Chanjo ya ukimwi (Imeandikwa tena 2018)


Afrika Kusini
Image captionChanjo ya ugonjwa na virusi vya ukimwi

Chanjo mpya dhidi ya virusi vya ukimwi na ukimwi inatarajiwa kufanyiwa majaribio hii leo nchini Afrika Kusini.wanasayansi wanaeleza kwamba itakuwa kliniki kubwa na ya aina yake katika nchi ambayo ugonjwa wa ukimwi umeota miziz.
Taasisi ya kitaifa ya Afya nchini Marekani, ambayo inafadhili jaribio hilo, imeeleza kwamba zaidi ya watu elfu moja hupata maambukizi mapya kila siku nchini humo.
Utafiti huo umepewa jina HVTN 702 una lengo la kuwafikia zaidi ya watu 5000 wanaojishirikisha na ngono wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi na ukimwi kwa wanaume na wanawake nchini Afrika Kusini.
Idadi hiyo imeahidiwa kupata sindano tano kwa mwaka. Chanjo hiyo ilikwisha fanyiwa majaribio mwaka 2009 nchini Taniland na kuonekana inaouwezo wa kuzuia maambukizi kwa asilimia thelathini na moja katika kipindi cha miaka mitatu.
Wanasayansi bado wanalo tumaini kwamba kwa asilimia hamsini na zaidi chanjo hiyo inao uwezo wa kuonesha mafanikio nchini Afrika Kusini kwa watu wanaokadiriwa kufikia milioni saba ambao wanaishi na virusi vya ukimwi na ukimwi.
Matokeo ya utafiti wa chanjo hiyo yanatarajiwa kutolewa hadharani katika kipindi cha miaka minne ijayo.je unahisi ni vizuri kupatikana kwake
Njia za kujikinga na UKIMWI

Utepe mwekundu, ishara ya mapambano dhidi ya UKIMWI.
Onyesho la jumba la ghorofa mbili lililo na mabango kadhaa yanayohusiana na kuzuia UKIMWI
Matibabu ya UKIMWI, McLeod Ganj, Himachel Pradesh, India, 2010
Kuna njia nyingi za watu kupambana na janga hilo. Kuzuia maambukizi ya VVU, hasa kupitia kondomu na miradi ya kubadilishabadilisha sindano, ni mikakati mikuu inayotumika kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huu. Lakini wengine wanahoji kwamba bila kubadili tabia, teknolojia peke yake haitaweza kushinda ugonjwa huo.
KWA SASA.............

Chanjo

Njia bora ya kuzuia VVU ni wazo la kuwa na chanjo. Wanasayansi wengi wanatafuta chanjo ya VVU ili kuokoa uhai wa mamilioni ya watu, lakini kufikia mwaka 2012, hakuna chanjo mwafaka dhidi ya VVU/UKIMWI.[92]Jaribio moja la chanjo ya RV 144 iliyotolewa mwaka 2009 lilipelekea kupunguza hatari ya kuambukiza kwa takriban 30%, hivyo kuchochea matarajio ya jamii ya utafiti ya kutengeneza chanjo mwafaka zaidi.[93] Majaribio zaidi ya chanjo ya RV 144 yanaendelea.[94][95]

Kondomu
Vitendo vya kijinsia ni njia kuu ya kupata VVU. Kama watu wanatumia kondomu wanapofanya mapenzi, kuna nafasi ndogo zaidi ya kuambukizana VVU, lakini ukweli kamili ni kwamba hakuna ngono salama kwa hakika.

Matumizi ya kondomu ya kila mara hupunguza hatari ya kuambukizana UKIMWI kwa takriban 80% katika muda mrefu wa usoni.[96] Iwapo mwenzi mmoja ameambukizwa, kutumia kondomu kila mara hupelekea viwango vya chini ya 1% kwa mwaka vya huyo mwingine kuambukizwa.[97]

Kuna ushahidi mdogo unaoonyesha kuwa kondomu za wanawake una kiwango sawa cha kinga.[98]

Dawa za ukeni
Kutumia mafuta ya ukeni yanaliyo na tenofovir muda mfupi kabla ya ngono hukisiwa kupunguza viwango vya maambukizi kwa takriban 40% miongoni mwa wanawake wa Kiafrika.[99] Kinyume na hili, matumizi ya spemisidi nonoxynol-9 yanaweza kuongeza hatari ya kuambukizwa kwa sababu ya uwezo wake wa kuleta mwasho wa uke na rektamu.[100]

Tohara
Tohara katika eneo la Kusini kwa Sahara "hupunguza uambukizaji wa VVU katika wanaume wanaohusiana na wanawake kimapenzi kwa kati ya 38% na 66% kwa muda wa miezi 24". [101] Kwa msingi wa tafiti hizi, mashirika ya SAD na UNAIDS yalipendekeza tohara kama mbinu ya kuzuia uambukizaji VVU kutoka kwa mwanamke hadi mwanamume mwaka 2007.[102] Haijabainika wazi iwapo njia hii huzuia uambukizaji kutoka kwa mwanamume hadi mwanamke[103][104] na iwapo mbinu hii ina manufaa katika mataifa yaliyostawi na haijabainika miongoni mwa mashoga.[105][106][107] Baadhi ya wataalamu wanahofia kuwa dhana ya kiwango cha chini cha hatari miongoni mwa wanaume waliotahiriwa inaweza kupelekea mienendo hatari zaidi, hivyo wanapinga faida ya mbinu hii katika kukinga.[108] Wanawake waliofanyiwa ukeketaji wana hatari zaidi ya kuambukizwa.[109]

Post a Comment

Previous Post Next Post