Mshubiri ni mmea wenye Miujiza ya kutibu maradhi sugu kama ugonjwa wa Saratani (Cancer), ugonjwa wa Kisukari, kolesto, ugonjwa wa kuvimba sehemu ya mwili na magonjwa mengine mengi.
Faida za mmea wa aloe vera au mshubiri
1. Huondoa uvimbe katika jicho
Weka kiasi kidogo cha majimaji ya mu-aloe vera freshi kisha kuamka asubuhi, acha kwa dakika kadhaa kisha jisafishe. Uvimbe lazima ukimbie. Pia unaweza kuloweka pamba katika majimaji ya mualoe vera na kisha jisafishe katika jicho lenye uvimbe.
2. Huzuia na kuondoa michirizi ya tumbo itokanayo na ujauzito
Anza kwa kupakaa majimaji ya mualoevera juu ya tumbo lako na ufanye kama masaji hivi taratibu juu ya tumbo mara 2 kwa siku katika kipindi chote cha ujauzito na baada ya kujifungua kwa miezi michache mpaka michirizi ipotee yote.
3. Hutibu bawasiri
Ile ile sifa moja iliyonayo ya kutibu uvimbe ambayo inaweza pia kutibu malengelenge na uvimbeuchungu kwenye mwako wa mwili, ndiyo hiyo hiyo pia husaidia kutibu au kupunguza maumivu ya bawasiri. Chana tawi la aloe vera freshi na upate jeli yake, kisha pakaa eneo linalosumbuliwa na bawasiri mara mbili mpaka tatu kwa siku kwa wiki kadhaa hasa kama bawasiri imejitokeza sehemu ya nje hadi hapo uvimbe huo utakapopotea.
4. Ni tiba kwa matatizo ya tumbo
Kama utainywa, hutibu vidonda vya tumbo na kiungulia, na kwa ujumla ni kuwa husafisha mfumo wote wa mmeng’enyo wa chakula. Chukua jeli ya aloe vera nusu kikombe (ml 125) changanya na maji ya kawaida nusu kikombe tena kupata ujazo wa robo lita, changanya vizuri mchanganyiko huu na unywe kutwa mara 2 kwa siku 3 hadi wiki 1 kujitibu matatizo ya tumbo kama kuum, kuondoa sumu, kuunguruma, kuhara na hata kutibu malaria.
Madhara ambayo yameripotiwa kutokana na kunywa aloe vera ikiwa freshi kupita kiasi ndani ya tumbo ni pamoja na kuharisha na matatizo kwenye figo.
Namna ya kutengeneza jeli ya aloe vera:
5. Huziimarisha kucha dhaifu
Kwa taratibu pakaa majimaji ya aloe vera juu ya kucha zako sehemu zote juu na chini kila siku na uzitazame baada ya siku kadhaa uone zitakavyokuwa zimerudisha ule uzuri na ugumu wake wa mwanzo.
6. Huondoa Makeup
Kwa usalama kabisa huondoa makeup kwenye jicho na ni nzuri kwa ngozi laini inayozunguka jicho lako.
7. Husafisha ngozi na kuondoa alama zitokanazo na kuungua na jua
Chunusi, ukurutu na kuungua kwa ngozi kutokana na jua vyote hivi vinatibika kirahisi kwa kutumia aloe-vera. Pakaa mara 2 hadi 3 kwa siku katika ngozi mpaka uone umepona kabisa. Mu-aloe vera pia una sifa ya kupoza kama ilivyo menthol ambayo unaufanya Mu-aloe vera kuwa dawa ya asili nzuri zaidi katika kutibu alama zitokanazo na kuungua na jua.
8. Ni jeli ya asili ya kunyolea na baada ya kunyoa
Aloe Vera ni dawa ya asili katika kutibu michubuko asante kwa vimeng’enya vyake ambavyo huwa na kiasi kingi cha maji ambayo ni mhimu kuzuia kukauka kwa ngozi. Wakati unanyoa ndevu pakaa jeli ya aloe vera na hata baada ya kunyoa pakaa kama after shave jel kuzuia na kuponya michubuko itokanayo na kunyoa.
9. Huondoa makunyanzi na mikunjo ya ngozi
Ngozi hupenda sana Vitamini C na E ambazo zote zinapatikana katika aloe vera na kusaidia kuboresha unene wa ngozi na kuiacha katika hali ya umajimaji. Ikiwa utachanganya jeli ya aloe-vera na mafuta ya asili ya nazi utapata krimu nzuri ya kuongezea viinilishe, mafuta mhimu na unyevunyevu katika ngozi.
