busha ni nini?
huu ni uvimbe kwenye korodani ambao unasababishwa na kujaa kwa maji kwenye moja ya sehemu zinazounda korodani kitaalamu kama tunica vaginalis..busha hutokea pale maji yanayotengenezwa kwenye korodani kua mengi sana kuliko yale yanayo ondolewa.
busha huweza kutokea kwa watoto wadogo wakati wa kuzaliwa lakini mara nyingi hupotea baada ya muda mfupi tu, kama ukiona halipotei kwa mtoto wako ni vizuri kuonana na daktari.
chanzo cha busha ni nini?
kuna aina kuu nne za vyanzo vya busha kama ifuatavyo.
idiopathic; hii ni busha inayotokea tu bila hata kujua chanzo ni nini.
kuumia; busha huweza kutokea sababu ya kuumia kwa kupigwa na kitu kwenye korodani au kuanguka na kuumiza sehemu hizo.
uvimbe; uvimbe kama wa kansa huweza kusababisha busha.
magonjwa; ugonjwa unao ambukizwa na mbu kitaalamu kama filariasisis huleta busha na aina hii ya mbu hupatikana mwambao wa bahari na ndio maana wagonjwa ni wengi sana huko.
dalili za busha..
ugonjwa huu huanza kwa kuvimba taratibu kwa korodani na baadae kua kubwa sana, hakuna maumivu yeyote ambayo mgonjwa anayapata isipokua uvimbe ukiwa mkubwa sana mgonjwa huathirika kisaikolojia kwa kutengwa au kuchekwa na jamii.
vipimo;
ugonjwa huu unaweza kutambulika kwa kuangaliwa tu na daktari mzoefu lakini pia anaweza kupiga picha kuhakikisha sio ugonjwa mwingine unaosababisha kuvimba kwa korodani.
matibabu;
hapa ndio waganga wengi wa kienyeji wanapodanganya watu,...ugonjwa huu ukiupata lazima upasuliwe kuondoa hayo maji na kuzuia chanzo cha tatizo na hakuna dawa yeyote ya kupaka, kunywa au kuchanja ambayo inaweza kutibu hili tatizo.
siri za afya