Madhara ya kushangaza ya dawa za kupanga uzazi katika ubongo wa mwanamke

Ilikua mwaka 1942 wakati profesa wa somo la kemia kutoka mjini Pennsylvania, nchini Marekani alikua akitafuta chanzo cha homoni progesterone.
Wakati huo homoni hiyo ilikuwa na matumizi mingi.
Ilikuwa miongoni mwa vitu vilivyokuwa vinatumika kuzuia utoaji mimba na tiba kwa wanawake waliofikisha umri wa kutoweza kushika mimba.
Russell Marker tayari alikua amebuni njia ya kutengeza homoni ya kike progesterone kutokana na kemikali inayopatikana ndani ya mmea.
Baada ya kuchunguza mimea 400 tofauti, Marker aligundua mchoro wa ajabu katika kitabu cha mambo ya mimea.
Mchoro huo ulikua wa nduma asili kutoka nchini Mexico.
Mmea huo ulikua maarufu sana na wanasayansi walizuru nchi hiyo kupata mbegu ya kupanda katika mataifa yao.
MwanamkeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMwanamke
Baada ya kupata chanzo cha homoni ya gharama nafuu ya progesterone, watafiti walianza kuitumia kama njia ya kupanga uzazi.
Muongo mmoja baadaye kidonge cha ya kupanga uzazi ikabuniwa.

Siri kuhusu dawa ya kupanga uzazi

  • Umuhimu wa dawa hiyo kiuchumi na kijamii umeangaziwa kwa kina katika tafiti mbali mbali.
  • Kutoka siku moja hadi nyingine watu walifurahia kushiriki tendo la ndoa bila hofu ya kushika mimba.
  • Wanawake waliweza kuendelea na masomo yao badala ya kulea watoto na kufanya kazi nyingine za nyumbani.
  • Hata hivyo kuanzia mwanzo dawa hiyo haikufichua siri fulani.
  • Miaka michache baadaye, wanasayansi waligundua kuwa akili ya mwanamke anayetumia dawa ya kupanga uzazi ilibadilika.
  • Katika maeneo mengine wanawake walikua na muonekano wa ''kiume''
  • Pia waligundua tofauti katika tabia zao. Wanawake wanaotumia dawa za kupanga uzazi walikabiliwa na tatizo la kusahau mambo, hali ambayo si ya kawaida kwa wanawake.
  • cha kushangaza ni kuwa wanawake hao walikua na uwezo wa kukumbuka nyuso za watu walizoona, sifa ambayo inahusishwa na wanaume.
Hali hizi huchangiwa na nini?
  • Wataalamu wa afya ya uzazi wamekuwa wakisema kuwa dawa ya kupanga uzazi imetengenezwa kwa kutumia machanganyiko wa homoni za kike na za kiume.
  • Lakini ukweli ni kwamba hakuna dawa iliyo na homoni hizo
  • Kidonge cha dawa hiyo kimetengenezwa kutokana na homoni imara ambayo imebadilishwa ili kuiga kazi inayofanywa na homoni za kike na za kiume.
  • Japo homoni hizi zina uwezo wa kumkinga mwanamke dhidi ya kushika mimba hazifanani na homini halisi za binadamu.
  • Kutokana na hali hiyo wanawake wanaotumia dawa za kupanga uzazi wanakabiliwa na changamoto kadhaa.
  • Maelfu ya wanawake wameripoti visa vya kutokwa na jasho kupita kiasi, kupata chunusi na kunenepa kupita kiasi.
Mipira ya kondomu haiaminiki kuzuiwa uja uzito ikilinganishwa na mbinu nyingine za kupanga uzaziHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMipira ya kondomu haiaminiki kuzuiwa uja uzito ikilinganishwa na mbinu nyingine za kupanga uzazi
Katika utafiti wa mwaka 2014 uliyochapishwa na mwanasayansi Belinda Pletzer, kutoka chuo kikuu cha Salzburg, nchini Austria ,ameelezea madhara ya dawa hizi katika maumbile ya
wanawake wanaozitumia.
Hata hivyo ni tafiti chache zimeangazia jinsi dawa hizo zinavyoathiri fikira za mtumiaji.
Katika utafiti wake, Pletzer alilinganisha bongo za wanawake waliyotumia aina mbili ya dawa za kupanga uzazi na wale ambao hawajawahi kuzitumia.
Aligundua kuwa sehemu kadhaa ya ubongo wa wanawake waliyotumia dawa mpya iliyo na homoni ya antiandrogenic progestins zilionyesha dalili ya kukua.
Katika maeneo mengine pia wanawake waliyotumia dawa aina ya androgenic, walionyesha dalili ya kuongeza misuli sawa na ile ya wanaume.
Pletzer aidha anasema dawa zote hizo za kupanga uzazi zilizo na homoni ya antiandrogenic progestins zina viungo vinavyofanana na maumbili ya wanawake.
Mwanamke mja mzitoHaki miliki ya pichaAFP
''Hii inamaanisha kwamba ubongo wa wanawake wanaotumia dawa hizo huenda unaathiriwa na vitu viwii wakati mmoja, jinsia ya kiume na ya kike''.
Katika utafiti wake wa mwaka 2014 Bi Belinda Pletzer,anasema wanariadha wanaotumia dawa za kusisimua misuli hudaidai kufanya uhalifu michezoni.
Anahoji kuwa mamilioni ya wanawake duniani wanatumia dawa zilizo na homoni hizo na wengine wao wamezitumia tangu walipo balehe hadi walipofika umri
wa kutoweza kushika mimba na hakuna mtu anayezungumzia suala hilo.
Wanasayansi hata hivyo hawajabaini ikiwa madhara ya dawa za kupanga uzazi kwa ubongo wa mwanawake yana uhusiano wowote na tabia zao.
Huenda kuna haja ya kutafakari wazo hilo.

Post a Comment

Previous Post Next Post