Wasichana na wanawake milioni 200 katika mataifa 30 duniani tayari wameshakeketwa kwa mujibu wa shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia afya WHO
Ukeketaji ni neno ambalo huibua jazba na hisia tofauti kila mara linapotajwa. Watetezi wake huitetea mila na utamaduni huo kwa jino na ukucha huku wanaopinga wakipinga kwa kila silaha walio nayo.
Lakini vita dhidi ya ukeketaji vinapozidi kuchacha wasichana na wanawake milioni 200 katika mataifa 30 duniani tayari wameshakeketwa kwa mujibu wa shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia afya WHO.
Makala ya BBC Funguka yamezamia suala hili yakitaka kubaini majibu ya maswali kadhaa kwa kuzungumza na waathiriwa na wanaharakati.
Mariam ni mama aliyekeketwa akaolewa kisha akaachana na mumewe baada ya kupata ujauzito. Alikeketwa akiwa na miaka minane pamoja na dada zake baada ya wazazi wake kufanya uamuzi huo.
Jamii ya Maasai ni baadhi ya zile ambazo bado zinaendesha tamaduni ya ukeketaji wasichanaHaki miliki ya picha Getty Images
Image caption
Jamii ya Maasai ni baadhi ya zile ambazo bado zinaendesha tamaduni ya ukeketaji wasichana
"Nilikuwa na miaka minane, dadangu miaka 10 na mdogo wetu alikuwa na miaka mitano. Ikabidi basi tulizike tungefanya nini?" anasema Mariam.
Alipofikisha umri wa miaka 18, Mariam aliingia kwenye ndoa. Baadaye akapata ujauzito. Baada ya miezi mitatu mumewe akamfukuza. Anakiri kuwa alipata matatizo mengi wakati wa kujifungua kwa kuwa alikuwa amekeketwa. Alipelekwa kwenye hospitali ya wilaya kujifungua kwa usafiri wa trekta.
"Niliumwa siku moja nikapata uchungu wa kuzaa kuanzia saa kumi alfajiri, hadi saa mbili za usiku. Kwa sababu mtoto hakuweza kutoka. Mtoto alitoka amekufa."
Machozi yanamdondoka Mariam, huku amevaa uso wa huzuni anapofunguka. "unapojifungua, jamii nzima hushangilia na ikiwa huna mtoto na watu wanaongea kukuhusu inahuzunisha." Anasema.
Changamoto za maisha za wananawake kunzia wanapokeketwa hadi wanapokuwa watu wazima
Image caption
Changamoto za maisha za wananawake kunzia wanapokeketwa hadi wanapokuwa watu wazima
Maisha yake yalikuwa magumu sana baada ya kumpoteza yule mtoto."yule mtoto aliharibu kila kitu mwilini mwangu, nyonga zikaharibika, nikapata fistula...Kwa miaka mitano alitaabika. Hatimaye alifanyiwa operesheni na akaolewa tena. Hata hivyo mumewe hana habari kuhusu kadhia yake siri aliyoificha kwa miaka mitatu.
"Nilipata fistula iliyosababishwa na kukutewa maana njia ilikuwa finyu. Singeweza kutembea kwa miaka mitano. Nilikuwa nimekataa tamaa, nikahisi nimetengwa."
Mumewe anamsikiza kwa makini na kumpa ubavu wa kumfariji. Mumewe anamuahidi kuwa atazidi kumpenda kwa hali na mali hadi kifo kitakapowatenganisha. Maria anahisi kuondokewa na mzigo mzito baada ya kumfungukia mumewe ishara tosha ni tabasamu ambalo anamvalia mumewe ambaye anaridhia hali yake.
Hali yake Maria ni moja ya sababu kubwa ya watoto kuzaliwa wakiwa wamekufa nchini Tanzania. Nchini Tanzania asilimia 15 ya wanawake wameshakeketwa huku wengi wakiathiriwa kwenye sehemu za siri.
Changamoto za maisha za wananawake kunzia wanapokeketwa hadi wanapokuwa watu wazima
Image caption
Changamoto za maisha za wananawake kunzia wanapokeketwa hadi wanapokuwa watu wazima
Mwanaharakati dhidi ya ukeketaji, Sadia Hussein kutoka jimbo la TANA River nchini Kenya, alikeketwa akiwa na umri wa miaka 10. Anakiri kuwa ni changamoto kubwa katika jamii za wafugaji.
"Kina mama wengi huumia sana kwa siri na mara nyingi wanaume hawana ufahamu wanachopitia wanawake. Kule kwetu utakuta mwanaume anarudi jioni baada ya kuchunga ng'ombe au mbuzi anaambiwa mama amejifungua wala hajui matatizo ambayo mkewe aliyapitia hadi akajifungua." Anasema Sadia.
Anasema alipokeketwa hakujua madhara yake, hadi alipokuwa mtu mzima. Shuleni wasichana wenzake walikuwa wanamtenga wakisema kuwa yeye ni mchafu kwa kuwa hakuwa amekeketwa. Nyanyake ndiye alimkeketa. Alifurahia sana alipoambiwa kuwa angekeketwa kwani wasichana wenzake hawangemtenga tena.
"Nilipelekwa msituni. Ilikuwa asubuhi. Niliambiwa hufai kupiga kelele, utaonekana kuwa mwoga. Ukinyamaza wavulana wataona wewe ni shujaa. Nilifikiri kijembe kinapita mara moja, inaisha. Kumbe wanatoa nyama. Unasikia sauti ya kijembe. Wameweka vitambaa kwa kinywa huwezi kupiga kelele."
