Sababu za WASTARA kutotaka kukatwa mguu kwa mara nyingine


Habari zenu wapenzi wasomaji wa blog yetu hii ya AFYA ZETU 360 leo nimeona tuangazie maisha ya mwanadada ambae ni msanii maarufu aliyekumbwa na matatizo katika mguu wake. JINA lake n WASTARA.
Kwa habari zilizo sasa dada yetu anapata maumivu makali katika mguu wake na sehemu za mgongo kutokana na mguu wa bandia anaotumia kuwa umipitwa na wakati. Na kikubwa zaidi ni kwamba mguu wake bado unamsumbua na unahitaji matibabu zaidi ambapo matibabu hayo anakuwa na machagulio mawili.
  • kukatwa mguu
  • kupata milioni 37 na kuepuka kukatwa mguu

kwanini hataki kukatwa mguu?

Wastara ni mpambanaji hakuna asiyejua kama kweli wewe unafuatilia maisha ya mwanadada huyu amekuwa mpambanaji kwa siku nyingi akijitahidi kujitafutia pesa yeye mwenyewe. Kukatwa mguu kwa mara ya pili kutasababisha Wastara apate shida kutumia tena mguu wa bandia kutembelea jambo litakalo mpelekea awe anatumia magongo. Kwa upambanaji wa mwanadada huyu hilo jambo litamuweka katika spidi ndogo ya mihangaiko na kumfanya uzalishaji wake upungue.

chaguo la pekee alilonalo

japokuwa pesa ndio kikwazo lakini chagulio la pekee kwa mwanadada huyu ni kwenda kupata matibabu ya sh mil 37 kuliko kukatwa mguu kwani hiyo itamsaidia mwanadada huyu kujizalishia bila kumtegemea mtu baada ya matibabu.

msaada

kwa mtu yoyote aliyeguswa na mahangaiko ya mwanadada huyu anaweza kumsaidia Wastara kwa chochote kitu maana akikosa hiyo pesa kitu cha pekee itakuwa ni kukatwa kwa mguu wake Wastara anahitaji msaada wako, yeyote anayeweza kumsaidia awasiliane naye kwa namba yake 0768666113.(chanzo cha namba NA PICHA ya wastara ni GLOBAL publishers)

Post a Comment

Previous Post Next Post