Utafiti mpya wa kiafya umebaini kuwa watu warefu zaidi wapo katika hatari ya kuwa na ugonjwa wa Saratani.
Mwandishi wa ripoti ya utafiti huu Dr Leonard Nunney anasema watu walio katika mazingira ya kupata ugonjwa wa saratani iwapo tu atakuwa na ongezeko la urefu wa kawaida kwa kuanzia sentimita kumi,basi hapo ni jambo la kujiuliza mara mbili.
"Iwapo wastani wa wanawake 50 kati ya 500 watapata saratani, wastani huo unabadilika ifikapo kwa wanawake 60 kwa 500 warefu kufikia kimo cha sentimita 178 ambao kwa mjibu wa utafiti huo, wanakuwa katika uwezekano mkubwa wa kupata Saratani''.imebainisha ripoti hiyo.
Ripoti ya utafiti huu mpya inakuja huku suala la uvutaji sigara likiendelea kutajwa kuwa chanzo kikubwa cha kupata ugonjwa wa Saratani,sasa kama kimo nacho ni sababu kubwa ya kupata ugonjwa huo wastani unabadilika kutoka uwezekano kwamba watu 50 wana saratani kati ya kila watu 500 na kufikia wastani wa kila watu 300 kuwa na saratani kati ya watu 500.
Takwimu za utafiti huu ziliwahusisha wanawake wapatao milioni moja kuangalia aina 23 za vimelea vya saratani katika nchi za Uingereza,Marekani, Korea Kusini, Australia, Norway na Sweden.
Kila kundi lililochaguliwa kufanyiwa utafiti lilipaswa kuwa na matukio 10,000 ya ugonjwa wa Saratani kwa kila jinsia.
Jumla ya aina 18 za Saratani zilifanyiwa uchunguzi kwa jinsia zote yaani wanaume kwa wanawake,ambapo ilibainika aina hizo za saratani hazina uhusiano na kimo kisicho cha kawaida cha kimo.
Ripoti ya utafiti huo ya Royal Society,inasema kuwa ngezeko la sentimita 10 kutoka urefu wa kawaida wa kati ya futi 5 hadi 7 kwa wanaume na ule wa futi 5 kwa wanawake unasabaisha kuwa na asilimia 10 ya uwezekano wa kupata Sratani.
Utafiti huu umezua mjadala wa watalaam wengine
Tafiti zilizotangulia pia zimewahi kutoa suluhisho kama hilo katika suala la uhusiano wa urefu na uwezekano mkubwa wa kuwa na saratani hali ambayo ina zaa swali kwamba je ni watu warefu tu?
Je kuhusu makundi mengine na tahadhari kuhusiana na saratani.
Wataalam wengine wanamashaka na matokea ya utafiti huu na kudai kuwa kiwango cha sababu za urefu ni kidogo mno ikilinganishwa na sababu nyingine za ugonjwa huu kama vile uvutaji sigara.
Utetezi wa watafiti hawa wanaotaja kigezo cha urefu,wao wanashikilia msimamo wao wa kisayansi ni kwamba watu warefu wa seli nyingi mwilini hali ambayo inachangia kupata saratani.
Mjadala huu ni wa kisayansi zaidi.
Nini mawazo ya watalaam wengine wa afya katika hili
Kimo ni moja ya sababu muhimu kiafya zinazotajwa kuwa na uwezekano wa mtu kupata saratani,na ni wazi kwamba sababu za kimo si kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na sababu nyingine za wazi zinazosababisha ugonjwa huo kama vile uvutaji sigara,ambapo hapo sasa mtu bila kujali kimo chake anaweza kujikuta akipata saratani,lakini msisitizo wa watalaam hawa pia wanasema kuwa kimo huwezi
Georgina Hill, kutoka kitengo cha utafiti nchini Uingereza,yeye anasema kwamba kuna mambo mengi unayoweza kufanya ili kuepuka ugonjwa wa saratani,kama vile kuachana na uvutaji sigara pamoja na kuwa katika uzito wa mwili unaokubalika kiafya
Kwa upande wake Dr John O'Neill, kiongozi wa kundi la utaifi la maabara ya Biolojia ya MRC yeye anasema ikiwa mtu utakuwa na idadi nyingi ya seli upo katika uwezekano mkubwa wa kuwa na saratani,ambapo akizungumzia watu warefu ameelezea kuwa wanaeneo kubwa mwilini ambapo kitaalamu anasema kuwa ni rahisi kwao kukumbwa na saratani ya ngozi kitaalamu ikijulikana kama melanoma.
Profesa Andrew Sharrocks wa Biolojia ya Molekyuli katika chuo kikuu cha Manchester yeye ana mtazamo tofauti kidogo kuhusiana na suala la urefu,ambapo yeye anasema kwamba madhara ya satarani yanaanza kuonekana katika umri mkubwa,hivyo anasema urefu katika kipindi cha kuendelea kukua mtu anaweza asipate madhara ya saratani ila hadi utu uzima wake japo kuwa ni mrefu.
Lakini nini faida za urefu wa kimo?
Ripoti hii kuhusiana na masuala ya urefu na saratani iliyotolewa sasa,inakuja wakati kukiwa na ripoti nyingine ya utafiti iliyotolewa mwaka 2011 kutoka chuo kikuu cha a Oxford inayofanana na utafiti mwingine uliofanywa nchini Sweden mwaka 2015 ambazo zilieleza faida za watu warefu na kwamba hawapaswi kuwa na mashaka kuhusiana na masuala ya afya zao.
Profesa Tim Cole, kutoka chuo kikuu cha London,yeye alisema kuwa watu warefu hawapaswi kuwa na mashaka na matokeo ya utafiti wowote unaobainisha hali ya mashaka dhidi yao.Aliiambia BBC kuwa kuwa mrefu kuna faida nyingi sana kuliko hasara.Lakini akaongeza pia kuwa watu wenye fedha nyingi duniani wengi wao ni warefu,na hata viongozi maarufu duniani wengi wao ni warefu.
Watu warefu wana tazama vipi matokeo ya utafiti huu
Stuart Logan ambaye ni mkurugenzi wa chama cha watu warefu nchini Uingereza UK's Tall Persons Club, anahisi watafiti hawa wamefanya kazi yao isivyo.
Anasema kuwa ndani ya chama chao kilichoanzishwa mwa 1991 kina wanachama wapatao 250 nchini Uingereza na Ireland na pia katika maeneo mengine ya Ulaya,ambapo anasema kuwa watafiti hao wangeliweza kutumia wanachama wao katika utafiti kwa sababu wana vimo sawa na vile vilitakuwa katika utafiti,na kwamba hapo ndipo wangeliweza kuamini matokeo yaliyotolewa.Utafiti huu unaleta mtazamo mpya hata kwa nchi nyingi zikiwemo za Afrika ambapo,jambo kubwa ambalo linahimizwa ni kupunguza uzito ili kujiepusha na baadhi ya magonjwa na kuwa na afya njema.
Lakini ni wachache ambao wamekuwa wakiwaza kwamba urefu kupita kiasi yaweza kuwa sababu ya matatizo,japo watu husikika wakisema aah jamaa kaenda hewani yaani ni mrefu lakini sasa ukiambiwa hivyo huenda ukaenda kupimwa saratani ili ujue mbivu na mbichi kwa afya yako.