Virusi vya HPV: Unaweza kupata virusi hivyo kupitia ngono salama

Laura Flaherty
Utafiti mpya umebaini kuwa viwango vya juu vya ukosefu wa kujua pamoja na fedheha inayohusishwa na virusi vinavyosababisha magonjwa ya zinaa yaani HPV, huathiri 80% ya watu.
Serikali ya Uingereza imezindua vipimo vya HPV kama sehemu ya uchunguzi wa kawaida wa saratani ya shingo ya uzazi.
Karibu nusu ya wanawake waliyohusishwa katika utafiti huo waliamini kuwa wapenzi wao huenda walishiriki mapenzi na mtu mwingine na kuwaambukiza virusi hivyo japo inaarifiwa kuwa virusi vya HPV, vinaweza kuwa hai katika mwili wa binadamu kwa miaka kadhaa.

Wanaharakati wanahofia wanawake huenda wasikubali kufanyiwa uchunguzi kwa sababu ya kuogopa kutengwa.
Utafiti huo uliyohusisha wanawake 2,000 ulifanywa mwezi uliyopita na hazina Jo ambayo jukumu lake ni kupambana na saratani ya shingo ya uzazi.
Utafiti huo ulibaini kuwa nusu ya wanawake waliona aibu na kusitisha kufanya mapenzi kwa kuhofia aambukizwa virusi vya HPV.
Karibu 35% ya wanawake hawakuwa na ufahamu HPV ni nini na wengine karibu 60% walijibu kuwa inamaanisha wanaugua saratani.
Laura Flaherty, 31, aliyepatikana na saratani ya malango wa uzazi mwaka 2016, ni mmoja wao.
"Kwanza nilipoona barua ya matokeo ya vipimo vyangu vimethibitisha niko na virusi vya HPV,sikuelewa hiyo ni nini. Nilipotafuta maana yake kwenye mtandao wa Google nikafahamu ni ugonjwa wa kuabukiza wa zinaa , kwa hiyo moja kwa moja nidhani mpenzi wangu alikuwa na anatembea na wanawake wengine.
"Sikuelewa choco kuhusiana na ugonjwa huo lakini nilijihisi mchafu. Sikujua huenda nilikuwa na virusi hivyo kwa muda mrefu. Nilipoarifiwa kuwa HPV ni virusi vya kawaida nishangaa sana. Sikuwahi kusikia lolote kutoka kwa watu niliyosema nao, huku wengi wao wakiwa katika hatari ya kuabukizwa.

Kukabiliana na dhana fiche kuhusu virusi vya HPV

Dhana: Unaweza kupata virusi vya HPV kwa njia ya kujamiana pekee
Ukweli: HPV sana sana huenezwa kwa njia ya kujamiana lakini pia mtu anaweza kupata virusi hivyo kugusana kimwili hasa maeneo ya utupu na mtu aliye navyo.
Dhana: HPV ni inaashiria mtu ni mzinifu
Ukweli: 80% ya watu watapatikana na virusi vya HPV wakati mmoja katika maisha yao, ni rahisi kupata virusi hivyo na kuvisambaza kwa mto wa kwanza utakayefanya mapenzi nae
Dhana: HPV inamaanisha niko na maradhi ya saratani
Ukweli: Kuna karibu aina 200 ya HPV. Karibu aina 40 ya virusi hivyo huathiri maeneo ya utupu, hii ina maananisha virusi hivyo vitaishi maeneo hayo ya mwili na baadhi ya virusi hivyo huenda vikasababisha magonjwa ya zinaa. Karibu aina 13 ya virusi hivyo huenda vikasababisa saratani ya shingo ya uzazi na aina nyingine ya saratani kama vile ya mdomo au koo lakini visa hivyo ni vichache.
Dhana: Utajua ikiwa una virusi vya HPV
Ukweli: HPV haina dalili zozote na wakati mwingine mfumo wa kinga ya mwili huweza kukabiliana na maambukizi. uchunguzi wa shingo ya uzazi unaweza kubaini seli zozote tumbo
Utafiti huu unakuja wkati serikali iko katika harakati ya kuzindua mpango wa kwanza wa watu kufanyiwa uchunguzi wa virusi vya HPV katika eneo la shingo ya uzazi. Wales itakuwa ya kwanza kuendesha mpango huo wiki ijayo haijazinduliwa England kufikia mwaka 2019 na baada kupelekwa Scotland ifikapo 2020 japo muda wa zoezi hilo Ireland kaskazini haujatolewa.

picha inayoashiria hali ya mgonjwa wa zinaaHaki miliki ya pichaSIPHOTOGRAPHY
Image captionVipimo vya kwanza vya HPV vimeanzishwa Wales juma hili

Robert Music, Afisa mkuu mtendaji wa, wakfu Jo wa saratani ya shingo ya uzazi, amesema: "Uchunguzi wa HPV kwanza ni njia bora zaidi ya kuwatambua watu waliyo katika hatari ya kupat asaratani ya shingo ya uzazi. Mabadiliko haya ya utaratibu wa uchunguzi haimaanishi wanawake wengi zaidi wataambiwa wana virusi vya HPV.
"Virusi vya HPV hata hivyo vinaweza kuchanganya watu,kwa hiyo ni vyema kuwahamasisha wasiwe na hofuu wala kuona aibu wanapoambiwa kuwa wana virusi hivyo."

Viwango vya maambukizi ya virusi vya HPV vimepungua kwa wasichana waliyo na umri wa kati ya miaka 12 na 18 kufuatia chanjo ya kukabiliana na virusi hivyo iliyoanzishwa mwa 2008.
Mwaka jana chanjo hiyo iliwajumuisha wanaume waliyo na umri wa kati ya miaka 16 hadi 45 na ambao ni wapenzi wa jinsia moja. Kufikia mwezi Julai mwaka huu serikali ya Uingereza ilitangaza hatua ya kutoa chanjo hiyo kwa wavulana pia japo haijatoa tarehe ya kuanzishwa kwa mpango huo.
Wataalamu wa masuala ya afya wanatarajiwa kuendeleza mdahalo kuhusu virusi vya HPV na wagonjwa katika juhudi za kuimarisha uelewa wao wa ni vipi virusi hivyo vinavyosambazwa na jinsi ya kukabiliana na suala la unyanyapaa.

Post a Comment

Previous Post Next Post