Jeli ya Aloe Vera hupenyeza katika ngozi kwa haraka mara nne zaidi ya maji ya kawaida na sifa yake ya kulainisha ngozi husaidia ngozi kubaki na unyevunyevu muda wote.
10. Hutibu homa, malaria na mafua
Jeli ya Aloe Vera huongeza kinga ya mwili. Mu-aloe-vera una viinilishe vingi sana mhimu kwa afya ya binadamu. Ina Vitamini A, B, C, na E. Mmea huu una orodha ndefu ya madini mhimu kwa mwili na vimeng’enya vingine mhimu.
11. Vitamini B12 kwa wale wasiotumia nyama (Vegans)
Matumizi makuu ya aloe vera kimatibabu ni kusaidia na kuboresha uundwaji wa bakteria wazuri. Kwa kuongezea aloe vera huwa na jumla ya madini ambayo bakteria huyahitaji katika kutengeneza Vitamini B12.
12. Huongeza nguvu mwilini
Matumizi mengine ya kitabibu ya mmea wa mu aloe vera au mshubiri kwa kiswahili chake hasa, ni kuongeza usawa wa nguvu mwilini. Hii ni kutokana na uwepo wa vitamin b 14 na viinilishe vingine ambavyo husaidia kubadili asilimia kubwa ya chakula katika tumbo lako na kuunda nguvu.
13. Huondoa mba kichwani
Changanya jeli ya asili ya aloe vera na shampoo yako, dakika chache kabla ya kwenda kulala pakaa vizuri mchanganyiko huo kwenye nywele zako na uache zikauke kidogo na usafishe nywele zako asubuhi.
14. Huondoa maumivu wakati wa hedhi
Changanya jeli ya Aloe vera na pilipili manga ya unga kidooogo, meza kijiko cha chakula kimoja mara tatu kwa siku kila siku hadi maumivu yatakapoacha.
15. Hulainisha nywele
Jeli ya Aloe vera ni nzuri katika kutibu tatizo la nywele kujisokota na ni mbadala mzuri kwa bidhaa nyingi za madukani zenye gharama kwa ajili ya nywele.
16. Ni dawa ya asili ya kusafishia mdomo
Changanya jeli ya aloe-vera ml 100, vijiko 3 vya chai vya baking soda, maji ml 100 na kijiko 1 kidogo cha juisi ya limao. Changanya vizuri vyote kwa pamoja na utumie kama dawa yako ya asili ya kusafishia mdomo.
17. Hutibu matatizo katika mmeng’enyo wa chakula
Juisi ya Aloe vera ni nzuri sana katika kurekebisha matatizo katika mmeng’enyo wa chakula, hurekebisha kuvurugika kwa tumbo na kiungulia. Itumie kama ilivyoelezewa kwenye kutibu matatizo ya tumbo hapo juu namba 4.
18. Hushusha lehemu (Cholesterol)
Tafiti zimeonyesha kuwa kunywa juisi ya aloe vera kwa kipindi kirefu kunaweza kushusha kiwango cha lehemu mwilini. Itumie kama ilivyoelezewa kwenye kutibu matatizo ya tumbo hapo juu namba 4.
19. Hutibu chunusi
Aloe Vera huondoa chunusi kwa kuziondoa seli zilizokufa katika ngozi na hivyo kuvifungua vishimo katika ngozi na kuondoa mafuta yaliyoganda katika hivyo vishimo. Pakaa jeli ya aloe vera moja kwa moja katika eneo lililoathirika na chunusi. Pia makovu yaliyoachwa kutokana na chunusi yanaweza kuondolewa kwa kupakaa jeli ya aloe vera pekee.
20. Hutibu ukurutu na upele
Ukurutu ambao ni matokeo ya juu ya tetekuwanga kwa kawaida hutokea kwa watu wazima wenye kinga ya mwili pungufu. Aloe Vera inaweza kutumika kutibu tetekuwanga zinazosababishwa na kirusi aina ya herpes virus. Kwa kupakaa jeli ya aloe vera moja kwa moja kwenye sehemu zilizowazi hutanua mishipa ya damu jambo linalosaidia kutibu vidonda.
