa hayo ni pamoja na kutoa dawa zisizo sahihi na kucheleweshwa kwa kutolewa kwa dawa.
Tafiti hiyo hata hivyo imebainisha kuwa mengi ya mapungufu hayo hayasababishi matatizo. Hata hivyo, robo tatu ya makosa hayo yanaweza kupelekea madhara.
Robbie Turner, mkurugenzi wa chama cha mafamasia cha Uingereza amesema chama hicho kinampa "pole" mwanamke huyo baada ya kuusikia mkasa wake.
"Makosa huchukuliwa kwa uzito mkubwa na mafamasia ambao hufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha afya za wagonjwa zinalindwa, kutokana na madhara ambayo wanajua yanaweza kutokea. Taarifa nyingi za kutoa dawa siku hizi zipo kidijitali na lengo hasa ni kupunguza makosa kutokana na maandishi ya mkono. Bila kujali tatizo katika kesi hii limetokea wapi, ushirikiano kati ya madaktari na mafamasia huboresha huduma na kuhakikisha usalama wa mgonjwa," amesema.
Katika mafunzo ya utoaji dawa nchini Uingereza, madaktari na mafamasia huoneshwa mfano mmoja ambapo mgonjwa alifariki baada ya kupewa dawa ya shinikizo la damu badala ya dawa ya kifua.
Mkasa huo ulitokea nchii Marekani ambapo cheti cha daktari kiliandika mgonjwa apewe isordil (isosorbide mononitrate) badala yake mfamasia alisoma kama imeandikwa plendil (felodipine). Matokeo yake mgonjwa alifariki ndani ya wiki moja.

Post a Comment

Previous Post Next Post