Mvinyo mwekundu awali ulihusishwa na faida mbali mbali za kiafya, kuanzia kusaidia kupunguza kihatari za kupata magonjwa ya moyo na na kisukari.
Sasa utafiti mpya unasema mvinyo huu una kemikali ambazo zinakabiliana na kuoza kwa meno na ugonjwa ufizi.
Watafiti walibaini kuwa mchanganyiko wa kemikali unaotengeneza kinywaji hicho, unaofahamika kama polyphenols, husaidia kumaliza kuwamaliza vimelea (bakteria) hatari kinywani.
Mkimbizi avikwa 'taji la mvinyo' Ujerumani
Lakini watafiti hawa wanaonya kuwa matokeo ya utafiti wao hayatoi "ruhusa'' ya kunywa mvinyo kupita kiasi.
Utafiti wa awali ulionnyesha kuwa faida za kiafya za polyphenols zilihusishwa na kuwa na uwezo wa kuulinda mwili dhidi ya vimelea hatari wanaoshambulia mwili.
Kangaroo afariki katika kiti akiwa na mvinyo Australia
Hata hivyo, utafiti wa hivi karibuni umeonyesha kuwa kemikali salama ya polyphenols inaweza kuboresha afya kwa kufanya kazi na "vimelea wazuri " katika tumbo zetu.
Katika utafitihuu uliochapishwa katika jarida la Kemikali za Kilimo na Chakula , wanasayansi walichunguza ikiwa kemikali ya mvinyo ya polyphenols inaweza pia kuwa nzuri kwa afya ya kinywa.
China yashinda tuzo la kutambua mvinyo duniani
Watafiti walilinganisha athari za aina mbili za kemikali ya polyphenols kutoka kwa mvinyo mwekundu dhidi ya mbegu ya zabibu na kiasi kidogo cha mvinyo mbadala kwenye bakteria wanaoganda kwenye ufizi na meno na kusababisha magonjwa ya kinywa, kuoza kwa meno naugonjwa wa ufizi.
Walibaini kuwa kemikali ya mvinyo na mvinyo kwa pamoja vilipunguza uwezo wa Bakteria wa kukaa kwenye seli, lakini kemikali zaa polyphenols - caffeic na p-coumaric acids - zilifanya kazi bora zaidi .
Unaweza kupata wapi kemikali salama za polyphenols?
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Zabibu ni chanzo bora cha kemikali za polyphenols
Mvinyo mwekundu una kiwango kikubwa cha kemikali za polyphenols, lakini pia zinaweza kupatikana katika machungwa na vinywaji na vyakula vifuatavyo:
Vinywaji:
Kahawa
Chai ya majani chai mabichi
Chai ya kawaida ya majani
Maji ya matunda tufaha
Maji ya machungwa na limao
Katika vyakula hupatikana katika:
madini ya bluberi
maharagwe
Zabibu nyeusi