utengenezaji wa nyama za kuku maabara kutokana na unyoya

kuku
Hofu ya ongezeko la ulaji nyama duniani, imewafanya wanasayansi kuvumbua mfumo wa kutengeneza nyama ya kuku katika maabara kutokana na seli ya unyoya wa kuku.
Kampuni moja ya chakula mjini San Francisco imevumbua mfumo wa kukuza nyama ya kuku katika maabara kutokana na seli ya unyoya wa kuku.
Ladha ya nyama hiyo-ni sawa na ile ya kuku wa kawaida,tofauti ni kuwa imekuzwa kitaalamu katika maabara kutokana na seli ya mnyama.
Wanasayansi wanasema kuwa inachukua karibu siku mbili kutengeneza vipande vya nyama ya kuku katika maabara kwa kutumia protini ili kuiwezesha seli kupata umbo la nyama kadiri inavyokuwa.

Nyama ya kuku iliyotengenezwa katika maabara
Image captionNyama ya kuku iliyotengenezwa katika maabara

Afisa mkuu mtendaji wa shirika linalojihushisha na mpango huo, Josh Tetrick amesema majaribio ya kuuza nyama hiyo katika migahawa migahawa mikubwa duniani itaanza kufikia mwisho wa mwaka huu.
Tetrick pia amesema "Tunatengeneza vitu kama mayai au barafu iliyo na krimu au siagi kutokana na mimea sawa na jinsi tunavyo tengeneza nyama kutokana na nyama. Hakuna haja ya kkuangamiza wanyama.
McDonalds au KFC walipewa nyama hiyo kujaribu katika mapishi yao na matokeo yalikua mazuri sana.
Tetrick na wajasiri amali wengine wanaotengeneza nyama mbadala kwa kutumia njia ya kisayansi wanasema lengo lao ni kusitisha uchinjaji wa wanyama na kuhifadhi mazingira.
Umoja wa Mataifa unasema kufuga wanyama kwa ajili ya chakula ni moja ya vitu vinavyochangia ongezeko la joto duniani pamoja na uharibifu wa mazingira.
Dr Uma Valeti, mtaalamu wa magonjwa ya moyo ambaye pia ni mwanzilishi wa kampuni maarufu utengenezaji nyama ya Memphis mjini California-Memphis, anasema watu huchinja wanyama bilioni 70 kila mwaka ili kuwalisha watu billioni saba.

Mahitaji ya nyama inazidi kuongezeka duniani
Image captionMahitaji ya nyama inazidi kuongezeka duniani

Anasema ongezeko la mahitaji ya nyama duniani imefika kiwango cha juu huku kukiwa na hofu kwamba watu watashindwa kufuga wanyama.
"Kile tunachoweza kufanya ni kukuza nyama ya aina yoyote katika maabara, iwe ni ya kuku au samaki moja kwa moja kutokana na seli ya wanyamahaos"
Wamarekani wengi wanasema kua hawali nyama lakini takwimu kutoka wizara ya kilimo zinaashiria kuwa wamekula zaidi ya kilo 100 ya nyama nyekundu na kuku zaidi ya jinsi walivyokula bidhaa hiyo miaka ya 1970.
Mwanasayansi Mark Post ambaye ni mwanzilishi wa bidhaa za kilimo zinazokuzwa kwa njia ya kisayansini nchini Ujerumani anasema maabara yake ya kwanza iliunda hamburger, kwa gharama ya dola 300,000 sawa na (£228,000), mwaka 2013
Anasema gharama hiyo ni ya juu sana hali ambayo inawatia hofu wanasayansi wengi kujiingiza katika biashara hiyo.
Kuna mataifa kadhaa ya bara Ulaya na Asia ambayo yameshauriana na Dr Uma Valeti, kuhusiana na suala la kutengeneza nyama katika maabara.

Kalena and Billy Bruce, with Willa
Image captionKalena na Billy Bruce, pamoja na Willa

Dr Valeti anasema''Nadhani mataifa yanataka kuwekeza katika mfumo huu iwe ni kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa chakula au kuimarisha uchumi wao''.

Amesema siku zijazo anatazamia kutengeneza nyama hiyo katika viwanda vikubwa badala ya maabara.
Mjadala kuhusiana na nyama inayokuzwa kupitia njia ya kisayansi ikiendelea kushika kasi, baadhi ya wafugaji wanahoji jinsi bidhaa hiyo itakavyo uzwa- Je ni nyama safi, nyama bila myama kuchinjwa, ptotini safi au nyama ya kawaida tu.

Post a Comment

Previous Post Next Post