Saratani ya matiti kwa wanaume ipo
Moses Musonga: Kawaida wanaume hawana matiti lakini mimi ninayo
Saratani ya matiti inapozungumziwa, moja kwa moja kinachowaingia fikirani watu wengi huwa ni wanawake. Lakini wajua kuwa ugonjwa huu huwaathiri wanaume pia?

Moses Musonga, 67, ni mmoja wa wanaume wanaougua saratani ya matiti.
Aligunduliwa kwamba alikuwa anaugua ugonjwa huu mwaka wa 2013 yake kutembelea hospitali ili kupata matibabu kutokana na uvimbe uliotokea kwenye titi lake la kulia.

Advertisement

Anasema kuwa alipuuza uvimbe huo uliotokea, maana ulikuwa mdogo na hakudhani kuwa ulikuwa na madhara yoyote.
Lakini baada ya muda, uvimbe huo ukawa mkubwa, hali iliyompelekea kutafuta ushauri was daktari.
◾Mambo 10 yanayopunguza hatari ya kuugua saratani
◾Kwa nini Saratani nyingine ni 'hatari'
◾Kuvimbiwa tumbo inaweza kuwa dalili ya saratani
Alitembelea hospitali ya taifa ya Kenyatta jijini Nairobi na baada ya kufanyiwa uchunguzi, akaelekezwa katika hospitali ya Nairobi ili kufanyiwa uchunguzi zaidi.
Uchunguzi ulionyesha kuwa alikuwa anaugua saratani ya matiti, na akashauriwa aanze matibabu mara moja.
"Nilifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe huo, baada ya kidonda kupona, nikaja Nairobi kufanyiwa tiba kemia kwa miezi sita baada ya kila wiki tatu".
Kwa kipindi cha miezi sita, Moses alianza matibabu hayo maalum ya kudhibiti viwango vya seli zinazosababisha ugonjwa wa saratani. Na baada ya matibabu hayo, hali yake ya afya ikaimarika.
"Nilimaliza tiba kemia mwaka wa 2014, nikapona, nikaona kwamba nimepona na nikafikiri kwamba nilikuwa huru. Lakini nilishauriwa kwamba nirudi kufanya tibaredio (matibabu kwa njia ya eksirei yaani Radiotherapy) na tiba ya homoni (Hormonal Therapy)," ameambia BBC.
"Hivyo viwili ni kama nilipuuza, kwa sababu ya ukosefu wa fedha. Kwa sababu fedha nyingi sana za matibabu nilipungukiwa na pesa, nikauza kila kitu nyumbani. Nikawa nimechoka, na mwili nao ukachoshwa na matibabu makali uliyokuwa unapokea."
Daktari alimshauri aanze kipindi cha matibabu ya pili ambayo inajulikana kama Radiotherapy. Hii ni matibabu ya kuua na kumaliza seli za saratani katika mwili.

Moses Musonga ameugua saratani ya matiti kwa miaka mitano sasa
Image caption

Kwa sababu ya ukosefu wa fedha, Moses hangeweza kuendelea na matibabu ya Radiotherapy.
"Baada ya miaka mitano, nikaanza kupatwa na mfadhaiko hadi nikawa naona kwamba nachungulia mlango wa mauti."
Moses alianza kuugua tena.
Alikuwa akipatwa na mfadhaiko na msongo wa mawazo na kushindwa kupumua hali iliyompelekea kutafuta huduma ya daktari tena.
"Wakagundua kwamba kuna kitu kwa mapafu. Wakasema inaweza kuwa saratani tena. Nikashtuka, nikapatwa na mfadhaiko. Nikashindwa hata kutembea, pumzi ikapungua "
Daktari alitolewa mjini Nairobi akachukua sampuli kutoka kwenye mapafu yake ili kufanya uchunguzi zaidi.
◾Utafiti: Vyakula vya kusindika huleta saratani
◾Sababu ya Waafrika kutatizika kuzuru nchi za Afrika
◾Wasiwasi kuhusu mbegu za kiume Ulaya na Marekani
◾Mifuko ya Plastiki hatari kwa afya yako
Baada ya wiki moja na nusu utafiti ulithibitishwa kwamba ni saratani lakini ni ile ya matiti ilikuwa imehamia kwenye mapafu.
"Nilihofia kweli, kwa sababu matibabu hayo yalikuwa makali kweli kweli na madhara yenyewe ambayo nilipitia wakati huo, nikahofia tena kwa sababu wananipa dawa ambayo ina nguvu kuliko ya kwanza, sasa sijui kama nitaweza kwa sababu pia niko na ugonjwa msukumo wa moyo na pia wa kisukari. Niliomba Mungu anisaidie ili nimalize hiyo safari ".

Saratani mwiliniHaki miliki ya picha Getty Images
Mwalimu huyu wa chuo cha mafunzo ya dini cha Kaimosi magharibi mwa Kenya anasema kuwa hali hii imebadilisha maisha yake Kwa kiwango kikubwa na matibabu yamemgharimu pesa nyingi.
"Nimeuza ngombe, nimeuza mashamba yangu, nimeuza kila kitu, lakini familia wamesimama nami. Hasa zaidi wale ambao wana mapato angalau. Wengine hata walichukua mikopo ili wagharamie matibabu yangu."
Ugonjwa wa saratani ya matiti kwa wanaume bado haujaeleweka katika jamii licha ya kwamba wanaume wengi wanaweza kuupata, tatizo ni kwamba, hugundulika wengi wakiwa wamechelewa zaid.
Hii ni kwa sababu wanaume wengi hawapendi kwenda kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.
Kuna tofauti kati ya wanaume na wanawake?
Daktari Catherine Nyongesa wa kituo cha matibabu ya saratani cha Texas Cancer Centre jijini Nairobi anasema kuwa saratani ya matiti ni mojawapo ya aina ya saratani inayoongoza nchini Kenya, lakini wanaume wanaathirika kwa asilimia 3 pekee ikilinganishwa na 96% kwa wanawake.
Mtu yeyote anaweza kuugua.
"Kile kinachosababisha saratani hii kwa wanaume bado hakijabainika, lakini kinakisiwa kuwa ni hali ya mazingira ama pia mtu anapopfikisha umri wa zaidi ya miaka thelathini".
Vijana wa kiume wa chini ya miaka 30 huwa nadra sana kwao kuugua.
Daktari Catherine anasema kuwa mwanamume anapaswa kuwa makini na maumbile ya mwili wake.
"Ni vizuri mwanaume ajue matiti yake vile yanakaa kwa kawaida, akiona tofauti yoyote kama uvimbe hivi, ngozi kubadilika, titi moja kuwa kubwa kuliko jingine, uvimbe uliyo kwenye titi kuuma, basi ni dalili kwamba anafaa kupimwa," anasema.
Mtaalamu huyu wa saratani ya matiti amesema kwamba dalili na matibabu ya saratani kwa wanaume na wanawake ni sawa

Post a Comment

Previous Post Next Post