Kondom ikipasuka nini unatakiwa kufanya?

Mipira ya kondomu
Mtu mmoja nchini Kenya amevishtaki vitengo vya serikali na kampuni za kuuza dawa kuhusu mpira wa kondomu uliopasuka na kumfanya kuambukizwa magonjwa.
Mlalamishi anataka kulipwa fidia kutoka kwa kampuni ya dawa ya Beta Healthcare Limited kufuatia kisa hicho ambacho anasema kuwa kondomu hiyo ilipasuka alipokuwa akifanya mapenzi na mpango wake wa kando swala lililosababisha ndoa yake kuvunjika.
Kulingana na mwandishi wa BBC Ferdnand Omondi mtu huyo anasema kwamba alitumia kondomu hiyo kufanya mapenzi na mwananmke aliyekutana naye katika harusi, lakini ikapasuka wakati wa tendo la ngono.
Anasema kuwa alipuuzilia mbali kisa hicho na siku tatu baadaye akafanya mapenzi na mkewe.
Lakini siku chache baadaye alipatikana na ugonjwa wa zinaa. Mkewe pia aliambukizwa na baadaye alimwacha na kwenda kwa mwanamume mwengine.
"..Nilikuwa nikifanya tendo la ngono na mwanamke huyo , ndiposa mpira huo wa kondomu ukapasuka , swala nililogundua baada ya tendo hilo. Wakati huo nilipuuzilia mbali kisa hicho na siku tatu baadaye nilkifanya tendo la ndoa na mke wangu'', alisema.
Mlalamishi sasa anataka kampuni ya Beta health Care-kampuni ya dawa inayouza mipira hiyo ya kondomu kumlipa kwa dhiki na hasara ya kibinafsi aliyopata wakati wa kisa hicho.

Mipira ya kondomu ikitengezwa katika kiwanda
Image captionMipira ya kondomu ikitengezwa katika kiwanda

Pia anataka halmashauri ya kutoza kodi KRA na ile ya ubora wa bidhaa KBS kupigwa faini kwa kuruhusu bidhaa zisizofikia viwango vya kuingia humu nchini kuuzwa kwa raia.
Mwaka 2009 Kenya ilipiga marufuku aina moja ya mipira ya kondomu siku chache tu baada ya taifa la Zambia kutekeleza hatua hiyo kutokana na mipira ya kondomu iliodaiwa kupasuka
Chapa hiyo ya mipira ya kondomu kwa jina Hot ambayo hutengenezwa kutoka Uingereza iligunduliwa kuwa na tatizo hilo kufuatia habari iliopeperushwa hewani na runinga moja.
Maafisa waliipiga marufuku baada ya vipimo vyake kuonyesha kwamba vina udhaifu.
Serikali ya kenya inayosambaza takriban mipira ya kondomu milioni 160 kila mwaka , ilihofia kwamba habari kuhusu kuvuja kwa mipira ya kondomu zinaweza kuathiri vita vyake dhidi ya HIV.

Hapa kuna hatua nne za kufuata iwapo kondomu imepasuka:

1. Kuwa mtulivu na baadaye tafuta kondomu hiyo iliopasuka.

Mara nyengine vipande vya mpira huo wa kondomu unaweza kuingia ndani ya mwili.
Ingiza vidole vyako ndani yake ishike na kuitoa nje.
Mipira ama vipande vya kondomu vinavyosalia ndani ya mwili wa binadamu vinaweza kusababisha hasira hivyobasi ni muhimu kuangalia na kuhakikisha kuwa umetoa kondomu yote.

2. Tumia dawa za kuzuia kushika mimba iwapo hamjakubaliana kupata mtoto pamoja

Dawa hizi zinapaswa kutumiwa katika kipindi cha saa 72. Zinauzwa dukani-ikimaanisha kwamba zinapatikana katika maduka ya dawa.
Iwapo huna mpango mbadala unaweza kutumia dawa za kupanga uzazi.

3. Kupimwa magonjwa ya zinaa hususan HIV iwapo hujui hali ya mwenzako

Nenda katika kituo cha dharura karibu nawe na umwambie daktari yaliofanyika.
Pia unaweza kuchukua dawa aina ya Post Exposure Prophylaxis (PEP) katika kipindi cha saa 72.

Mwanamke katika duka la jumlaHaki miliki ya pichaBEHROUZ MEHRI

PEP ni mchanganyiko wa dawa za kukabiliana dhidi ya virusi vya ukimwi ambazo zinakuzuiwa kutoambukizwa HIV iwapo mwenzako ni mwathiriwa.
Kumbuka kwamba kila ugonjwa wa zinaa una muda wake wakati unapoambukizwa na wakati utakapoonyesha unapopimwa.
Unashauriwa kufanyiwa vipimo zaidi vya vya magonjwa ya zinaa baada ya mwezi na baada ya miezi sita ili kujua hali yako.

4. Chunguza kilichotokea

Wapenzi wengi huruka hatua hii-hayo ni makosa makubwa, kwa sababu ni hadi utakapoelewa ni kwa nini mpira huo ulipasuka ndiposa unaweza kujiweka katika hatari nyengine. Hivyobasi jiulize swali hilo.
  • Je mpira huo wa kondomu ulipasuka kwa sababu wakati wake ulikuwa umekwisha?
Iwapo hilo ni kweli unaweza kutupa paketi ulio nayo na kununua pakiti nyengine . Ziweke mbali na joto ama hata mwangaza na usizibebe katika kipochi chako na usizifungue kwa kutumia makasi ama meno.
  • Je mpira huo wa kondomu ulipasuka kwa sababu ulivaliwa vibaya?
Weka mafuta ndani ya kondomu hiyo iwapo utahitaji , lakini hakikisha kuwa hutumii mafuta nje ya mpira huo, Finya eneo la mbele la mpira huo ili kutoa upepo Ukishavaa kondomu hiyo wacha nafasi mbele ya mpira huo ambayo itaweka shahawa.
  • Je mpira huo wa kondomu ulipasuka kwa kuwa ulikuwa mdogo sana?

Pima ukubwa wa uume wake wakati unaposimama. Halafu uangalie chapisho hili ili kujua ni ukubwa gani wa kondomu unaopaswa kutumia. Unaweza kushangaa!
  • Je mnpira huo wa kondomu ulipasuka baada ya kuupaka mafuta?
Utumizi wa mafuta kama vile ya Olive ama mafuta ya nazi unaweza kuwa hatari kwasababu yanaweza kufanya kondomu kupasuka
Kumbuka kwamba ajali za kondomu zinaweza kumtokea mtu yeyote.

Post a Comment

Previous Post Next Post