Cameron Underwood anasema watu waliokuwa wanamtazama usoni na kupigwa na butwaa wamepungua, tangu alipofanyiwa upasuaji na kupandikizwa uso.
"Niko na pua na mdomo kwa hivyo ninaweza kutabasamu, kuongea na kula chakula kigumu tena," anasema.
Cameron alikuwa azingumza miaka miwili baada ya kujipiga risasi alipojaribu kujiua mwaka 2016.
Alipoteza pua yake, sehemu kubwa ya chini ya mdomo na meno yake yote isipokuwa moja tu katika kisa hicho.
"Ninashukuru sana kwa upasuaji huu wa kupandikizwa uso kwa sababu imenipa fursa ya pili ya maisha," mwanamume huyo mwenye miaka 26 alisema kwneye mkutano wa waandishi wa habari huko New York Marekani siku ya Alhamisi.
"Nimefanikiwa kurejea shughuli nyingi ninazozipenda kama kukaa nje, kushiriki michezo na kutumia muda na marafiki na familia yangu.
Nina matumaini ya kurudi kazini karibuni na wakati mmoja kuwa na familia.
Januari mwaka huu, zaidi ya madaktari na wahudumu wengine wa afya 100 walichukua muda wa saa 25 kumfanyia upasuaji Cameron kwenyr kituo cha afya cha NYU Langone huko Manhattan, New York na taarifa za kupona kwake zilifichuliwa wiki hii.
Upasuaji huo ulifanyika miaka 18 bada ya jaribio la Cameron kutaka kujiua-ambao kituo hicho kinasema ndio muda mfupi zaidi kati ya jeraha na upasuaji katika hostoria ya Marekani.
Tangu upasuaji wa kwanza wa kupandikizwa uso mwaka 2005, zaidi ya upasuaji mwingine 40 umefanyika kote duniani.
Upasuaji huo uliongozwa na Dr Eduardo D. Rodriguez ambaye anasema kando na hatua kubwa za matibabu, ni moyo wa kutaka kuishi aliokuwa nao Cameron ulifanikisha upasuaji huo.
Upasuaji wa Cameron ndio wa tatu kufanywa na Dr Rodrigues na anasema kuwa muda mfupi ambao Cameron alikuwa ameishi na majeraha pia ilikuwa sababu kuu ya kupona kwake.
"Cameron hajaishi na majeraha yake kwa muongo mmoja au zaidi kama vile watu wengine," alisema.
Kutokana na hilo hukuweza kukumbwa na matatizo mengine ya kisaikolojia jambo ambalo husababisha madhara kama msongo wa mawazo, matumizi ya madawa ya kelevya na tabia zingine zenye madhara.
Wakati wa upasuaji, daktari alijenga upya sehemu za chini za mdomo na pua na kurejesha meno yote 32.
'Mtoto wangu anamsaidia Cameron kuishi maisha mazuri'
Aliyechangia viungo hivyo alikuwa mwanamume wa miaka 23 Will Fisher.
"Kifo cha mtoto wangu kilikuwa janga," anasema mama yake Will, sally.
"Ninashukuru kwa sababu ya kuheshimu uamuzi wake tuliwez kuwapa wengine maisha, hasa wakati huu Will na Dr Rodriguez wamempa Cameron na familia yake fursa kutimzia ndoto zao.
"Kuwa sehemu ya suala hili imenipa nguvu nyakati ngumu katika maisha yangu.
Cameron alimshukuru Will na msaada wa familia ya Fisher wakati wa hotuba kwenye mkutano wa waandishi wa habari katika hospitalini.
"Ninataka Sally na familia yake kujua ni kwa kiwango gani familia yangu inashukuru kwa zawadi hii na kamwe nitamshukuru Will, anasema.
"Kumekuwa na hatua nyingi kubwa zaidi za upasuaji na mimi ni mfano wa hizo. Lakini hii inafanyika tu kwa sababu watu speshemi kama Will na familia yake."