21. Huzuia ngozi kuunguzwa na jua (Sunscreen)
Kupakaa jeli ya Aloe Vera katika mwili hulinda ngozi dhidi ya miale yote ya jua kutua moja kwa moja kwenye ngozi na hivyo kukufanya usizeeke mapema, pia ni dawa nzuri kwa ngozi inayofubaa.
22. Hulainisha sehemu kavu za siri
Aloe Vera hufanya kazi kama kilainishi bora kabisa cha asili katika maeneo ya siri kwa jinsia zote mbili na kutoa unyevunyevu wa asili.
23. Hutibu vidonda katika mdomo
Mu Aloe vera unazo vitamini na asidi amino ambazo husaidia kuzitengeneza upya tishu zilizoharibika. Tafiti zimeonyesha kuwa watu wanaosumbuliwa na vidonda mdomoni waliotumia jeli ya aloe vera walifanikiwa kutibu karibu asilimia 50 haraka zaidi kuliko wale ambao hawakutumia jeli ya aloe vera.
24. Hutibu maambukizi katika uke
Unaweza kutibu maambukizi katika uke kwa kupakaa jeli ya aloe vera kwa nje na kwa kuinywa jeli kupata faida yake ya kutibu fangasi. Mililita 70 mpaka 100 za jeli ya aloe vera kila siku zinaweza kusaidia kutibu maambukizi na fangasi katika uke na ikiwa utaendelea kuinywa kwa muda mrefu kunaweza kuzuia maambukizi zaidi kutokujirudia baadaye.
Pia hutumika kurudishia uke uliolegea, pakaa tu huko jeli fresh ya aloe vera kila siku na hutakawia kuwa binti mdogo tena. Dawa nyingine kwa ajili hii ya kurudisha uke uliolegea ni unga wa mbegu za maembe.
25. Husaidia kukaza uke
Wakati sisi wanaume tukilaumiwa kuwa na vibamia, wanawake nao huwa wanapatwa na tatizo la kuwa na uke mkubwa kiasi kwamba unaweza kuhoji huu ni uwanja wa taifa au!. Basi kina mama msiache kunipa zawadi kwa hili. Ikiwa misuli ya uke wako imelegea na uke umekuwa mkubwa na unahitaji kuubana na kuwa mdogo tena basi unachohitaji ni mshubiri freshi. Chukua aloe vera fresh, chukua jeli yake (maji maji yake) na upakae huko ndani kutwa mara 2 mpaka 3 kwa wiki 3 mpaka mwezi mmoja hivi utaona umekuwa kama binti mdogo tena na mme atabaki na wewe. Kazi ni kwenu.
26. Husaidia wawindaji
Wawindaji wa wanyama katika barani Afrika mara kwa mara hupakaa jeli ya aloe vera katika miili ili kupunguza kutokwa jasho na kuondoa harufu yao ya asili katika mwili isisikike na wanyama.
27. Suluhisho kwa watafuna kucha
Burashi kucha za mtoto anayependa kutafuna kucha na jeli ya aloe vera, ile radha ya uchungu katika aloe vera kutamfanya aache kuzitafuna kucha zake.
28. Hutumika katika kupunguza uzito
Watafiti wameweza kugundua kuwa kunywa juisi ya aloe vera husaidia kupunguza sukari kwenye damu jambo mhimu kwa wale wenye kisukari cha aina ya pili. Wanasayansi wanaamini kuwa kuweka kiwango cha sukari chini hupunguza uzito.
29. Hutibu upungufu wa damu (Anemia)
Kunywa jeli ya aloe vera kunasaidia uzalishaji zaidi wa seli nyekundu za damu katika mwili wako na hivyo kutibu tatizo la kupungua kwa damu.
30. Huondoa maumivu ya mishipa
Kutokana na sifa yake ya kutibu uvimbe, unaweza kutibu uvimbechungu (inflammation) katika maungio yanayopelekea maumivu katika mishipa kwa kupakaa jeli ya aloe vera katika eneo unalosikia maumivu.
31. Hutibu maumivu katika sikio
Matone kadhaa ya aloe vera yakinyunyizwa sikioni yanaweza kuleta nafuu kubwa kama unapatwa na maumivu katika masikio. Hii ni nzuri pia kwa masikio yanayotoa usaha na maumivu mengine katika masikio.
src fadhili blog
ni msaada mkubwa sana
ReplyDelete