kwanini UKIMWI hauambukizwi kwa mate?

 Image result for hiv in saliva
Suala la maambukizi ya virusi vya HIV vinavyosababisa ugonjwa wa Ukimwi bado linaendelea kuwakosesha usingizi wataalamu wa afya kote duniani.
Kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani (WHO) ugonjwa huo umewaangamiza zaidi ya watu milioni 35 kufikia sasa.
Mwaka jana pekee, karibu watu milioni moja walifariki kutokana na magonjwa yanayohusishwa na virusi vya HIV.
Kuna karibu watu milioni 37 ambao wanaishi na virusi hivyo - 70% kati yao wanapatikana barani Afrika - huku watu milioni 1.8 wakiambukizwa umpya mwaka 2017.
Tangu ugonjwa wa Ukimwi ulipogunduliwa miaka ya 1980, kumekuwa na gumzo kuhusiana na jinsi virusi vyake vinavyoweza kusambazwa.
Je maisha ya waathiriwa wa ugonjwa huo katika jamii yamekuaje?
Leo Ulimwengu unapoadhimisha siku ya Ukimwi Duniani, tunaangazia baadhi ya dhana potofu zinazosababisha kunyanyapaliwa kwa waathiriwa.
Dhana: Naweza kuambukizwa virusi vya HIV kwa kutangamana na watu waliyoathirika
 
Uchunguzi wa damu ni muhimu ili kubaini kama una virusi vya HIV
Dhana hizi zimesababisha unyanyapaa dhidi ya waathiriwa wa ugonjwa wa UKIMWI kwa muda mrefu.
Licha ya kuendeshwa kwa kampeini ya mwaka 2016 ya kuhamasisha watu nchini Uingereza kuhusiana na suala hilo 20% ya watu nchini humo wanaamini HIV inaweza kusambazwa kupitia mate au kumgusa mtu aliyeambukizwa virusi hivyo.
Huwezi kuambukizwa virusi vya HIV kupitia:
  • Kwa kuvuta hewa moja
  • Kukumbatiana, kubusiana, au kusalimiana
  • Kutumia pamoja vyombo vya kula chakula
  • Kutumia maji pamoja
  • Kutumia pamoja vitu vya kibinasi
  • Kutumia pamoja vifaa vya mazoezi
  • Kugusa kiti cha msalani, komeo la mlango na kadhalika
Haki miliki ya picha Ronald Grant
Image caption Mwaka 1991, Princess Diana wa Wales alikutana na waathiriwa wa Ukimwi mjini London katika juhudi za kukabiliana na dhana kuhusu njia za maambukizi ya virusi vya HIV
Virusi vya HIV huambukizwa kupitia damu, kunyonyesha au kufanya ngono bila kinga na mtu aliye na virusi hivyo.
Dhana: Dawa za kienyeji zinaweza kuzuia maambukizi ya HIV
Huu si ukweli hata kidogo . Dawa za kienyeji, kuoga baada ya kufanya tendo la ndoa au kufanya ngono ya mdomo haina athari yoyote dhidi ya HIV.
Utamaduni wa utakaso ambao ulipata umaarufu katika mataifa ya jangwa la sahara , na maeneo ya India na Thailand, umetajwa kuwa hatari sana.
Umesababisha wasichana kubakwa na watoto wadogo kunajisiwa hali ambayo inawaeka katika hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV.
Chimbuko la utamaduni huo linaaminiwa kuwa barani Ulaya katika karne ya 16 ambapo watu walianza kuambukizwa magonjwa ya zinaa kama vile kisonono na kaswende.
Utamaduni huo hata vyo haukuwahi kutibu magonjwa hayo pia.
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption HIV haiambukizwi kwa kumgusa mtu aliyeathiriwa au kwa kuumwa na mbu
Dhana: Mbu wanaweza kusambaza virusi vya HIV
Japo maambukizi hupitia damu, tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa mtu hawezi kupata maambukizi kutoka kwa wadudu wanaofyonza damu kwa sababu hizi mbili.
1) Mbu hamuongezei mtu damu mwilini kabla ya kumuuma mtu.
2) Virusi vya HIV huishi ndani yao kwa kwa muda mchache.
Kwa hivyo hata mtu akiishi katika eneo lililo na mbu wengi, maambukizi ya HIV hayahusiani kwa vyovyote na mbu hao.
Dhana: Siwezi kupata virusi vya HIVkwa kufanya ngono ya mdomo
Ni kweli ngono ya mdomo huenda si hatari sana ikilinganishwa na aina nyingine ya ngono.
Viwango vya maambukizi ni chini ya nne katika visa 10,000.
Lakini mtu anaweza kupata maambukizi ya virusi vya kufanya ngono ya mdomo na mwanamume au mwanamke aliye na virusi hivyo.
Ndio maana madaktari wanapendekeza matumizi ya mpiria wa kondomu wakati wa kufanya gono ya mdomo.
Dhana: siwezi kuambukizwa virusi vya HIV nikivaa mpira wa kondomu
Mipira ya Kondomu inaweza kupasuka, kutoka au kuvuja wakati wa tendo la ndoa hali ambayo huenda ikawaeka katika hatari ya maambukizi ya virusi wapenzi wote wawili
Hii ndio maana kufanikiwa kwa kampeini dhidi ya UKIMWI hakukomei katika muktadha wa kuwaambia watu kutumia kinga pekee, bali bia kuna haja ya wale waliyeambukizwa virusi vya HIV kupata matibabu.
Kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani WHO, mmoja kati ya kila watu wanne ana virusi vya HIV na mtu huyo hana habari - hii inamaanisha watu milioni 9.4 - wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa huo hatari.
Dhana: Kama huna dalili huna virusi vya
Mtu anaweza kuwa na virusi vya ukimwi na asiwe na habari.
Hata hivyo huenda akapatikana na magonjwa kama vile homa inayofanana na influenza-ikiwa ni pamoja na kuumwa na kichwa,kushikwa na homa, harara mwilini au kuumwa na koo katika wiki chache za kwanza baada ya kuambukizwa viini vinavyosababisha ugonjwa wa UKIMWI.

