Dysmenorrhea Ni Kitu Gani?
Dysmenorrhea ni jina la kitabibu kwa maumivu kipindi cha hedhi, ambayo hutokana na kusinyaa kwa misuli ya mji wa mimba wakati wa kipindi cha hedhi ili kuruhusu kumeguka kwa ukuta wa mfuko wa mimba na kutoa damu iliyochanganyika na yai ambalo halikurutubishwa nje.mumivu haya yamegawanyika katika aina mbili
Maumivu Ya Hedhi Aina Ya Kwanza Ya Kawaida (Primary Dysmenorrhea)
Maumivu haya ni ya kawaida kabisa kwa wanawake wanapopitia kipindi hikia ambacho hujirudia kila mwezi. Maumivu kikawaida huanza kati ya siku moja ama mbili kabla ya hedhi kuanza kutoka, mwanamke hujiskia mamumivu haya kwenye tumbo la chini, kwenye nyonga na kiuno kwa ujumla. Maumivu haya yanaweza kuwa madogo au yakawa makali sana na huisha ndani ya masaa 12 mpaka 72 huku yanaweza kuambatana na kutapika na kupata kizunguzungu. Kwa wanawake wengi maumivu haya ambayo ni ya kawaida kabisa hupungua kadiri umri unavoenda na pia pale mwanamke akijifungua.
Maumivu Aina Ya Pili Yasiyo Ya Kawaida (Secondary Dysmenorrhea)
Maumivu haya ni kutokana na tatizo fulani la kiafya kweye via vya uzazi vya mwanamke kama vile uvimbe ambayo siyo wa saratani ndani ya mfuko wa mimba (uterine fibroids), kukua kwa tishu laini za mfuko wa mimba kuelekea kwenye viungo vingine kama uke na mifuko ya mayai (endometriosis) na pia kupanuka kwa ukuta wa uterus kutokana na kukua kwa tishu za ndani za uterus kuelekea ukuta wa nje (adenomyosis). Maumivu haya pia yasiyo ya kawaida yanweza kuwa yamesababishwa kwa athari za bacteria ama virusi katika via vya uzazi. Kikawaida maumivu haya huanza mapema Zaidi wakati wa hedhi ya huchukua muda mrefu Zaidi kuisha ukilinganisha na maumivu yake ya kawaida (primary dysmenorrhea), na pia maumivu haya yanakuwa hayaambatani na kutapika, kuharisha, kizunguzungu wala kukosa nguvu na ganzi.
Maumivu Kipindi Cha Hedhi Kwa Kiasi Kikubwa Hulenga Katika Viungo Hivi
- Via vya uzazi, kama maumivu yako ni kutokana na kukua Zaidi kwa tishu za uterus basi maumivu husambaa hadi kwenye tumbo la uzazi.
- Tumbo la chini—huathirika pia na maumivu haya kwa kiasi kikubwa, kama maumivu haya ni kutokana na kukua kwa tishu za uterus basi mwanamke anahisi kama ameunguzwa na kitu cha moto kwenye tumbo.
- Maumivu ya chini ya mgongo- mara nyingi hutokana na kukua kwa tishu za uterus kuelekea kwenye uke na pia kwenye mifuko ya mayai.
- Miguu- maumivu yanaweza pia kutekea kwenye hips yakishuka chini ya miguu na kufanya mwanamke kushindwa kutembea .
- Maumivu ya kisaikologia hutokea pia kwa kiwango kukubwa kwa wanawake ambao maumivu yao ya hedhi ni kutokanana kukua tishu za uterus bila mpangilio, wanawake hawa huapata msongo wa mawazo kutokana na kufikiri kwamba
- Pengine tatizo la uvimbe haliwezi kupona na hakuna dawa
- Ama hawataweza kupata mtoto kwa siku za baadae
- Mahusiano ya Rafiki ama wapenzi wao yatavunjika kama wakijua ana tatizo la uvimbe
- Ama kufikiri jinsi ambavyo ahawatafanya kazi zao kwa ufasaha na kutofurahia maisha kama mwanzo walipokuwa wazima.
Nini Chanzo Cha Maumivu Kipindi Cha Hedhi?
Maumivu haya hutokana na kitendo cha misuli ya uterasi kukaza na kusinyaa kupitia, kitendo hichi huratibiwa na homoni ya prostaglandins. Ni kawaida kwa uterus ambao ni mfuko unaobeba mimba kusinyaa kipindi chote cha mzunguko wa hedhi ambacho huchukua siku 28. Lakini utofauti ni kwamba wakati wa kutoa hedhi yenyewe mfuko huu husinyaa na kujikaza Zaidi na hivo kukatisha hewa safi ya oyygeni kufika kwenye misuli ya mfuko huu wa mimba. Maumivu ni matokeo ya kukosekana kwa muda kwa hewa ya oxygen kwenye baadhi ya misuli ya uterus.
Nini Cha Kufanya Pale Unapopata Maumivu Kipindi Cha Hedhi
Kuna njia nyingi ambazo husaidia kupunguza maumivu ya hedhi ambazo unaweza kutumia ukiwa nyumbani kwako pasipo kwenda hospitali. Kama mauvimu ni makali sana unaweza
- Kumeza dawa za kukata maumivu kama asprini na ibuprofen kwa ahueni ya haraka. Angalizo: dawa za maumivu isiwe ni nia ya kutumika kila mara kwani madhara yake ni makubwa kiafya, dawa hizi zitumike kwa uangalifu.
- Tumia maji ya uvuguvugu kukandakanda mahali pa tumbo la chini ukiwa umelala chali
- Usitumie vinywaji na vyakula vyenye caffeine mfano majani ya chai na kahawa
- Fanya masaji kwenye upande wa chini wa mgongo na sehemu ya tumbo la chini.
- Pata muda mwingi wa kupumzika
- Weka ratiba ya kufanya mazoezi mara kwa mara, tafiti zinasema wanawake wanaofanya mazoezi hupunguza maumivu ya hedhi kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na wasiofanya mazoezi.
Ni Kipindi Gani Unatakiwa Kumuona Dactari Ili Kupata Matibabu Na Ushauri Zaidi.
Kama maumivu yako ni makali Zaidi kuliko kawaida na yanachukua Zaidi ya siku 3 hakikisha unamwona dactari wako haraka, kwanini?, kwasababu yawezekana maumivu yako siyo ya kawaida na yaweza kuwa una uvimbe ama maambukizi ya bacteria na virusi kwenye mfuko wa mimba, hivo kuwahi hospitali itasaidia kutibu tatizo lako mapema kabla halijawa kubwa. Pia tunashauri kuwahi kumwona dactari kwa sababu ukkuaji wa tishu za mfuko wa mimba unahusishwa na kusababisha saratani ya shingo ya kizazi, na hivo kujua chanzo cha tatizo lako mapema kutasaidia kulitibu mapema.