Wanawake ambao vidole vyao vya pete na kidole kinacho fuata baada ya kidole gumba katika mkono wa kushoto vina urefu tofauti wana uwezekano mkubwa wa kuwa na mahusiano ya jinsia moja, utafiti unaonyesha.
Wanasayansi wamepima jozi 18 za vidole vya mapacha wa kike wanao fanana, ambapo mmoja alikuwa sawa na mwingine ni shoga.
Kwa wastani, wale waliokuiwa katika mapenzi ya jinsia moja walikuwa na ripoti tofauti ya ukubwa wa vidole ambapo kawaida ni tabia ya kiume lakini hii ni kwa mkono wa kushoto pekee.
Hii inaweza kuwa ni matokeo ya kuwa na homoni za testosterone kwenye tumbo, utafiti wa chuo cha Essex unasema.
Wanasayansi hao pia walipima dazeni 14 ya vidole vya mapacha wakiume wanao fanana, ambapo mmoja alikuwa sawa na mwingine alikuwa shoga, lakini hapa hawakuona uhusiano wowote.
Kwa upande wa wanawake, kawaida kidole cha pili kutoka kidole gumba na kidole cha pete huwa vina urefu sawa. Wakati kwa wanaume kuna tofauti kubwa baina ya vidole hivyo.
Wote wanawake na wanaume walipata homoni za kiume za testesterone wakiwa bado tumboni, lakini baadhi wanaweza kuwa walipata homoni hizo nyingi Zaidi tofauti na wengine, wanasayansi wanasema.
Mwandishi wa utafiti huo daktari Tuesday Watts kutoka kitengo cha saikolojia katika chuo kikuu cha Essex anasema,
"Kwasababu mapacha wanao fanana ambao wana shea asilimia 100 ya jenes wanatofautiana katika mwelekeo wao kijinsia sababu zingine tofauti na sababu za kijenetiki lazima zinahusika.
Tafiti zinasema kwamba jinsia zetu zinatambuliwa ndani ya tumbo na inategemea kiasi cha homoni za kiume ambazo mtu amezipata akiwa tumboni au namna mwili wa kila mtu unavyo pokea homoni hizo, na wale ambao wanao pata homoni hizo za kiume kwa kiwango cha juuwanauwezekano wakuwa mashoga au watu wanao weza kuwa na mahusiano na jinsia yoyote ile.
"Wote wanawake na wanaume walipata homoni za kiume za testosterone wakiwa bado tumboni, lakini baadhi wanaweza kuwa walipata homoni hizo nyingi zaidi tofauti na wengine"