Ukosefu wa vimelea vya magonjwa ndicho chanzo saratani miongoni mwa watoto, kwa mujibu wa wanasayansi wakuu nchini Uingereza.
Saratani ya damu inayofahamika kama lymphoblastic leukaemia inaathiri mmoja kati ya watoto 2,000.
Prof Mel Greaves, kutoka taasisi ya utafiti wa saratani amekusanya ushahidi wa miaka 30 kuonyesha kuwa kinga ya mwili inaweza kugeka na kuwa saratani ikiwa haitapambana na magojwa mapema katika maisha ya mtoto.
Ina maana kuwa itakuwa vigumua kuuzuia ugonjwa huo.
Aina hii ya saratani ya damu inaathiri sana watoto katika nchi zilizostawi na kuonyesha kuwa maisha ya kisasa yanaweza kuwa chanzo cha saratani hiyo.
Kumekuwa na madai ya kuhusisha saratani hiyo na nyaya za umeme, miale au kemikali.
Hayo yote yametupiliwa mbali kwenye utafiti uliochapishwa
Utafiti sio kabisa kuhusu kuwalaumu wazazi kwa kudumisha usafi wa juu.
Bali unaonyesha kuwa kuna gharama ya kulipa licha ya hatua ambazo zimepigwa katika jamii na matibabu.
Kukaribiana na vimelea vyenye manufaa ni jambo gumu na sio tu kwa kuruhusu mazingira machafu.
Lakini Prof Greaves anasema kuwa visa vingi vya saratani ya watoto vinaweza kuzuiwa.
Kulingana na maoni yake ni kuwa kuwaruhusu watoto kukaribiana na vimeala ili kuwezesha mwili kujifunza namna kujiking.
Pia Prof Greaves anawashauri wazaz kutokuwa na hofu ya maambukizi na kuwaruhusu watoto wao kukaribiana na wengine na wale wa umri mkubwa.