Vaginismus: Tatizo la kuhisi maumivu unaposhiriki tendo la ndoa

Isley Lynn
"Huna uwezo wa kudhibiti yale yanayofanyika ndani ya mwili wako. Uwe umechangia hali hiyo au la."
Isley Lynn anakumbuka mara ya kwanza aliposhiriki tendo la ndo akiwa kijana na anaelezea wakati huo kama wakati ambao haukua na maana yoyoyte kwake.
"Nilihisi kuvunjika moyo sana. Nilijihisi nimekosa kwa jambo ambalo halikuwa kosa langu."
Baadhi ya watu huenda wamejikuta katika hali kama hii waliposhiriki tendo la ndoa kwa mara ya kwanza.
Lakni kwa Isley ilikuwa vibaya zaidi kwa sababu hakua na ufahamu wowote kuhusiana na hali hiyo inayofahamika kama vaginismus na watu hawaizungumzii kama tatizo la kimatibabu linalofaa kuangaziwa.
Isley,ambaye sasa ana miaka 30, bado anakabiliwa na tatizo la 'vaginismus' yaani kuhisi uchungu kila unaposhiriki tendo la ndoa.
Sasa ameamua kuandika mchezo wa kuigiza unaofahamika kama Skin a Cat ili kusimulia yale anayokabiliana nayo maishani.
Mchezo wa kuigiza wa Skin a Cat unaangazia maisha ya wanawake wenye tatizo la vaginismusHaki miliki ya pichaTHE OTHER RICHARD
Image captionMchezo wa kuigiza wa Skin a Cat unaangazia maisha ya wanawake wenye tatizo la vaginismus
Kwa mujibu wa huduma ya kitaifa ya afya NHS, vaginismus ni sawa na majibu ya moja kwa moja ya mwili kuwa na hofu ya baadhi au aina yoyote ya kitu kupenya kwa uke.
Misuli ya uke huwa ngumu na wakati huo mwanamke hana udhibiti wa mwili wake.
Wakati mwingine ni vigumu kwa mtu aliye na tatizo hilokutumia hata tampon, akiwa kwenye hedhi.

Mhasiriwa pia hapata shida kushiriki tendo la ndoa kwa sababu ya kuhisi maumivu makali.
Isley anasema: "Nilijaribu kutumia tampon mara ya kwanza nikiwa na miaka 10.
''Nilihisi uchungu sana, kana kwamba hapakuwa na njia, nilihisa kama kulikua na ukuta badala ya sehemu ya siri ya mwanamke''
Isley ameongeza kuwa alijua anakabiliwa na tatizo kubwa hasa baada y akusjaribu kushiriki tendo la ndoa.
TamponsHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWatu walio na tatizo la vaginismus huenda wakapata shida kutumia tampons
Hali hiyo iliathiri pakubwa uhusiano wa Isley wa kimapenzi.
"Nakumbuka nilikuwa na hofu huenda mpenzi wangu akafikiria simpendi," .
Mwandishi huyo wa michezo ya kuigiza alipatikana na ugonjwa wa vaginismus akiwa kijana.
Daktari alijaribu kutumia kifaa maalumu kilichoingizwa ndani ya uke wake.
Kifaa hicho kiliongezwa ukubwa taratibu ili kusaidia kutuliza misuli katika eneo la uke wake.
Licha ya juhudi zote hizo za kutafuta matibabu Isley,anasema kwa muda mrefu hakupata suluhisho la kudumu.
Daktari akimtibu mgonjwaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
"Wakati mmoja daktari aliniuliza ikiwa nina haja sana ya kutibu hali yangu.
"Hayo ni mazungumzo unayojionea katika sehemu ya mwisho wa mchezo wa kuigiza, ambapo mhusika anaulizwa kuelezea kile anachotazamia katika maisha yake.
"Ni hapo aligundua si lazima afurahie tendo la ndoa kama kila mtu.
"Kumaanisha kuwa unaweza kujiamulia kile unachotaka maishani kwa kufanya kile unachofurahia."
wapenzi kitandaniHaki miliki ya pichaSCIENCE PHOTO LIBRARY
Ni vigumu kukadiria ni wanawake wangapi nchini Uingereza wanakabiliwa na tatizo la vaginismus japo utafiti wa hivi karibuni umebaini kuwa mmoja kati ya wanawake kumi nchini humo huhisi uchungu wakati wanaposhiriki tendo la ndoa. Hata hivyo idadi hiyo huenda imechangiwa na sababu tofauti- vaginismus ikiwa ni mojawapo.

Dkt Vanessa Mackay, mtaalamu wa afya ya uzazi kutoka hospitali ya chuo kikuu cha Queen Elizabeth mjini Glasgow anasema,"Vaginismus ni tofauti na hali ya kuhisi maumivu makali wakati wa kushiriki tendo la ndoa kwa sababu hali hiyo hutokana na mfumo wa mwili wa mtu binafsi''
Pia anasema mbali na kushughulikia matibabu ya upande wa kimwili ni vyema pia kuzingatia matibabu ya kiakili kwa sababu muathiriwa anakabiliwa na hofu ya kupenya kwa kitu chochote katika uke wake.
Dkt Mackay anasema kuwa mgonjwa anastahili kupewa ushauri nasaha." Hali hiyo ya matibabu itamsaidia kufahamu mabadiliko ya hisia akilini mwake sambamba na mwili wake''
BBCHaki miliki ya pichaTERESA
Image captionTeresa ana tatizo la vaginismus
Teresa,mwenye umri wa miaka 23,ambaye pia anakabiliwa na tatizo vaginismus na anasema baada ya kupatikana na hali hiyo amepewa aina tofauti za matibabu.
"Nimejaribu kila aina ya matibabu na hakuna hata moja iliyonisaidia. Nimekuwa nikijiuliza ikiwa nitawahi kupata matibabu''.


Teresa hata hivyo ameongeza kuwa njia pekee ya kupata matibabu ni kujifunza kuwa mtulivu.
Anasema kuna vifaa maalum vinavyotumika kumsaidia mgonjwa kupata utulivu.
"Maisha sasa ni mazuri sana, sina hofu tena, Ilikuwa vigumu mwanzoni lakini nadhani unapopata suluhisho lako binafsi inakuwa ni rahisi kutoka katika hali hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post