Dalili zingine kama vile kupungua uzani, kuharisha na kukohoa hujitokeza kadiri kinga ya mwili inavyoendelea kupungua.
Muathiriwa asipopata matibabu huenda akapatikana na magonjwa kama vile kifua kikuu, homa ya utandu wa ubongo miongoni mwa zingine
Dhana: Mtu aliyepatikana na virusi vya HIV atafariki akiwa na umri mdogo
Watu wanaojua hali yao ya HIV na kuzingatia matibabu na lishe bora huishi kwa muda mrefu.
Shirika la UNAids linasema 47% ya watu wote wanaoishi na virusi vya HIV huwa wamedhibiti kiwango cha virusi hivyo mwilini kwa kutumia dawa.
Hii inamaanisha watu hao hawawezi kusambaza virusi hivyo hata wakijamiana na mtu ambaye hana virusi hivyo.
Hata hivyo wakisitisha matibabu viwango vya virusi vinaongezeka na vinaweza kuonekana katika damu yake.
Kwa mujibu wa WHO, watu milioni 21.7 waliyo na virusi vya HIV wamekuwa wakitumia dawa za kukabiliana na virusi hivyo mwaka 2017.
Idadi hiyo imeongezeka kutoka watu milioni 8 mwaka 2010 - hii inamaanisha 78% ya watu waliyo na virusi vya HIV wanajua hali yao.
Dhana: Kunamama waliyoathirika watawaambukiza watoto wao
Suala hilo lina mjadala lakini uwezekano wa akina mama ambao wamedhibiti kabisa kiwango cha virusi vya HIV katika miili yao wanaweza kuwanyonyesha watoto wao bila kuwaambukiza virusi hivyo

Post a Comment

Previous Post Next Post