Mambo mengi yalikuwa yanapita mawazoni mwake wakati huo. Uchungu aliokuwa akipitia ulimfanya kujiuliza maswali iwapo mamake alikuwa amefanya kosa. Hatimaye mganga alikamilisha kazi yake bila ya kuwekewa dawa.
"Hakuna dawa yoyote ya kuzuia maumivu, wanaweka kinyesi cha punda, makaa moto, wanachimba shimo hiyo ndio dawa yako, unakalia yale makaa moto. Tayari umeshonwa, miguu imefungwa kuanzia kwenye nyayo hadi kwenye nyonga. " anaongeza Sadia
Changamoto za maisha za wananawake kunzia wanapokeketwa hadi wanapokuwa watu wazima
Image caption
Changamoto za maisha za wananawake kunzia wanapokeketwa hadi wanapokuwa watu wazima
Viwango vya ukeketaji ni tofauti, wanaokeketa wanataja kuwepo kwa ukeketaji mdogo hadi kwa ule ambao sehemu yote ya siri hukatwa na inayosalia kushonwa, huku nafasi ndogo ikiachwa kwa ajili ya hedhi na kupitisha mkojo. Saida aliyevumilia hali ile kwa mwezi mmoja, anasema kuwa ukeketaji una madhara mengi kwani mtu hutokwa na damu nyingi, 'unahisi maumivu mengi joto na kichwa kinakuuma."
Baadaye alipoolewa alipata ujauzito. Wakati alipokuwa anajifungua alihisi maumivu kwa siku tatu. Uchungu wa mwana aujauaye ni mzazi, mamake aliyekuwa karibu naye alimwambia, huku akilia, "hata mtoto akizaliwa plastiki au chura, mradi atoke tu."
Kwa kudura za Mungu, Sadia alijifungua mtoto wa kike. Kadhia aliyopitia ilibadilisha mtazamo wake kuhusu ukeketaji, "kila siku nikiamka, nilikuwa namtazama mtoto wangu kisha naangalia kidonda changu, kisha nasema sitakubali mtoto wangu ayapitie machungu ambayo niliyapitia."
◾Msimu mpya wa Wanawake 100 wa BBC
Machozi yanamdondoka Saidia kila anapojaribu kuelezea kadhia yake huku akivuta zile kumbukizi. Baada ya kuuguza maumivu akapata afueni, alianza kutembelea majirani huku akiwashauri wasiwakekete mabinti zao. Hata hivyo alikutana na upinzani mkubwa, "niliambiwa kuwa hii ni dini yetu, mbona mamako na nyanyako walipitia?"
Sadia anakiri kuwa changamnoto kubwa ilikuwa kusimama mbele ya wanaume kujaribu kuwashauri waache tabia ya kuwakeketa wasichana. Hata hivyo mkuu wa wilaya alipoambiwa kuhusu safari yake mpya, badala ya kuadhibiwa serikali ilimuunga mkono.
Changamoto za maisha za wananawake kunzia wanapokeketwa hadi wanapokuwa watu wazima
Image caption
Changamoto za maisha za wananawake kunzia wanapokeketwa hadi wanapokuwa watu wazima
Wasichana na kina mama wengi wakajitokeza kuelezea changamoto zao. "Kwanza mimi nilipokeketwa nilishindwa kukujoa kwa siku tatu ilibidi nyanyangu aje kunifungua." Anasema Sadia, "Mtazamo wa watu kuhusu ukeketaji unaendelea kubadilika." Saidia ameunda kikundi cha kina mama 20 ambao wamepitia ukeketaji na sasa wanahamasisha jamii katika jimbo la Tana River kuhusu madhara yake.
Ripoti ya Shirika la Afya Duniani -WHO, inaonyesha kuwa aslimia 98 ya wanawake na wasichana wamekeketwa nchini Somalia. Taifa hili la upembe wa Afrika bila shaka linaongoza kwenye orodha ya mataifa ya Afrika.
Jamila Mwanjisi ni afisa mawasilinao katika shirika la Save the Children nchini Somalia, anasema, "ukeketaji ni unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto." Licha ya kuwa na madhara makubwa mila hii ingali inafanyika katika jamii nyingi. Anasema, "ni kwa sababu jamii haina ufahamu wa madhara ya ukeketaji."
Changamoto za maisha za wananawake kunzia wanapokeketwa hadi wanapokuwa watu wazimaHaki miliki ya picha Getty Images
Image caption
Changamoto za maisha za wananawake kunzia wanapokeketwa hadi wanapokuwa watu wazima
Baadhi ya madahara ya ukeketaji ni pamoja na maumivu wakati wa hedhi, kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi na hata wakati mwingine kupotez maisha. Hata hivyo Jamilla ni mwepesi wa kusema kuwa kuna madhara mengine, "wanawake wengi wanakosa hisia za mapenzi. Anapopata fistula anakuwa ananukaa, hivyo anaogopa kutangamana na wenzake. Pia ndoa nyingi zinavunjika pamoja na maumivu."
Fistula ni hali ya kushindwa kuzuia mkojo ama haja kubwa baada mama mjamzito anapokuwa na maumivu ya muda mrefu akijifungua.
Ili kukabiliana na mila na utamaduni huu ambao umekolea katika baadhi ya mataifa, Jamilla anashauri wavulana na wanaume wahusishwe kwa ukamilifu. Anaogeza kusema, "sheria pekee hazitoshi lakini ni muhimu kuwa na mifumo inayosaidia katika utekelezaji wake".
Tags:
MAGONJWA YA WANAWAKE