hebu tuangazie kwanini baadhi ya nchi zimehalalisha bangi mfano Canada ni nchi ya pili baada ya Uruguay kuhalilisha matumizi ya bangi kwa starehe
Kuhalilishwa kwa bangi kunatimiza ahadi aliyotoa waziri mkuu Justin Trudeau, katika kampeni ya uchaguzi mnamo mwaka 2015.
Kiongozi huyo wa chama tawala cha ki Liberali ameeleza kwamba sheria za jadi za nchi hiyo dhidi ya matumizi ya bangi hazifanyi kazi, ukizingatia kwamba raia nchini humo ni miongoni mwa wanaotumiwa kwa kiasi kikubwa bangi duniani.
Ameeleza kuwa sheria hiyo mpya imeundwa kuwaondolewa watoto bangi karibu, na kuondosha faida wanayoipata wahalifu.
Serikali ya shirikisho inakadiria pia itapata $ milioni 400 kwa mwaka katika tozo la kodi katika mauzo ya bangi.
Zimbabwe nayo kuhalalisha upanzi na matumizi ya bangi, Serikali ilisema watu nchini Zimbabwe sasa wanaweza kutuma maombi ya kukuza bangi.
Hadi sasa, imekuwa ni haramu kupanda, kumiliki au kutumia bangi nchini Zimbabwe ambapo yeyote ambaye atakutwa na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 12 jela
HIZO NI BAADHI TU YA NCHI, HEBU TUANGALIE BANGI INA NINI KIMATIBABU
Cannabinoids ndizo kemikali zinazofanya zao hili kuwa na mwamko katika nchi mbali mbali ambazo zimeangazia bangi kama dawa mfano ni nchi ya Lesotho ambayoWakulima wanavyogeukia kilimo cha bangi kutokana na faida zake.Serikali ya Lesotho tayari imetoa leseni kwa kampuni kadhaa za kimatiafa kukuuza na kuuza bidhaa za bangi.
Nchi hiyo imefanikiwa kuwavutia wawekezaji kutoka Canada, ambao wamepata mazingira bora na gharama ya chini ya kufanya biashara zao.
Mwaka huu pekee kampuni ya bangi kutoka Toronto iliwekeza dola milioni 10 huko Medigrow Lesotho ikiwa ni asilimia 10 ya hisa kwenye kampuni hiyo.
Kemikali muhimu zaidi kwenye zao la bangi ni mbili ikiwemo delta-9-tetrahydrocannabinol (THC), ambazo zinadaiwa hata miili yetu hujitengenezea kemikali za namna hiyo kujiwezesha na jukumu la kusimamia radha, kumbukumbu, kufikiri, mkusanyiko, harakati za mwili, ufahamu wa wakati, hamu, maumivu, na hisia (ladha, kugusa, harufu, kusikia, na kuona).
JE BANGI IRUHUSIWE NCHINI KWAKO? ANDIKA MAONI YAKO
Tags:
MIMEA