Je ultra sound huathiri jinsia ya mtoto tumboni?

Kufahamu jinsia ya mtoto akiwa tumboni kwa kutumia teknolojia ni mtindo ambao umekuwa ukipata umaarufu, lakini pia kuzua mdahalo mkubwa hasa katika nchini za Kiafrika.
Kila mtu na imani yake, baadhi ya kina mama huamini kujua jinsia ya mtoto mapema ni kutafuta mikosi.
Lakini wengine huamini ni jambo jema kwani inakupa fursa ya kujiandaa na vitu muhimu vya mtoto, kwa mfano mavazi na pia jina la mtoto.
Wanawake wa kisasa hupendelea zaidi kujua jinsia ili waweze kuandaa sherehe maalumu inayoitwa Baby Shower. Katika sherehe hii akina mama hawa huweka wazi jinsia ya mtoto kwa kupamba mandari ya pinki kwa mtoto wa kike na buluu kwa mtoto wa kiume.
Baadhi hupokea zawadi zenye rangi mbali mbali zisizobagua jinsia mfano rangi nyeupe, kijivu, njano na hata nyeusi na nyekundu.
Si wote wanaotafuta kujua jinsia ya mtoto mapema kwa ajili ya sherehe, wengine hutafuta kujua ili wajiandae na mavazi ya mtoto.
Baby showerHaki miliki ya pichaDEBORAH NGAJILO
Image captionBaadhi ya kina mama hufurahia zaidi kufanya sherehe ya kumkaribisha mtoto punde wanapo jua jinsia.
Katika harakati za kufahamu jinsia ya mtoto kitamaduni kuna mambo mengi sana hufanyika, kwani baadhi hutoa majibu ya jinsia ya mtoto kwa kumwangalia mama mjamzito kwa macho tu.
Hawa huamini mwonekano wa mama anapokuwa na mimba unatafsiri amebeba mtoto wa jinsia gani.

Mtoto wa kike ana wivu?

Baadhi husema mama mjamzito akivimba na kuharibika sura maana yake amebeba mtoto wa kike, kwani mtoto wa kike anawivu. Lakini kama mama mjamzito anapendeza ngozi sura na shepu huyu amebeba mtoto wa kiume kwa sababu watoo wa kiume hawana wivu.
Lakini njia inayoaminika zaidi ni kutazama jinsia kwa kutumia kifaa maalumu cha hospitali yaani kufanya Ultrasound.
BBC imezungumza na baadhi ya kina mama kufahamu mtazamo wao juu ya kuangalia jinsia ya mtoto.
Kufahamu jinsiaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mama Janeth yeye anaumri kati ya miaka kati ya 55 na 63 anasema hajui lolote kuhusu kuangalia mtoto akiwa tumboni na haaminikuna manufaa ya kufanya hivyo.
"Mimi sijawahi kuangalia jinsia ya mtoto, kwanza unaangalia vya nini? Kwa kweli kusema ukweli mimi sijui kabisa kuhusu hicho kitu," anasema mama Janeth.
Naye Viola, mama wa watoto watatu, anasema alikuwa na hamu ya kujua jinsia lakini awali hakukubaliana na matokeo ya daktari akataka mpaka ajifungue ndio aamini.
"Mimi kikubwa kilichonisukuma ni kwa sababu nilikuwa na wawili wa kiume mmoja wa kike kwa hivyo nafsi yangu nlitamani nizae mwingine wa kike kwa hiyo nikaangalia lakini nlipoambiwa wa kiume sikuamini. Yaani mpaka nikanunua vitu vya mtoto vya rangi zisizobagua basi nilipojifungua kuona kweli wa kiume ndo nikaamini," Violla anaiambia BBC.
BBC pia imezungumza na mama wa watoto wa wili Joyce Mbogo yeye anasema mambo yamebadilika sasa.
"Watu wanaenda na wakati halafu pia tunapenda kufanya maandalizi ya mtoto. Ujue siku hizi sio kama zamani kipindi mtoto anavaa nguo yoyote ya rangi yoyote, siku hizi nmambo yamebadilika. Kama ni mtoto wa kike aonekane ki-kike zaidi na kama ni wa kiume aonekane kiume zaidi," Joyce anaiambia BBC.
Joyce anasema kufahamu jinsia kulimsaidia kujiandaa vyemaHaki miliki ya pichaHISANI
Image captionJoyce anasema kufahamu jinsia kulimsaidia kujiandaa vyema
"Kwa sababu hata mimi nilifanya kwa mtoto wangu wa kwanza, ilinisaidia nikaandaa vitu vya mtoto mvulana, yaani ni kitu kizuri,"
Wapo wale ambao wanatajiwa jinsia ya mtoto lakini hawakutaka kujua.
"Yaani daktari aliponiambia tu mtoto wako wa kiume, nililia kama mtoto kwa sababu mimi hua siamini katika hizo habari. Niache na mimba yangu napokea mtoto yeyote ninayeletewa na mwenyezi Mungu," Aisha ameiambia BBC.

Kuna madhara yoyote?

Dkt Abdiel Mmile kutoka katika hospitali ya BOCHI jijini Dar es Salaam, anasema hakuna madhara yoyote japo waweza pata changamoto ya kisaikolojia.
"Kwa mfano una watoto wawili au watatu wa jinsia moja alafu ukapata majibu mtoto aliye tumboni ni wa jinsia ileile, unaathirika kisaikolojia na kuna uwezekano wa kupuuzia huo ujauzito kidogo," anasema.
"Kitaalamu hakuna madhara ila kisaikolojia hii hali ujitokeza."
Daktari anasema kuwa mwanzoni ilitumika X-Ray kubaini jinsia ya mtoto mtoto lakini baadae ikaonekana kwenye mimba changa si salama kwa sababu ya mionzi nururishi.
Kwa hivyo ikaja Ultrasound ambayo yenyewe hutumia sauti ya mawimbi badala ya mionzi.
Dkt Mmile anasisitiza kuwa umuhimu wa kuangalia jinsia uliongezeka umaarufu wakati ambapo nchi nyingine ziliweka marufuku ya kuwa na mtoto zaidi ya mmoja mfano China.
Wakati huo waliruhusiwa kuchagua jinsia ya mtoto wanayemtaka na waliruhusiwa hata kutoa mimba kama ulitaka mtoto wa kike akaja wa kiume.
"Kama unaruhusiwa kuzaa watoto idadi yoyote ile hamna ulazima wa kujua jinsia," Dkt Mmile aliambia BBC

Post a Comment

Previous Post Next Post